ajira ya foreigners nchini

jobseeker

Member
Feb 25, 2012
70
7
Naomba kuuliza hivi hawa wageni hupata pata vipi ruhusa za kufanya kazi nchini?
Tanzania kwa sasa imejaa watasha na wachina. Ajabu wote hawaongei lugha ya nchi
na wachina wengine hata kiingilishi kinawapiga chenga. nataka kujua ni nani mwenye
majukumu ya kutowa ruhusa na kuishi na kufanya kazi kwa wageni hawa? Kuna kazi
tele ambazo wazawa wanaweza kuzifanya lakini zimekwenda kwa watasha, why?
 
The whole system is corrupt,kibaya zaidi ni kwamba hakuna centralisation kwenye kutoa permit kwani migration,Wizara ya kazi na TIC wote kwa wakati wao wanatoa au kubariki hii kitu.Migodini ndio hali mbaya zaidi,cha kusikitisha zaidi ni kwamba baadhi ya WaTZnia wenzetu ambao wako kwenye nafasi ndio wanafanya hivyo.Ninao ushahidi wa Ma-HR officers migodini wanahusika kufanya hizo lobbying.


Trust me,hii nchi ilishauzwa.
 
These are common reasoning.......ambazo tunazugwa nazo

-Specialised skill not available within
-Investors
 
Hii ni hatari kubwa kwa vijana wa leo:-

Migodini wamejaa makaburu, wazungu.

Kwenye biashara (eg KKoo, gereji, viwanda vidogo etc) wamejaa wachina.

Kwenye makampuni ya ujenzi wa majengo na barabara wamejaa wachina.

Kwenye makampuni ya simu (eg Voda, Airtel etc) wamejaa Wahindi na wanaongezeka kwa kasi.

Kwenye stationery kubwa na maduka ya computer used eg kariakoo na city center wamejaa Wasomali.

Kwenye ardhi nono ifaayo kwa kilimo vijijini wamechukua Wawekezaji.

N.k, n.k, n.k


Enyi watu wa uhamiaji, uwekezaji, watoa vibari vya kazi amkeni kutoka katika usingizi huo mzito mliolala.
Hii mianya mnayoiachia inaumiza watanzania na jamii ambayo hata ninyi mmo ndani yake.

HRs na maafisa mbalimbali wa serikali simamieni haki, taratibu na sheria ili kunusuru jamii yetu hasa vijana wengi wanaosoma na kumaliza vyuoni.
 
These are common reasoning.......ambazo tunazugwa nazo

-Specialised skill not available within
-Investors

Nimeangalia profile ya mtasha mmoja anaefanya kazi kwenye kampuni fulani ambayo nilikuwa naitafiti kwani nataka kuomba kazi huko, anyway kwenye linkedIn profile yake si lolote na to be honest naamini wapo wabongo tele wenye elimu zaidi na uzoefu mkubwa na wanaweza kufanya kazi anayoifanya yeye. Sikuona specilised skills zozote kwa kazi anayofanya au experience alonayo.

Investors? oh please! im not buying that at all. Viongozi mnatuumiza!!!!
 
Hili swala ni gumu sana ma-HR wanashirikiana na ma-officer wa uhamiaji kula mirungula ya foreigners hili waendelee kufanya kazi bila vibali vya kazi.
 
These are common reasoning.......ambazo tunazugwa nazo

-Specialised skill not available within
-Investors

Sikubaliani na wewe hata kidogo!
Kuna Watanzania kibao waliosoma elimu ya kueleweka, hata wengine wana MSc zao, lakini wanazunguka street kutafuta kazi, bila mafanikio.

Wachina hao hao wanye elimu kama yangu hii duni(STD VII), wamepewa vibali vya kufanya kazi nchini kama Supervisors.
 
Back
Top Bottom