Alichokisema Prof Muhongo: Kwenye Mjadala wa Bajeti ya Nishati na Madini

I don't get it. What kind of democracy is this? Maybe it is domocracy. The moment unaanza kuhoji mambo ambayo yanafanywa na chama chako unaanza kufikiriwa si mwanachama! So wanataka mabozo tu wanaosema yes kwa kila kitu? Na argument ad hominem aliyotumia mheshimiwa Muhongo dhidi ya Ole Sendeka ni just plain stupid. Mimi mwenyewe nilicheka nilipoona matokeo ya mheshimiwa mbunge. But for the minister had to bring himself to such a low level as bring it up in the bunge to win an argument ... now that is the definition of stupid, incompetent, ridiculous ineptitude.
 
nimeona hii hali najichelewesha,kuna fursa kibao za kupiga deal mawizarani,eti najifanya kamanda!kuba bake,wezi wanalindwa nchi hii
 
mambo niliyoyaona kuhusu prof na hotuba kwa ujumla,

1. mbunge ni kiongozi ambaye amechaguliwa na wananchi ili awaongoze bila kujali elimu ila wao ndio wameona anafaa.anapotaka vyeti vya wabunge na wewe unamshangilia tena hujibu hoja ya msingi, kwani kanuni zinasema mbunge bora awe anaelimu gani? wananchi hatuna muda na elimu zenu tunahitajia hoja zenye mashiko ndio maana maraisi kumi wa marekani hawakumaliza shule akiwemo JEMBE na genious linkoln kipenzi cha wamarekani.

2. wameuliza maswali wabunge wengi, Mbunge wa Nzega kaongea hoja zake hakuna aleyejibu, Maige kagusia kanuni za usalama kuvunjwa kwa ulipuzi underground BULY wakati mfanyakazi yuko chini ya shimo mwishoni akidai jibu anapewa utaratibu mrefu sana na spika.

3. Mzee sendeka kawawakilisha wananchi kuhusu ahadi ya wananchi aliyotoa rais na mambo yake hii mara ya pili, Sio yeye ni wananchi wake ndio wanaotaka kujua badala yake anakebehewa na kuonekana hafai hata kuwa ccm.

4. wananchi wanajiandaa kupokea hesabu ya ajabu kutoka kwa prof badala yake anatoa hesabu ambayo ni tusi. kwa hotuba yake na cheo chake sikuona sababu ya kufika huko.

5. Kwa jinsi nilivyoona wachangiaji na viongoji walitaka huruma iwe ndio msingi wa kupitishwa kwa hotuba. kwa sababu yeyote mwenye mawazo tofauti ni kama adui, amelipwa, katumwa anataka kukwamisha budget, ana huruma na nchi hii tulivu. Ukisema kinyume na prof unaonekana huna adabu na elimu yako ina mashaka.

6. waziri anasema malipo ESCOW ni halali na GAvana kasign haina shida tena wachangiaji hawana adabu kumsema huyo muasia wa iptl, Huyo huyo anasema yeye anaushahidi makaratasi tani moja na ni mzito kuliko mtu yoyote. ushaidi wa nini kama malipo ni halali? Pia CAG na takukuru waendelee na uchunguzi kama alivyosema waziri mkuu kama tatizo halipo kwa nini tena CAG na TAKUKURU. wananchi tunashindwa kutoka na wazo moja hususani sisi tusioelewa sakata hili.

7. Kama zaidi ya asilimia sabini na tano wanapongeza na kusifu hotuba hawa wachache wakitoa challenge inaonekana kama wanakosea saana hii nchi. watawala wanasahau kuwa leo hakuna hata mmoja aliye shukuru chochote kwenye maelezo ya wapinzani na watu wenye mitazamo tofauti na hotuba ya prof.

