Aliyetolewa macho yawezekana yeye ndiye mkosaji

7.inasemekana jamaa alitibiwa bila PF3, je hiyo imekaaje?

8.kama huyo scorpion wanasema jamaa ni mtoa macho mzoeefu mbna mpaka sasa hakuna wengne waliojitokeza kuwa walifanyiwa hivo

Sipati picha aibu watakaoipata walomtetea jamaa usiku na mchana siku watakapoambiwa jamaa ndo mkosaji,na mheshimiwa wetu wa faster faster sijui atatoka na gia gani katika hiyo aibu!!!,tusiwe wepesi kuhukumu jaman

Ni ajabu sana hukumu imeshatolewa wakati upepelezi unaendelea. Radios zetu na social media zinajua sana kuhukumu.
 
Ni kosa gani ambalo adhabu yake ni kutolewa macho? Hata kama ni street justice..... hii imezidi.
Scorpion hana Janja ya kuukwepa mkono wa nyapara
Wezi wakichomwa moto kwa kuvishwa tire au kukatwa mikono au miguu mbona huwa mnaona kawaida..... Sasa huyo mwizi kutolewa watu povu kibao
 
Mtu anakutolea kisu ili akuchome unawezaje kumfikisha mahala husika kwa muda huohuo? Au unamaanisha angemruhusu bila kufanya chochote achomwe ndipo apeleke mahala husika?
Kwa sisi tunaoishi Dar es salaam uswahilini suala la vijana wahuni kutoleana visu ni jambo la kawaida sana, lakini hili la kutoboana macho ni jambo La kushangaza mnoo na la kutisha pia!
 
Ukiwa kwenye hiyo nafasi...utakumbuka ulivokuwa unacharanga watu mapanga kama unakata nyama mpaka kuwasababishia vilema vya maisha au hata kifo na wakati huohuo unawaona watoto wake wakihangaika kwa kukosa malezi...sio sawa kutobolewa macho lakini kabla ya kujua chanzo cha tatizo si vema kwa wenye mamlaka kulibeba kindakindaki..
Waliolibeba wamelibeba kwa huruma zao za mioyo yao! Mamlaka husika ni Mahakama tu na ndio watakaolibeba kindaki ndaki watupe ufumbuzi wa maswali yako juu ya janga hili kwa kijana mwenzetu
 
Kwanza sijahalalisha adhabu mkuu ila nimeongelea mazingira halisi na hasira za kibinadamu

Kama yesu mwenyewe ana hasira na mfano ni pale alipokuta watu wanafanya biashara katika nyumba ya ibaada unasoma alichokifanya?

Nielewe sasa hasira na inabid tujue story ndo tu judge kwa uzito wake
Wewe kama si mshirika wa scorpion basi ni ndugu yake! Hasira za hivi mkazifanyie kwenye miili ya mama zenu msituletee upuuzi wa kufananisha yesu na utumbo wako huu,Na usubiri muda ufike jibu litapatikana ya nini kujipotezea muda kutaka kutushawishi kuwa Said alistahili alichofanyiwa!!!?
 
mahakama ina njia zake za kufanya kazi ambazo si kama mahakama za social media . Pili tusije shangaa mtu kashinda kesi cku hyo na kuonekana aliefanyiwa kitendo na yy ana kesi ya kujibu kwani siku zote kunaitajika mashaidi na lazima muhusika atambuliwe na mshitaki kingine napata wasiwasi je toka bwana said kapata ajari mpaka kapona alikwenda police??? na napata wasiwasi hv mtu mwenye mafunzo ya ziada kwenye mapigano akuchome visu wakati ana uwezo wa kukudhibiti bila ya kutumia siraha nina waswas na kile kisu kilikuwa cha ..............
 
Ivi ni nani mwenye kosa mendaji au mtendewa Kwa maana mtendewa tmeona alichofanyiwa na kama ilikuwa ni mhalifu he ni kwann apigwe na MTU mmoja badala ya wananchi wote? Kosa analo alomtoa macho uyu jamaa
 
Maswali yangu kwenu mliomhukumu huyu mtuhumiwa kabla hata ya hukumu halali ya mahakama. Kwanza niseme kuwa watanzania tuache kufanya mambo kwa mihemuko na kutoa hukum haraka,mimi binafsi sitaamini kama huyu jamaa kaonewa mpaka nijibiwe maswali haya

1. Baada ya kutolewa macho kwanini hakwenda kushitaki kama yeye alikuwa na haki mpaka media zimemfata ndio kasema

2. Haiingii akili kusema eti watu wote waliokuwapo wakati anatolewa macho hawakuwa na uwezo wa kumsaidia kwa kumkabili scorpion, Je kwanini hawakumsaidia wala kwenda ku report polisi?

3. Je, watu wanaomzunguka huyo Said mbona hawajitokezi kumwongelea kwa mema yoyote na wala kumsitikia,je ni kwakuwa na wao walishamchoka?

4. Jina la scorpion ni kama majina mengne ya kibabe kama warrior nk ambayo vijana hupenda kuyatumia,sasa yeye ana uhakika gani kuwa mtuhumiwa ndio scorpion alomtoa macho na kama alikuwa anamfahamu kwanini hata nduguze hawakwenda kushitaki?

