Alipokuwa akihutubia wakuu wapya wa Wilaya alisema haamini katika watu kujilundikia vyeo viwili

Let me now declare Unequivocally,Unambiguously,without prevacation or Circumlocution that John Magufuli is such unprincipled,Inconsitent,Inept,Incompetent and Selfish Leader.

Ben Saanane

Baptism of fire!

Mtaongea lugha zote lakini no more juice Magogoni!
 
Kilichonifurahisha zaidi Jana katika tukio la Dodoma ni kitendo cha magu kupata ushindi Wa asilimia 100!
Mzee wangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa "kosa lako ni kutokuwa na kosa" yaani wahumbe wote wameridhika na magufuli!
Wabunge waliotumia nguvu kubwa kupata nafasi hizo ili waule kupitia wadhifa huo kwa safari na semina ambazo sasa hazipo, nao wameunga mkono asilimia 100? Hata kitwanga!
Tumbuatumbua yote kwa mifano ya akina mama malechela na vita kawawa nao walipiga kura ya ndio!

Hata sadam Hussein hakupata ushindi Wa hivi
Duu..! Big up kwa uchambuzi wa haja
 
Article ndefu yenye false cause ambayo hitimisho lake ni pumba tupu.

Kwa hiyo ulitaka Majaliwa akae wakati utaratibu wa NEC ni kusimama wakati viongozi wakuu wanapoingia ndani ya ukumbi wa mkutano.

Ulitaka wajumbe wabaguane sehemu ya kukaa kutokana na makundi ya wagombea?

Naona mmeanza kubatizwa kwa moto!

Kamsaidie Sumaye kupiga kampeni za mchangani ili asije kudondoshwa na mbunge mwenye elimu ya hapa na pale, Kubenea katika nafasi ya unyenyekiti wa kanda.
 
Shida ya CCM ni pale ambapo hawataki free and fair game wanataka kutawala wao tu kitu ambacho hakipo hata mzazi ufikia wakati anaacha watoto wamshauri na wamlee mana uwezo hupungua. Sasa wakifanye wao nyoka mvua magambaz waone walijaribu kipindi fulani ikashindikana ndio maana wenye Akili akina Sumaye na Laigwan Lowassa bila kumsahau mzee wa busara kadi namba nane mzee Kingunge wakaamua kuondoka mapema wakaachia lichama Lao. Sasa ona jinsi ufalme unavyo fitiniana wenyewe kwa wenyewe kwa mujibu wa maandiko utaanguka tu.
 
Let me now declare Unequivocally,Unambiguously,without prevacation or Circumlocution that John Magufuli is such unprincipled,Inconsitent,Inept,Incompetent and Selfish Leader.

Alipokua akihutubia wakuu wapya wa Wilaya alisema haamini katika watu kujilundikia vyeo viwili

Yeye Amekubalije kuwa Mwenyekiti wa Chama wakati huo huo ni Rais? Si angewaachia wengine?

Vipi mbona anasema Sekretarieti ya CCM itaendelea ina Maana Nape Katibu wa Itikadi na Uenezi ambae ni Waziri,Asha-Migiro ambae ni Balozi ataendelea?

Sifa kuu ya Mnafiki ni kutoaminika na kutekeleza anachoahidi.

Anatangaza angekua Mwenyekiti wa Chama watu walipoimba tuna Imani na Lowassa angewapoteza Robo au nusu yao. Mbona Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anaonekana kwenye hii video nitakayoweka hapa Chini yupo karibu na Sophia Simba .Mbona akina Jenista Mhagama wanaonekana hapa chini na ni wateule wake.Sasa awafute kwenye Uongozi .Inaonesha jinsi anavyoongea bila kufanya utafiti,chuki,visasi na ubabe dhidi ya wale asiokubaliana nao.Huu ni udhaifu na incompetence ya hali ya juu.

Lile Bonanza la jana pale Dodoma ni Mwanzo mpya wa Ujenzi wa Mnara wa Babeli

Ngoja tuone jinsi kambi yetu iliyopo humo CCM itakavyofanyia kitu mbaya maana tangazo la Magufuli kuwa hatavumilia wasaliti labda watubu ,tutaona ni wangapi watatubu kwa sababu ya lile Povu alilomwaga jana.

