Alinipenda akanionesha kila dalili, wamemuoa

Dr criminal

JF-Expert Member
May 16, 2022
2,278
4,273
Wagonjwa wapo hospitali, kwa huruma yake mungu atawaponya.

Day one naingia shule A mwaka B mkoa X vijijini uko, kama kawaida kuku mgeni hakosi kamba mguuni maaana nilichelewa wiki tano kureport kidato cha kwanza. Ukiniona unajua kabisa ile nyumbu ngeni maana shingo haitulii huku na huku kila kitu kigeni. Dah, acha tu ugeni unatisha.

Shule ilikuwa ni ya kata kwaiyo 99% ya wanadarasa kama siyo shule kwa ujumla tunajuana tangu kitaa. Yaani kama siyo tumesoma shule moja, basi shule za karibu, mabasi ya njano kaeni chonjo.

Sasa kwa kuzingatia muktadha wa stori yangu, mule darasani kama kawaida kila aina ya msichana alikuwepo, mzuri kuliko wote, mbaya (sio kwa ubaya lakini), mtu wa Mungu sana, mpenda michezo, kazinzi, wakishua, kichwani hamna kitu, hivo yani kama mjuavyo na wale saizi ya kati pia wapo.

Mlengwa wetu alikuwa mzuri lakini kwa visu vilimokuwemo mule ndani yeye ilikuwa ni ngumu sana kuonekana kwa haraka haraka, tumuite HK

Punde si punde form 3 hii hapa.
O-level sikuwa kabisa na habari za mahusiano ya mapenzi (tuelewane, siyo sikuwa na habari na wasichana, hapana, sikuwa na habari na mapenzi). Marafiki niliyokuwanao wote wakiume na wakike, lakini huyu HK hakuwa rafiki yangu, hata mtaani tunakaa sehemu mbalimbali.

Tukikutana hivi ni ile tu pw, pw imeisha hiyo. Sasa mmoja wa marafiki zangu wa kike, tumwite KC tulikuwa tunasoma wote namaanisha mimi, yeye KC na HK. Aliniambia siku moja "Criminal, HK anakupenda"

KC: Afu Criminal nikuambie kitu?
Mimi: Nakusikiliza...
KC: Nahisi HK anakupenda.
Mimi: Hauna stori nyingine?
KC: Anapenda sana kukuongelea, halafu yeye ni kukusifia tu, wakati sisi tumemzoea ni mtu wa kuchamba watu.
Mimi: Sawa nimekuelewa (ili kumaliza tu hyo mada).
KC: Ndiyo ujiongeze sasa.
Mimi: Sawa nitajiongeza.

Sikuchukulia kwa uzito kabisa hilo swala, hasa ukizangatia uhusiano wangu na mtu aliyeleta taarifa, ila mara kwa mara baadae KC alikuwa ananiambia yule HK anakupenda wewe. HK asili yake ni mwongeji sana, yaani ile sana, kiasi kwamba ukizingua tu kitu kidogo yeye akiwa karibu hata kama ni darasani na mwalimu yupo yeye ataropoka tu watu wakucheke mpaka basi.

Hili lilifanya wanaume wamwogope, likija suala la kumtongoza (nikiwemo mimi, ila kwa muda huo siyo yeye tu, karibu wasichana wote nilikuwa nawaogopa likija suala la kutongoza). Maana ukimtongoza halafu hajakuelewa utajuta!

Nilikuwa na uwezo wa wastani darasani, yaani ni mdogo kuzidi robo ya darasa, ila ni mkubwa zaidi ya robo tatu ya darasa. Kwaiyo kulikuwa na vigogo wengi juu yangu, ila HK kikimshinda kitu ni mimi, na kuna waliokuwa juu humo ndani na wanajulikana kabisa kwamba fulani na fulani ndiyo mwisho wa matatizo, lakini asipoelewa kitu ni mimi. Halafu tukipiga stori na tukiwa wawili tu ule uongeaji sana wote unapotea, kanakuwa humble halafu kanaaibu aibu, nikasema sawaa.

