Alichonifanyia mdogo wangu naumia

Mankaa

Senior Member
Jan 21, 2012
156
49
Naamin hamjambo na mnaendelea vzr na kutusaidia ushaur sisi wenye matatz ya hapa na pale.

ni miezi minne imepita toka nimchukuwe mdogo wangu (mtoto wa baba mdogo) kijijini baada ya yeye kufeli form four na kuzalisha mtoto nikaona nimchukue nije nae mjini kwenye biashara yetu angalau apate pesa za maziwa ya mtoto

basi tumeishi vizuri siku zote na juz ndiyo akaniaga anataka arudi nyumbani akamuone mwanae,nikamwambia hakuna tatizo jiandae nkamwandalia pesa za safari vzr bas akaondoka jana.
baada ya kuondoka mume wangu akaniweka kwa mazungumzo nanukuu( mdogo wako kanieleza mambo ya kusikitisha umekuwa na mazoea mabaya na wanaume pale kwenye biashara wengne wanakuja kila siku,wengne wanaenda china wanakuletea zawadi unanidhalilidha,umekuwa malaya kwa kuzoeana na wanaume lukuki pale kazini na maneno meng sana)

Ukweli n kuwa hayo aliyoeleza mengne ni kweli nimezoeana na hao watu ni wateja wetu wazuri lakn hakuna cha zaidi hata huyu mdogo wangu anaelewa ukweli kwani muda wote nipo nae kazini.
nimemweleza mama yangu hajaamini kashangaa sana yani.
nafikiria najiuliza au huyu mdogo wangu alitumwa na mama yake kuja kuniharibia ndoa au ni kipi nilichomkosea au kosa langu kumsaidia had sasa amekuwa nae mtu anaonekana?au. ni kipi bado sielewi

mpaka sasa mume wangu ana kinyongo,
Huyo mdogo wangu cjamuuliza kitu chochote
nafikiria nimwambie neno gani ajue jinsi amenikosea au ninyamaze?

nishaurini wapendwa nifanye nini?
 
Syenzi huyo dogo na mumeo ni kama hajui nini maana ya kuwa mume pia!!!!!!
Ya alijua biashara ya duka watanunua ndugu zake???!!!!!


Ila nawe jicheki na kama vip fanya amendments,mkubwa hapangwi ati!!!!!!
 
Umeshapinduliwa hapo.Huyu mdogo wako alikuwa 'karibu' sana na mme wako ndiyo maan akampakia maneno mengi kirahisi hivyo

Mzee Tupatupa
Hapo nakataa kabisa hajakuwa karibu nae kiivyo nina uhakika asilimia 100
 
Kwanza, mtoe mama wa kinaja huyo kwenye ugomvi wenu.
Pili, kijana huyo asirudi kwako asilani

Mwisho, ukicheka na nyani utavuna mabua.
 
Kwanza, mtoe mama wa kinaja huyo kwenye ugomvi wenu.
Pili, kijana huyo asirudi kwako asilani

Mwisho, ukicheka na nyani utavuna mabua.
huyo msichana kurudi kwangu haipo nae anafahamu lakin nachofikiria ni jinsi ya yeye kujua how i feel kwa kitendo alichofanya
 
pole kwa ulio pitia!

Ila ukitaka kumsaidia ndugu usimkaribishe kwako!
Naongea out of experience!
Ungemuuliza anataka kufanya nn na umpe kamtaji kidogo aanzi hapo!
zaid ya yote ni Dume!!!

mwambie hutaki arudi kwako ila mumeo sasa atahisi ulio kuwa wafanya ni kweli!!!!
Msaidie huko huko aliko!
Ndugu kazi saaanaaa!
 
Kwa nini watu wengi wanafikiri ili wapendwe lazima wawaharibie wenzao? au watangaze umbea umbea lakini!!!! Aibu.......

Huyo mdogo wako amekosea na huenda lengo lake lilikua kumtahadharisha kakaye.... si unajua bado akili ya kijijini haijamtoka? au ndi ile kila akiona mtu kasimama na mwanaume anajua mnatoka wote.....

Or else anataka kukuharinia kitu kwenye ndoa yako.... Yoye kwa yote hekima yako ikuongoze.... na ikikushinda msaidie huko huko aliko na mwanawe.
 
Hapo nakataa kabisa hajakuwa karibu nae kiivyo nina uhakika asilimia 100
Sasa,kutaneni wote muendeshe shauri na mpate suluhisho.Huyo msichana naye lazima awepo ili aambiwe kuwa mawazo yake si sahihi na hakufanya vyema.

Lakini,asitokee mmoja wenu kuwanunua mashahidi. Asilani,msizungumze mambo yaliyoenezwa na mwingine peke yenu.Hamtaelewana.Hamtaaminiana.Mambo hayo yanazungumzika na kila kitu kitakwenda sawa. Nadhani umenipata mwanangu Mankaa? Mkinihitaji kuwa Msuluhishi,nitafuteni

Mzee Tupatupa
 
Daah dada Mankaa usikatae kuhusu uhusiano wao, embu kaa fikiria huo ukaribu umetokea wapi mpaka mdogo wako awe na guts za kumwambia hayo maneno mumeo? Na kama hamna kinachoendelea kati yao the watch out something is cooking
 
Last edited by a moderator:
Sasa,kutaneni wote muendeshe shauri na mpate suluhisho.Huyo msichana naye lazima awepo ili aambiwe kuwa mawazo yake si sahihi na hakufanya vyema.

Lakini,asitokee mmoja wenu kuwanunua mashahidi. Asilani,msizungumze mambo yaliyoenezwa na mwingine peke yenu.Hamtaelewana.Hamtaaminiana.Mambo hayo yanazungumzika na kila kitu kitakwenda sawa. Nadhani umenipata mwanangu Mankaa? Mkinihitaji kuwa Msuluhishi,nitafuteni

Mzee Tupatupa

siwez kuongea na huyo mdogo wang kabisa kabisa
 
kwa kwel dada yangu anakuomba kuitixha kikao cha wazaz wa pande mbili kama unataka kuinusuru ndoa yako maana ukmya sio dawa,sema usikike maana inaonekana kuwa mdogo wako hana nia nzur na anataka kukuharibia ndoa yako.wajibika uchukue hatua kwa kufanya maamuzi sahih
 
Ukitaka ndoa idumu ishi wewe na mumeo,watu wengine wakihusika lazima kutakuwa na chokochoko!
Nitaanza na kukupa lawama si tabia nzuri kuzoeana na wanaume wengine angali we ni mke wa mtu kwamaana hio wewe hapo umekosea,inawezekana aloyasema mdogo wako si yote yana ukweli ndani yake,lkn jishushe kwa mumeo na ukiri makosa yako na huyo mdogo wako mnafiki alitakiwa akupe taarifa hizo wewe na si azunguke nyuma ya mgongo wako kwa maana hio hapo kuna njama inachezwa!
Sikushauri uendelee kuishi na huyo mdogo wako maana keshaleta hitilafu,wanaadamu ni viumbe dhaifu sana hatuaminiki,na usifikirie kwasababu ni nduguyo atapenda maendeleo yako!Watu wengine hawafurahii kuona wengine wameendelea na wao wapo chini!THEY WILL WANT TO TAKE YOU DOWN WITH THEM OR TAKE OVER YOUR SPOT!!
 
Tatizo nini si kasema kweli. Acha kupokea vizawadi unajirahisisha. Jirekebishe tatizo si wewe?
 
Back
Top Bottom