Inaonekana hajui katiba za Vyama,anadhani akiwa Mwenyekiti ni kufukuza tu watu waliochaguliwa kwa kura kikatiba.

Aombe hata uzoefu kwa wale wazee wa jana Cheyo na Lyatonga waliokua wakitangaza jinsi walivyopelekwa Clinic na CCM .Lyatonga aliwahi kufanyiwa mapinduzi akiwa NCCR-Mageuzi.Cheyo alinusurika baada ya kusaidiwa na Msajili wa vyama asipinduliwe na akina Erasto Tumbo na Benson Kigaila,Jidula Mabambasi na kundi la Uasi ndani ya UDP

Wana-CCM mliopo ndani msikubali kuonewa kwa sababu ya chuki na Visasi ombeni msaada kwetu kisirisiri ,tunajua namna ya kushughulika na Wenyeviti Sampuli ya Magufuli na Lyatonga au Cheyo.

Ni rahisi kuanzisha vita ya Uasi ya kichinichini hadi mrudi mezani mjadiliane kwa heshima mkiwa katika Mood ya ama zake ama zenu kuliko kuishi kwa vitisho ndani ya chama ambacho sio mali yake

Msikubali kutishwa kwa sababu eti mlitumia haki yenu ya kikatiba kipindi cha Kampeni kumuunga Mkono Lowassa

Kwa sababu ya hofu yake dhidi ya Lowassa na pia wapinzani wake ndani ya chama alioingia nao tano bora kama Membe na January Makamba anaendesh mikakati ya kuwamaliza kisiasa wao na wafuasi wao.Anazidi kujimaliza na kukimaliza chama chenu

Liliwahi kutolewa andiko la mtu anayeitwa Prof.Mwandosya akidai kuwa Magufuli hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa Tawi na hatauweza uenyekiti wa Chama taifa.Hotuba yake jana tu amedhihirisha.Povu lile la Omo kwa jambo dogo tu je yakija makubwa atauweza mziki?

Fred Mpendazoe,muhurumieni tu hakuna kumjibu sanasana tutaibua zile makala zake RaiaMwema atakua amejianika ni mtu wa aina gani

Mwisho,Jakaya Kikwete nae anazeeka vibaya.Anampiga Vijembe Sumaye kugombea Uenyekiti wa Kanda nzima ya Pwani baaada ya kuwa Waziri Mkuu .Mbona hakusema Sumaye alipogombea Ujumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Hanang huko CCM? Sembuse sasa Uenyekiti wa Kanda?Sumaye sio mchumia tumbo na msaka vyeo.amejitoa kujenga upinzani.

Vipi Dr.Migiro aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na sasa ni Balozi na anawajibika kwa Waziri wa Mambo ya Nje .Je hapo alipanda cheo au alishuka? Mungu huwa hamfichi mnafiki.

Wale waliorudi CCM kwa Upande wetu hatupaswi kuwalaumu.Ni wasaka vyeo na hawakuvipata.Tusiwalaumu ila sisi tuwe na funzo.Sina hata muda wa kuwajadili

Yusuph Makamba nae anadhani anamjenga Magufuli kumbe anamtusi Kikwete.Anadai aliwahi kumtumia Kimemo Magufuli amteue ndugu yake kuwa Mkuu wa Wilaya akamkatalia.Kwa hiyo zile tuhuma kuwa watoto wake walibebwa kupata nafasi fulanifulani akiwa katibu Mkuu wa CCM chini ya Kikwete amezithibitisha maana inaonekana ndio style yake?

Badae kidogo



Victory Ascerta...

Ben Saanane


Dogo hivi unaelewa ulichoandika? Hapo unaongelea Magufuli kuwa Mwenyekiti wa ccm. Huo ni utaratibu wa chama kikatiba. Alichosema kiserikali hataki mbunge awe mkuuwa wilaya. Huo mfumo wa mtu kuwa katika utumishi wa umma kwa nafasi mbili ndiohautaki
 
Majaliwa na Jenista walisimama hawakuimba kuwa wanaimani na Fisadi mkuu Tanzania,walisimama kwa sababu mwenyekiti alikuwa ameingia,nyumbu acha kupotoshaji .