8. nilichokiona leo, Wabunge Mwigulu ("kwa sababu wameondoka ngoja niongee kama waziri"), Kigwangalala (umekili mwenyewe), kafulila, hisia zimezidi,kama inawezekana inabidi changamoto hii muishinde. Waziri Muhongo Umesoma tunajua , ila ukiongeza busara kwenye hoja zako wananchi watakupenda zaidi tena unaweza kuwa zaidi ya mwalimu nyerere kwa karne hii. tunawataka vijana zaidi humo ndani ili nchi hii iende mbele kwa uhakika.

Changamoto kwa wapinzani:
1. Sielewi kwa nini miaka yote hotuba zinakuwa sio mbadala ila ni shutuma na mapendekezo machache. Muwaelimishe wananchi kwa nini mnafanya hivyo ili mueleweke.

2. Binafsi sijafurahi mlivyotoka maana mlipoondoka na hata kama mngebaki bado ni wachahe mambo yangeenda tu. Mbinu hiyo mmetumia mara kadhaa inatosha mtafute mbinu mpya. mmetukosesha mawazo yenu mbadala na mdahalo wote ukapoteza ladha. kiukweli kuwepo kwenu tunajifunza mengi.

3. Mpinzani wa kweli inabidi usiwe na shutuma yoyote ili upinge vizuri. kama kweli mmeonekana kwenye CCTV Cameras mnasign wananchi mnatuchanganya na hatutawaelewa.

ushauri:

Kuingia bungeni ni fulsa ya kihistoria, Kila mbunge Mpinzani au CCM simamia miguu yako bila kuteteleka kutetea haki, rasilimali za nchi, jimbo, kemea uovu, Sifia vyema,

ni maoni yangu tu baada ya kuwatazama viongozi wetu, maana kupata fulsa ya kuangalia bunge wengi huwa mara mojamoja.
 
Hawa wanatuwakilisha au ni matumbo yao. Prof unaleta dharau za mimi kila siku ahadi umeme shida. Fanya kazi inayoenda na CV yako
 
A[SUP]4[/SUP]*4=A

Divide by A both sides

you will get

A[SUP]3[/SUP]*4=1 Hence proved, so

A=(1/4)[SUP]1/3[/SUP]
Tunaomba uprove aljebra ifutayo kulingana na Maelezo ya Pro.
A[SUP]4[/SUP] X 4=A
kama hujui maana ya kuprove kwa kufuata kanuni za kihesabu omba msaada
 
ha ha ha ha ha, hawa ndio maproesa wa Tanzania mbao wamenyweshwa maji ya bendera ya kijani. Ha ha ha ha ha ha, yaleyale ya Tibaijuka na Halima Mdee. Maprofesa wamekuwa assaulted na dot com wakahamaki wakajaribu ku-dance to the tune ya vijana wameishia kusaula mbele ya ya kadamnasi
 
Tunaomba uprove aljebra ifutayo kulingana na Maelezo ya Pro.
A[SUP]4[/SUP] X 4=A
kama hujui maana ya kuprove kwa kufuata kanuni za kihesabu omba msaada
Mara ya kwanza uliulizia kama huo mlinganyo kama unawezekana nikakwambia unawezekana ambapo nilikwambia ya kwamba A[SUP]4[/SUP]*4=A ni sawa na kusema A[SUP]3[/SUP]*4=1

Ukaniambia ni prove ninachosema kwamba A[SUP]4[/SUP]*4=A ni sawa na A[SUP]3[/SUP]*4=1 ndio maana nikaprove hapo juu ninachosema ndio maana nikakuandikia hence proved, nikakutafutia na thamani ya A, mara ya kwanza ulikuja kwa kuulizia kama huo mlinganyo wako unawezekana hapo ulikuwa unamaanisha kama unaweza kutafuta thamani ya A nikakwambia unawezekana

naona sasa unajifanya mjuaji wakati ulikuja kuomba msaada kama huo mlinganyo wako unawezekana nikakwambia unawezekana eti sasa hivi unataka unifundishe kabisa unaniambia na niombe msaada kabisa sasa sikiliza wewe Mwanafunzimg hesabu mi niko safi kwa milinganyo kama hii sidhani kama inaweza ikanitoa, we usidhani mi ni kilaza...

eti unaniambia sijui maana ya ku prove sikiliza hapa huwa tunasaidiana na hatupo kushindana nani mjuaji zaidi, kwa huu mlinganyo wako A[SUP]4[/SUP]*4=A hauwezi ku prove kwasababu L.H.S sio sawa na R.H.S, kwa hiyo siwezi ku prove hizo pande nikichukua upande wa kushoto hauwezi kunipeleka Kupata A ili uweze kulingana na upande wa kulia...
 
