Akaunti za mafisadi BoT zagundulika

Nina amini mafisadi wote wanatambulika na serikali yetu, itakuwa jambo la maana kama watachukuliwa hatua za kisheria ili haki itendeke kwa mtanzania. itakuwaje watu wachache wafaidike na familia zao wakati kuna kina mama na watoto wanakosa huduma za afya kwa serikali kukosa fedha kumbe ziko mikononi mwa watu wachache? Tumefikia hatua ya kusaidiwa hadi "neti za mbu"!

Kujivua magamba kwa chama tawala pekee haitoshi, hilo pia lifanyike kwenye serikali yake, ndio wananchi watarudisha imani na uongozi
 
Hii inaonyesha wazi kuwa Tanzania sio nchi maskini bali kuna watu wachache ambao wanafaidika na utajiri mkubwa ambo nchii hii unao. Mbali na wageni ambao kila leo wanavuna utajiri wa nchi hii lakini pia kuna Watanzania wenzetu ambao hawana chembe ya huruma kwa watanzania wenzeo ambao hata mlo wa siku moja haujui??? kwa kweli inasikitisha na kuhuzunisha kuona watu wa sample hii.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa

Mungu wanakamishe Mafisadi wote - ameen

Nakubaliana nawe. Tanzania ni tajiri sana,bali wachache wametufanya tuamini kuwa tu watu masikini wenye kustahili omba omba. Fikiria mradi mmoja tu, IPTL, tunalipa Tshs milion 152 kila siku kwa umeme ambao hautoshelezi watanzania. Watanzania tuko milioni 43. malipo ya 152milion ni sawa na kulipa kila mtanzania takribani milioni milioni 3 kila siku; mshahara kiasi gani huo?? utajiri kiasi gani wa tanzania huo??hata marekani hawapati kitu. Lakini mchawi wa mtanzania (kuzama katika umasikini) ni MTANZANIA mwenyewe!!!!!!!!!! Natamani kulia.
 
Duh! Ndio maana hawataki kabisa kuitoa hiyo ripoti ya ukaguzi wa EPA maana sirikali yote itaonekana IMEOZA kwa ufisadi! Hawa wabunge nao bado ni mabaradhuli! watakubali vipi bunge liahirishwe hadi mwishoni mwa April wakati kuna tuhuma nzito za ufisadi ndani ya BoT!
Kwa kuwa wamejivua Magamba wataitoa tu na wasipo itao iko siku wataitoa kwa nguvu ya umma...
 
Mkapa ana hotel south africa aeleze alijengaje?na epa ilichotwa wakati wake!
 
This is another bullshit from "wachunguzi wetu"

Inaeleweka kabisa kwamba the game is on kwsbabu gamba ilanataka kuondoka na sumu!!! I hate this uchunguzi, taarifa za kiintelijensia, uchunguzi wetu blah blah blah
 
Watanzania lazima muwe macho na giliba za CCM ambazo zitafuatia kujivua gamba!baada ya kuwa wameona kwamba si chama tu kilichopoteza mvuto kwa watz kwa sababu ya kuwakumbatia mafisadi bali ni udhaifu mwenyekiti katika kushughulia maswala magumu na ya msingi. Sasa wanakuja na mikakati ya kujaribu kujenga taswira yake mbele ya watanzania ili nchi iweze kutawalika (tatizo lao wanapenda sana kutawala na sio kuongoza). Hapa hakuna uchunguzi wala nini ni sanaa kwaajiri ya kuwaadaa watz. Na katika mkakati huu ipo mitandao mingi-redio, magazeti, tv, blogs etc. Baada ya uchaguzi Rais wa marekani aliwatumia salam watanzania kwa kuendesha kuchaguzi kwa amani nothing was said kuhusu kumpongeza aliyeshinda. This explain a lot why he is not a frequent flyer now days. He duped the election!
 
Hiyo ripoti nani kaiona? Wanaotajwa katika hiyo ripoti ni akina nani? Akaunti za akina nani zimezuiliwa ( ama bado wana uhuru wa kuhamisha fedha na kuzificha? ), Mahakamani wana fikishwa lini? Kama ni watendaji serikalini waliofukuzwa ama kusimamishwa ni akina nani? Hivi ndio vigezo vinavyodefine kufanya kweli!
 
Acheni habari za magazetini, kama kweli ilikuwa siri mbona imeshatoka?...
Nani mwenye account hizo ambaye kwa taarifa kama hii atakuwa bado amelala akizubiri report ya EPA ifikishwe bungeni..Hakuna siri Tanzania isipokuwa kuna kubebana..
Majina sii hoja, hoja na ushahidi ni kiasi gani cha fedha zipo huko na zimeokolewa... JK na serikali yako kama utafanya kweli fanya, hizi habari za kusubiri ziara ya Bush mara sijui nini hali kinachopotea ni zaidi ya msaada huo hatuwezi vumilia.
Chakula kinapoa mkubwa maswala ya kusubiri mgeni aondoke watu ndio kwanza wanashiba jikoni..na tonge likisha ingia tumboni kitakacho bakia ni lawama tupu...kinyesi hakiliki wala kuhesabika..
Mkandala waguma
 
Back
Top Bottom