Nakumbuka likizo ya mwezi wa 12 ya kidato cha 3, nimepoa zangu tu nyumbani, ujumbe huo:

HK: Mambo.
Mimi: :poa, nani?
HK: HK.
Mimi: Ohh, mzima?
HK: Mimi mzima, hofu kwako?
Mimi: Mimi mzima, niambie..
HK: Nilitaka tu nikusalimie.
Mimi: :eek:Sawa, poa, ahsante.
HK:ppoa.
Mimi: Namba yako hii?
HK: Ndio.
Mimi: :ppoa.
HK: :ppoa.

Alikuwa anantafuta mara kwa mara ile likizo na mimi namtafuta mara moja moja. Akawa ananiambia ambia nikachukue vitu vitu kwao kama karanga mbichi, mara aniambie kuna memory card hapa kaka ameiacha kama unaitaka, mara usiku nisindikize nikachukue unga mashineni, yaani tuvitu vitu tu ile tuwe karibu. Rafiki yangu sana wa kiume tumwite P tulikuwa tunasoma wote, nilikuwa nampa stori hizo zote, akaniambia dogo amekuelewa huyo tongozaaa. Lakini sikumtongoza, kwanini?

  1. Tulikuwa tunaelekea kidato cha nne na mimi kichwani kwangu nilikuwa na hii "Mapenzi yatakufelisha".
  2. Sikumuelewa. Kuna huyo mtoto nilimuelewa mule darasani tofauti na yeye.
  3. Mzee wake alikuwa mkorofi na mkoloni, yaani alipiga huo mkwara pale kitaaa kuhusu mtoto wake sio poa.
  4. Nilikuwa muoga kutongoza.
Siku zikakimbia sana mpaka tukaingia chumba cha mtihani kidato cha nne, lakini huo muda wote hakukata tamaa. Zile ishara zote bado zilikuwa zinaonekana, yaani ni kama kuniambia "Ukiwa tayari niambie". Mtihanj tukapiga likaisha, baada ya mtihani mimi nilitoka pale kijijini nikaenda mkoa "Z" kwa kaka, nikamuacha mtoto uku nyuma bila hata kumuaga kwasababu hakukuwa na ulazima. Baada kama ya wiki mbili uko mkoa "Z" nikaanza kupokea sms za makasiriko kutoka kwa HK, kwamba sijamuaga, sithamini uwepo wake, nini na nini, malalamika kibao kanakwamba ni wapenzi. Sema sawa mawasiliano yakaendelea, matokeo yakatoka mimi nikapata ufaulu wa kuniwezesha kuendela kidato cha tano yeye akapata ufaulu wa kushindwa hata kumpeleka chuo.

Mwanaume nikaingia zangu kidato cha tano mkoa "U" yeye akiwa kule kijijini, nikirudi likizo sifa nyingi namwagiwa, mawazawadi mengi napewa, huku mwishoni mpaka mama akaanza kuzoeana naye. Mimi nikamaliza kidato cha sita baadae yeye pale kitaa alijifunza kushona kwaiyo akawa fundi. Katika hiki kipindi pia sikumtongoza, kwanini?

Likizo yote ya kidato cha nne sikukuwa pale kijijini.
  1. Bado domo lilikuwa zito. Ila nilipoenda kidato cha tano udomo zege ndiyo ulitoka huko huko nikapata na msichana, na mbususu ya kwanza ikachakatwa huko huko sema hii ni stori nyingine.
  2. After form six kama unavojua fasta tu majibu haya hapa mwamba chuo mkoa "V", lamba mkopo , nikapaa zangu huyoooo, ilaaaaaaaa bado HK hachoki hata kidogo.
Kwann nilivorudi likizo kidato cha sita sikumtongoza?
  1. Nilipata msichana kule kidato cha sita na niliridhika naye, kwahiyo sikuona haja ya kuwa na mwingine.
  2. Wasichana wa kidato cha tano/sita walinifanya nimuone HK wa kawaida sana.
Piga zangu mwaka wa kwanza chuo ukaisha salama tu, nikaingia mwaka wa pili.