Hata Banda kule malawi alikuwa akiwakejeli na kuwakejeli wapinzani lkn leo haamini...bila kusahau kule india baada ya muda wapinzani wataeleweka tu.
 
Ni Mpuuuzi sana Tuna Ma Prof waajabu sana

Muhongo mjivuni mno

jamaa naongea kwa dharau sana , daaah, hawa ndio wasomi wetu

Siyo kwamba Muhongo anafanya haya kwa sababu ni profesa, tuna viongozi wa CCM wa ajabu! Katika historia ya chama hiki kila wakati huwa kuna mtu anajitokeza na kufanya upuuzi kabisa halafu anasifiwa!

Nakumbuka Malechela alipowaambia wapiga kura wake "Go to hell" wakati wakifa kwa njaa, Msuya akawaambia wa-TZ wote "kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe" wakati huo yeye kisha chota rushwa zake kibao kwa mikataba ya wizara ya fedha, sasa Muhongo kisha tuambia " wa-TZ ni wavivu wa kufikiri" Bahati mbaya kabisa viongozi wa aina hii ambao mimi nawaita ni wapuuzi, ktk chama wanapewa 'like.'
 
Ndio maana tpdc na wizara yake anawataka watu wenye 1st na upper second tu! Sasa nimejua
 
Mara ya kwanza uliulizia kama huo mlinganyo kama unawezekana nikakwambia unawezekana ambapo nilikwambia ya kwamba A[SUP]4[/SUP]*4=A ni sawa na kusema A[SUP]3[/SUP]*4=1 Ukaniambia ni prove ninachosema kwamba A[SUP]4[/SUP]*4=A ni sawa na A[SUP]3[/SUP]*4=1 ndio maana nikaprove hapo juu ninachosema ndio maana nikakuandikia hence proved, nikakutafutia na thamani ya A, mara ya kwanza ulikuja kwa kuulizia kama huo mlinganyo wako unawezekana hapo ulikuwa unamaanisha kama unaweza kutafuta thamani ya A nikakwambia unawezekana naona sasa unajifanya mjuaji wakati ulikuja kuomba msaada kama huo mlinganyo wako unawezekana nikakwambia unawezekana eti sasa hivi unataka unifundishe kabisa unaniambia na niombe msaada kabisa sasa sikiliza wewe Mwanafunzimg hesabu mi niko safi kwa milinganyo kama hii sidhani kama inaweza ikanitoa, we usidhani mi ni kilaza... eti unaniambia sijui maana ya ku prove sikiliza hapa huwa tunasaidiana na hatupo kushindana nani mjuaji zaidi, kwa huu mlinganyo wako A[SUP]4[/SUP]*4=A hauwezi ku prove kwasababu L.H.S sio sawa na R.H.S, kwa hiyo siwezi ku prove hizo pande nikichukua upande wa kushoto hauwezi kunipeleka Kupata A ili uweze kulingana na upande wa kulia...
Mkuu mlinganyo huu umetoka kwa waziri wetu tena akjitapa kwa kuwaambia watu waandike hesabu yake kwamba :mnyika kipeuo cha nne mara nne ni sawa na mnyika hili waziri kalisema bungeni sasa nikaomba wanamahesabu watusaidie kma mlinganyo huu ni sahihi nashukuru maelezo yako ya sasa yanaungana nami kwamba hiki kitu hakiwezekani kwani R.H.S si sawa na L.H.S
 
Back
Top Bottom