5. Kuna shutuma kuwa yeye mtendwa alifuatwa kwa amani akawa anaulizwa juu ya wizi uliotokea ila ghafla aka-panic na kutoa kisu ila akazidiwa ujanja,je ni kweli na kama kweli kama hakua na hatia kwanini atoe silaha mapema?!

6. Kuna sehemu niliona mama anasema anataka amtolee jicho lake moja ampe,je kama ana uchungu kiasi hiki kwanini hakuwahi kushitaki jambo hilo lililomfika mwanae?
Tayari hivyo vi misaada alivyopewa mmeanza kuona wivu wanaume wa daslam buwana
 
mkuu mawazo yako yameongozwa na ushabiki na si hali halisi mfano #2 ina kinzana na # 5 kama haikuingii akilini mtu kutobolewa macho mbele ya watu, inakuwaje ikuingie akilini alitoa kisu kumchoma jamaa akamuwahi (kama una kubali hili, lazima ukubali kuwa watu walikuwepo wakaona akitaka mchoma kissu akashindwa nguvu akatobolewa macho mbele ya hao watu)

tofaut na hapo umeongozwa na hisia sio uchambuzi makini
 
Kwa hiyo hata wewe ukikosea/ukiwa na makosa ni halali mtu uliyemkosea akutoe macho kikatili uwe kipofu?....

Vyovyote ilivyokuwa, hakuna mtu mwenye haki ya kumpa upofu mwenzake kikatili eti kwa sababu amekosea/ni mhalifu....

Kama Said alikuwa na makosa, angeepelekwa kwwenye vyombo vya sheria na sio kufanyiwa ukatili huu wa kutobolea macho.....Faanya ujiweke wenye nafasi ya Said (kwamba wewe ndiye SAID na umetobolewa macho na kupata upofu)...
Mkuu,

Nadhani hujaelewa uzi nachelea kusema umekurupuka. Hakuna anae halalisha unyama na huenda ni USHETANI wa Bwana Scorpion lakini Dhima ya Uzi ni kufahamu jeeeee, huenda Bwana said ndie alieamsha hasira za Bw Scorpion.

Wanasema in any action there is reaction sasa ukila ujue utaenda chooni.
 
Stories zenu hakuna anayetaka ...

Kama Jamaa ni mkosaji hatutaki pia kujua

Tunachojua hapa ni KUMJERUI vibaya kiasi cha kutaka kumtoa roho..

sheria INA ruhusu kila Mtu kutuhumiwa na kutuhumu .

Nikushauri mtoa Uzi ukasaidie Polisi umtetee SCORPION hatuwezi jua maslah yake kwako huku hakuna mahakama ..kapande Mahakamni plz

Inakuuma sana mtu kushtakiwa kwa kumtoa macho mwenzio ila haikuumi mwenzako kutolewa macho

Ndo watanzania mliobaki ..mnajitia ujuaji tu ..Kasimame mahakamani utete hili ..inawezekana UKAMTOA SCORPION
 
Mtoa uzi unamatatizo ya uelewa na fikra ila kama unaona ishu haipo ivo basi kamtoe ndani uyo alomtoboa mwenzie macho afu umfunge saidi ally
 
Maswali yangu kwenu mliomhukumu huyu mtuhumiwa kabla hata ya hukumu halali ya mahakama. Kwanza niseme kuwa watanzania tuache kufanya mambo kwa mihemuko na kutoa hukum haraka,mimi binafsi sitaamini kama huyu jamaa kaonewa mpaka nijibiwe maswali haya

1. Baada ya kutolewa macho kwanini hakwenda kushitaki kama yeye alikuwa na haki mpaka media zimemfata ndio kasema

2. Haiingii akili kusema eti watu wote waliokuwapo wakati anatolewa macho hawakuwa na uwezo wa kumsaidia kwa kumkabili scorpion, Je kwanini hawakumsaidia wala kwenda ku report polisi?

3. Je, watu wanaomzunguka huyo Said mbona hawajitokezi kumwongelea kwa mema yoyote na wala kumsitikia,je ni kwakuwa na wao walishamchoka?

4. Jina la scorpion ni kama majina mengne ya kibabe kama warrior nk ambayo vijana hupenda kuyatumia,sasa yeye ana uhakika gani kuwa mtuhumiwa ndio scorpion alomtoa macho na kama alikuwa anamfahamu kwanini hata nduguze hawakwenda kushitaki?

5. Kuna shutuma kuwa yeye mtendwa alifuatwa kwa amani akawa anaulizwa juu ya wizi uliotokea ila ghafla aka-panic na kutoa kisu ila akazidiwa ujanja,je ni kweli na kama kweli kama hakua na hatia kwanini atoe silaha mapema?!

6. Kuna sehemu niliona mama anasema anataka amtolee jicho lake moja ampe,je kama ana uchungu kiasi hiki kwanini hakuwahi kushitaki jambo hilo lililomfika mwanae?
Ukiwa na makosa ndiyo unatakiwa utolewe macho?
 
Back
Top Bottom