Kwanini nilivyokuwa chuo sikumtongoza? .
  1. Nilikuwa na msichana chuo mkali zaidi ya HK.
  2. Wasichana wa chuo walinifanya nimwone HK wa kawaida.
Sasa hiyo siku nimepoa zangu tu geto mwaka wa pili chuo mwishoni mwishoni si nikapokea ujumbe kwenye simu yangu ya kiganjani.

HK: Criminal mambo.
Mimi: :ppoa, mzima?
HK: Mimi mzima, hofu kwako.
Mimi: Mimi mzima.
HK: Nimekumisi.
Me: Nimekumiss pia.
HK: Muongo wewe, hujanimisi hata!
Mimi: kweli, kwanza nilikuwa nakuwaza hapa.
HK: Sawa bwana, kesho ndoa yangu.
Mimi: ..........
HK: Nini hiko?
Mimi: Kweli?
HK: Ndiyo.
Mimi: Kwanini umechelewa kuniambia hivi?
HK: Ungefanya nini kama ningekuambia mapema?
Mimi: kweli bwana sikuwa na chakufanya lakini ingependeza tuu.
HK: Au ungesitisha ndoa?
Mimi: Ningewezaje wakati watu mshapendana?
HK: Ni wewe pekee unaweza kusitisha hii ndoa hata sasa hivi ukitaka.
Mimi: Mh, kivipi?
HK: Sijawahi na sidhani kama ntampenda mtu kama nilivyokupenda wewe!
Me: kwahiyo unataka kuniambia siku zote ulikuwa unanipenda?
HK:Vitu vyote nilivyofanya, maneno yote nliyokuwa nakuambia, kujipendekeza kote kule we ulikuwa huelewi unataka kusema?
Mimi: Si ungenambia tu unanipenda?
HK: Siyo rahisi kama unavofikria, leo yenyewe nakuambia kwasababu kesho naolewa.
Mimi: .....
HK:Nini?
Me: Mjinga sana mimi!
HK: We ulinipenda?
Me: ndiyo, sana.
HK: kwanini hukunambia?
Mimi: Nilikuwa naogopa utanikatalia.
HK: Kweli kama usemavyo wewe ni mjinga kwenye suala la kusoma mwanamke, unaniogopa mwanamke niliyekuonyesha kila dalili ya kukupenda?
Mimi: :DDaah nimejifunza HK.
HK: Sawa bwana uniletee tu zawadi yangu ya harusi ukirudi huko.
Mimi: Sawa usijali.
HK: Ntajaribu kupunguza mawasiliano na wewe kadri ntavyoweza ila nikikumisssi ntakutafuta.
Me: Sawa nakuombea tu mumeo akupende sana.
HK: Ahsante, tukipata mtoto wakiume ntapendekeza jina lako
Me: Kwanini?
HK: Kwasababu nilikupenda, nakupenda na ntakupenda daimaa.
Mimi: Unazidi kuichoma roho yangu ujueee.
HK: Kweli? Pole basi upumzike sasa.
Me: Sawa usiku mwema.
HK: Na kwako pia.

Hiyo ndiyo ilikuwa hatma yangu na msichana aliyenipenda sana.
Roho iliniuma, kwanini??
  1. Naaamini kama ningemuoa HK ndoa yangu isingekuwa ngumu sana kwasababu alishatokea kunipenda sanaaa.
  2. Baadae hata mama alikujaga kuniambia habari za ndoa yake kwa maaana hata mama alimuelewa, imagine .
  3. Nilivyoifadhiwa kwa muda mrefu kwenye kifua cha yule binti bila kuchoka, naamini haitokuja kutokea tena.
HK ndoa yake iko salama ana amani na furaha, mimi bado naendelea kusikiliza ngoma za Marioo #Dear Ex, #Inatosha, #Ahsante.

#OneDayYouWillBeGone,
Dr. Criminal.
 
Aisee nilianza vizuri, aya ya kwanza nkaanza kuona mapicha picha ya simoultaneous equation mara X, mara Y, mara sijui Kc. Wooi nmekata tamaa. Subiri ningoje summary ti
 
Back
Top Bottom