Aliyemuua, kumtupa mwanafunzi UDOM ahukumiwa kunyongwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
"Ni kweli nilimuua Happiness na nilimuua Kigamboni mji mpya nyumbani kwetu kwenye chumba ninacholala,” hii ni sehemu ya maungamo ya muuaji wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), Happiness Fredrick.

Idrisa Mwangobola ambaye Ijumaa iliyopita alihukumiwa kunyongwa alieleza hayo katika maelezo aliyoandika polisi, “Kabla sijamuua nilinunua kinywaji aina ya juisi na kumwekea kidonge cha usingizi, ili alale niweze kumuua kirahisi.”

Happiness aliuawa Machi 18, 2019, siku aliyokwenda kununua tiketi katika basi la Kimbinyiko International Coach ili siku inayofuata arudi Dodoma chuoni, lakini hata baada ya kukata tiketi hiyo hakurejea nyumbani kwao.

Hii ilimtia shaka baba yake aitwaye Fredrick Francis ambapo alimpigia simu lakini haikupokelewa, badala yake ulitumwa ujumbe wa maandishi (SMS) ukisomwka “Niko kwenye wakati mgumu. Niombeeni, niagieni kwa wadogo zangu. Nawapenda”. Baada ya kupokea ujumbe huo, alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi ambao walimjulisha kuwa kuna mwili umepatikana eneo la Sigara Relini, hivyo Polisi walimchukua hadi Hospitali ya Temeke na kuutambua ni wa mwanae.

Muuaji alikamatwa Machi 21,2019 katika Kanisa Katoliki la Buza, Jijini Dar es Salaam alipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa marehemu na hii ni baada ya kutiliwa shaka juu ya namna alivyokuwa na taarifa za mwanzo za mauaji hayo.

Ushahidi uliotolewa mahakamani unaeleza kuwa baada ya mtuhumiwa kukamatwa na kufanyiwa mahojiano mbele ya mama yake mzazi, alikiri kumuua Happiness na kwenda kutupa mwili wake Buza Sigara.

Alivyotekeleza mauaji

Shahidi wa tisa wa upande wa mashtaka, Askari Polisi mwenye namba E 6053 Koplo Peter, ndiye aliyeandika maelezo ya onyo ya mshtakiwa mbele ya baba yake mzazi, ambapo alikiri kumuua Happiness na kueleza hatua kwa hatua.

“Nilimuua Happiness Fredrick Mbonde na nilimuulia Kigamboni mji mpya nyumbani kwetu kwenye chumba ninacholala. Kabla sijamuua nilinunua juisi na kumwekea kidonge cha usingizi, ili alale niweze kumuua kirahisi.

“Lakini hakulala ila mwili wake ulilegea, ndipo nilimkaba kwa kutumia mikono yangu hadi akafariki na kisha nilichukua simu zake mbili, moja ya tochi na ndogo aina ya Tecno na vitu mbalimbali kwenye mkoba,” alieleza na kuongeza;

“Baada ya kumaliza mambo yote wakati nambeba niliona ni mzito, mama aliniona akaja kunisaidia kubeba na kufungua mlango wa gari wakati tuko kwenye pilikapilika za kumweka siti ya nyuma nilimpiga kiwiko cha jicho…”

“Aliumia. Kisha nilitumia gari hilo la nyumbani na kumpeleka Yombo Sigara na kupaki pembeni mwa nyumba moja. Nilishuka ndani ya gari nikaenda msikitini kusali, kisha nikarudi na kufungua mlango nikavuta maiti hadi chini”

“Kisha nilirudi nyumbani. Kusema ukweli mama mzazi anajua ukweli na ndiye alinisaidia kumuingiza marehemu kwenye gari. Wakati ananisaidia hakujua kama amefariki, ila mimi nilijua,” alieleza.

“Sababu kubwa iliyofanya nimuue mpenzi wangu huyo nilibaini ananisaliti katika mapenzi yetu na hasa kilichonitia hasira zaidi ni wakati nikiwa naye alipokea simu kutoka kwa mpenzi wake wa zamani, Albert ambaye nilikuwa nahisi bado ana mahusiano naye,” alieleza Mwangobola katika maelezo yake hayo.

Katika utetezi wake uliokataliwa na mahakama, Mwangobola alidai Happiness alikuwa rafiki tu na hakuwa mpenzi wake na kwamba alikamatwa Machi 21, 2019 katika ibada ya mazishi iliyofanyika Buza kanisani.

Alidai alikamatwa kwa kuwa kifo cha Happiness hakikuwa cha kawaida na kwa sababu walikuwa marafiki, lakini alikana kuandika maelezo ya kukiri bali anakumbuka alitia saini nyaraka kwa ajili ya kupewa dhamana.

Hukumu ya kunyongwa

Julai 28, 2023, Jaji Ephery Kisanya wa Mahakama Kuu Dar es Salaam na nakala yake kupatikana jana katika tovuti ya mahakama kwa ajili ya kuchapisha uamuzi, sheria na kanuni bure mtandaoni.

Katika hukumu hiyo, Jaji Kisanya alisema hakuna shahidi hata mmoja aliyetoa ushahidi akisema alishuhudia mshtakiwa akimuua Happiness, lakini amehusishwa kutokana na kukiri kwake kwa mdomo na katika maelezo aliyoyaandika polisi. Jaji Kisanya alisema upande wa mashtaka umethibitisha shitaka dhidi ya mshtakiwa, hivyo anamtia hatiani na kueleza kwa mujibu wa sheria, adhabu ya kosa la kuua kwa kukusudia ni moja tu nayo ni kunyongwa hadi kufa.

MWANANCHI
 
endeleen kunyonga watu kwa kulipiza kisasi kwan haijaandkwa usihkumu usije uhukumiwa?
 
Bitabu vyote vya dini vinasema uzinzi na uasherati ni chafu msiusogelee, nyinyi vijana hamsikii.

Fikiri upo na mwanamke aua na mwanamme hajaoana halafu umauti wake ndiyo umefika chumbani upo nae? Mpaka uje kujinasuwa kuwa hujamuuwa, ushapoteza muelekeo wa maisha yako to the worst.

Kijana usimvulie chupi mtu yeyote ambae hamjaowana.

Msidanganywe na picha za Hollywood wale ni waigizaji tu, siyo uhalisia.
 
Back
Top Bottom