Aliyekuwa Gavana wa Nigeria, James Ibori kwenda jela miaka 13 kwa ufisadi huu

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
Mhasibu wa zamani wa duka la DIY mjini London ambaye alikuja kuwa gavana nchini Nigeria amefungwa jela miaka 13 kwa kufanya udanganyifu wa fedha karibu £50m ($77m).

James Ibori, gavana wa jimbo la Delta alikiri kujihusisha na makosa 10 ya ulaghai na biashara ya fedha haramu.

Mahakama ya Southwark Crown ilielezwa kuwa kiasi cha fedha alichoiba kutoka kwa watu wa jimbo la Delta kilikuwa ‘hakihesabiki’.

Ibori, aliyeepuka kukamatwa Nigeria baada ya kundi la mashabiki wake kuvamia kituo cha polisi, alikamatwa Dubai mwaka 2010.

Alihukumiwa Uingereza ambako alishtakiwa kwa ushahidi uliotolewa na Polisi wa London.

Mojawapo ya mashtaka yake Ibori alikiri kuhusika na udanganyifu wa kiasi cha $37m (£23m) kuhusu mauzo ya hisa za jimbo la Delta kwa kampuni ya simu nchini Nigeria iliyobinafsishwa ya V Mobile.

Alikuwa gavana wa Jimbo la Delta kati ya Mei 1999 na Mei 2007.

Wakili wa upande wa mashataka Sasha Wass, aliiambia mahakama kuwa Ibori "kwa makusudi na kwa mpangilio " aliwalaghai watu waliomchagua kuwawakilisha.

Mahakama pia iliarifiwa kuwa alikuja Uingereza miaka ya 1980 na kufanya kazi kama mhasibu wa duka la Wickes DIY huko Ruislip, kaskazini magharibi mwa London.

Kuinuka na kuanguka kwa James Ibori 1958: Alizaliwa Jimbo la Delta, Polisi wa Uinegereza wanaamini.

1980: Alihamia Uingereza

1991: Alishtakiwa kwa kuliibia duka la DIY, Wickes

1992: Alihukumiwa kwa udanganyifu............

FULL STORY: << GAVANA ATIWA JELA>>

 
Back
Top Bottom