Mamlaka husika ilichelewa sana kuwadhibiti hawa jamaa wamasababisha madhara makubwa sana katika tasnia ya matibabu, kikubwa walichofanya ni ile kuwa wao ni waganga wa tiba mbadala lakini wakajikita zaidi katika tiba ya kihospitali na kuanza kujitangaza kwa television.
Waganga wa kihospitali (medical personnel) huwa hawajitangazi kihivyo bali wanajamii wenyewe huwapa umaarufu kwa huduma zao wanazozipata kutoka kwao pindi wanapofika sehemu zao za kazi.
Walichokuwa wanafanya akina Dr. Mwaka ni upotoshaji mkubwa ambao umesababisha madhara yafuatayo
Wametangaza sana ati kuna ugonjwa wa UTI na mtu anaweza kupata hiyo UTI kwa kuchangia choo yaani unaweza kupata UTI chooni, hii siyo kweli ni uwongo, uwongo, uwongo. Chooni unaweza kupata uambukizo aidha kupitia miguuni kama hujavaa viatu au mikononi vidudu ukavila kama hujanawa mikono ukitoka huko.
Sasa matokeo yake akina mama wakiwashwa kidogo sehemu zao za siri huja na kusema nimepata UTI tunachangia choo. Tabu iko kwenye matibabu antibiotic za kawaida kama Tetracycline, Ampicilline au Amoxycline hawazitaki tena eti hazitibu hiyo UTI. Wanataka dawa kama Cepharexine au Ceftriaxone au Azithromax ambazo ni very broad spectrum antibiotic for nothing.
Uambukizo katika njia ya mkojo (urinary tract) upo na husabibishwa na vimelea ambavyo ni very weak antibiotic zile nilizozitaja hapo juu ni zinafaa sana.
Madhara ni kwamba hizo antibiotic wanazozitaka na wanazoamini ndizo zinatibu hiyo UTI ya akina Dr. Mwaka ambazo zinatumika sana sasa hivi zikiisha zoeleka na vimelea na vikawa sugu basi jamii itapata tabu sana kupona hata uambukizo wowote unaosababishwa na bacteria hasa hasa magonjwa ya zinaa.