Suala la umuhimu wa kofia mbili ya urais na uenyekiti wa chama kamuulize Thabo Mbeki yeye anafahamu madhara ya kutenganisha kofia ya urais na mwenyekiti wa chama tawala.
 
CHADEMA NA DHANA YA USALITI.
Hakuna anayewasaliti bali Mnajisaliti Wenyewe . Ngoja niwatajie Kwa Uchache ambao Chadema imewaita Wasaliti baada ya Kutoelewana na Mh Mwenyekiti wa Kudumu ndani ya Chama. Said Arfi alikuwa Makamu Mwenyekiti Taifa , Dk Slaa alikuwa Katibu Mkuu Taifa , Zitto Kabwe alikuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa , Samson Mwigamba alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha , Dk Kitila Mkumbo, John Shibuda, Ole Medeye, Mgana Msindai, nk nk nk nk hawa Wote mnawaita Wasaliti hivi kitu gani Wanachokisaliti ktka Chama Chenu ??
Na hao waliobaki Sio wasaliti ? Sumaye, Kingunge, Lowassa
, basila mwanakuzi, hemed Ally, Sango Kasera, Peter Kasera, mzee Mgeja, ole naiko, ole milya, Masha na wengineo sio Wasaliti ?
Chadema semeni tu Ukweli Chama Chenu kina Matatizo ya Kiongozi na Ushahuri ktka Chama .

Mada iliyo mezani ni Magufuli na vyeo vyake pamoja matatizo ya CCM yake.
Anzisha mada yako.
 
Kilichonifurahisha zaidi Jana katika tukio la Dodoma ni kitendo cha magu kupata ushindi Wa asilimia 100!
Mzee wangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa "kosa lako ni kutokuwa na kosa" yaani wahumbe wote wameridhika na magufuli!
Wabunge waliotumia nguvu kubwa kupata nafasi hizo ili waule kupitia wadhifa huo kwa safari na semina ambazo sasa hazipo, nao wameunga mkono asilimia 100? Hata kitwanga!
Tumbuatumbua yote kwa mifano ya akina mama malechela na vita kawawa nao walipiga kura ya ndio!

Hata sadam Hussein hakupata ushindi Wa hivi

Hata Kagame hatashinda kwa style hii.
 
Kuna reform itafanyika kuboresha Muundo wa CCM. Mwenyekiti katoa dondoo jana.
Kwa Mwanasiasa aliyebobea hawezi kushangaa kwa nini Rais Magufuli alikubali nafasi hiyo. Mwenyekiti mpya alieleza kabisa kuwa masuala ya Chama nitofauti ya urais. Urais unaweza kuamua mwenyewe lakini masuala ya Chama hata kama ni mwenyekiti lazima ufuate maamuzi ya chama. Kwa hiyo kutokana na maamuzi ya chama kupitia kamati, jumuia nakadhalika za chama ilishakubaliwa Maadamu Mh. Magufuli Mwanachama wa CCM amechaguliwa kuwa Rais lazima awe Mwenyekiti wa CCM.
Ndugu Ben, kwa maelezo hayo hapo juu huna sababu tena ya kumuita mwenyekiti mpya wa CCM hayo majina mabaya uloyoandika kwa kuzungu.
 
Article ndefu yenye false cause ambayo hitimisho lake ni pumba tupu.

Kamsaidie Sumaye kupiga kampeni za mchangani ili asije kudondoshwa na mbunge mwenye elimu ya hapa na pale, Kubenea katika nafasi ya unyenyekiti wa kanda.

Naona mmeanza kubatizwa kwa moto!
Nimemuona Pm na mama mhamaga wakiimba wana Imani na MMASAI, umewaona kwenye hio video Mkuu?
 
ng'ombe akikatika mkia zizini wenzake watajua kuwa hana mkia. usifikiri nimewaza vibaya naongea tu.
 
Hii video ni chungu na kumbukumbu mbaya kwa hawa jamaa.Kweli Lowassa alikuwa tishio ndani ya CCM.
 
Back
Top Bottom