Ajira Milioni 1.3 Alizotengeneza JK Hizi Hapa!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Wapendwa wanaJF mpya, mnakumbuka kuwa mh Rais wetu JK aliahidi ajira zaidi ya Milioni moja wakati anagombea urais mwaka 2005. Mnakumbuka pia kwamba kuna wakati Waziri Juma Kapuya aliwahi kutamka kwamba JK alishatekeleza ahadi yake. Juzi juzi tena Waziri Kapuya alirudia kauli hiyo kama ifuatavyo:

SEHEMU YA MABILIONI YA JK YAPOTEA!
"SHILINGI bilioni 13 ambazo ni sehemu ya mabilioni yaliyotolewa na Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuongeza ajira maarufu kama Mabilioni ya JK, zimepotea.

Ripoti ya Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kwa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, inaonesha kuwa kati ya fedha hizo Sh bilioni 6.7 zimewekwa katika kundi la mikopo ‘chefuchefu’ ambayo haiwezi kulipika.


Nyingine Sh bilioni 6.8 zimeshindikana kurejeshwa na wananchi waliokopa kutokana na wakopaji kushindwa kuzizalisha katika miradi ambayo iliwafanya wakope. Katika fedha hizo ambazo bado ziko mikononi mwa wananchi, Wizara jana ilikiri kuwa limekuwapo tatizo la wananchi wengi kutorejesha mikopo hiyo, kwa sababu mbalimbali zikiwamo za miradi iliyoanzishwa kutofanikiwa na zingine za kisiasa.


Kati ya Sh bilioni 6.8 ambazo wananchi wameshindwa kurejesha, Sh bilioni 3.4 ni kutoka Benki ya NMB na Sh bilioni 3.4 CRDB. Kwa upande wa mikopo chefuchefu ambayo inafikia Sh bilioni 6.7, Sh bilioni 3.3 ni kutoka NMB wakati Sh bilioni 3.3 CRDB.


“Hali hii inasababisha benki hizi kuidai Serikali fidia kulingana na mkataba uliosainiwa baina ya benki yao na Serikali,” alisema Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya.


Benki hizo mbili kwa mujibu wa Profesa Kapuya, zimemaliza mkataba wa makubaliano na Serikali katika kutekeleza mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi ulioanza mwaka wa fedha 2006/07 hadi 2008/09.


“Kutokana na kumalizika mkataba huu, Serikali inaandaa utaratibu wa kuhakiki madeni kulingana na makubaliano yaliyo kwenye mkataba,” alisema Waziri.


Akielezea changamoto zilizoukumba mpango huo alisema ni kuwapo kwa dhana potofu inayoenezwa na baadhi ya watu wakiwamo viongozi wa kisiasa kuwa fedha hizo ni zawadi iliyotolewa na Rais Kikwete kama shukrani kwa wananchi kwa kumchagua.


“Hivyo hawataki kuzirejesha fedha hizo,” alisema Profesa Kapuya na kuongeza kuwa fedha ambazo zimerejeshwa hadi Februari mwaka huu ni Sh bilioni 30.8. Serikali ilipanga katika awamu ya kwanza na ya pili ya utoaji wa mabilioni hayo ya JK kutoa Sh bilioni 45.2.


Changamoto nyingine iliyotajwa na Waziri ni baadhi ya maofisa wa NMB na CRDB kutozingatia maadili ya utoaji mikopo na kukosekana kwa dhamana kwa wakopaji, hali inayozifanya benki kushindwa kukamata mali za wadaiwa.


Hata wajasiriamali ambao walifaidika na mikopo hiyo hawana elimu ya kutosha, hivyo kushindwa kuzitumia kwa malengo husika.


Tatizo lingine ni vikundi vingi kukosa malengo madhubuti wakati wa kuchukua mikopo, hali ambayo iliwafanya kukwama katika urejeshaji.


Pamoja na matatizo hayo yaliyojitokeza, lakini Profesa Kapuya aliiambia Kamati kuwa mpango huo umeonesha mafanikio makubwa kwani umesaidia ajira milioni 1.3 kupatikana, na hivyo kuzidi lengo lililowekwa na CCM la ajira milioni moja.


"Mpango huu umeonesha mafanikio mazuri kama kuongezeka kwa pato na hivyo kukidhi mahitaji muhimu ya wananchi kama kusomesha watoto, kujenga na kupata lishe bora,” alisema Profesa Kapuya.


Wabunge kwa upande wao walionesha wasiwasi kuwa licha ya mpango huo kuwa na jina kubwa la Mabilioni ya JK, lakini wananchi wengi hawakuziona fedha hizo.


“Wanasikia tu kuna Mabilioni ya JK, lakini wananchi wengi bado ni masikini, hivi hayo mabilioni yako wapi? Hilo ni swali wanajiuliza wananchi walio wengi,” alisema Mbunge wa Viti Maalumu Florence Kyendesya (CCM).


Aliomba Wizara hiyo kufuatilia SACCOS ambako alidai yawezekana kuna wajanja walijikopesha na kufanyia shughuli zao na baadaye kuzikopesha nje ya utarataibu.


Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jenista Mhagama, alitaka mpango huo ugeukie kwa wazalishaji ambao wengi wao wako vijijini, badala ya wajasiriamali peke yao ambao wako mijini.


Waziri Kapuya alikiri kuwa maeneo ya mijini ndiko walikochangamkia haraka mabilioni hayo na akasema wizara yake imeandaa mkakati kuhakikisha wanazitumia kufikisha fedha hizo kwa wananchi vijijini hasa wazalishaji.


Lakini alionesha wasiwasi kuwa kukosekana kwa maofisa vijana katika wilaya nyingi, kumechangia wananchi wa chini kushindwa kufaidika na fedha hizo, kutokana na kutokuwapo watu wa kuwapa elimu ya namna ya kuandaa mradi."

Source: HabariLeo.

 

“Wanasikia tu kuna Mabilioni ya JK, lakini wananchi wengi bado ni masikini, hivi hayo mabilioni yako wapi? Hilo ni swali wanajiuliza wananchi walio wengi,” alisema Mbunge wa Viti Maalumu Florence Kyendesya (CCM).
"Mabilioni" itabaki kuwa nadharia tu. Kweli Siasa ni mchezo mchafu.
 
Utashangaa mwezi Oktoba JK atavuna kura za kishindo! Marekani imeitaka Tanzania kujichunguza kwa nini ni maskini wakati kuna raslimali nyingi sana kupita nchi nyingi duniani! Nakumbuka JK aliwahi kusema kwamba hajui ni kwa nini Tanzania ni maskini. Sijui kama sasa hivi ameshapata jibu sahihi!
 
Hakuna jipya hapa, wala ajira yoyote.
Nchi gani tunategemea misaada kwaa miaka hamsini ya uhuru?...Sasa hivi wanaanzisha mpango wa CHANGIA CCM KWA SMS!...Ni ujinga mtupu!
 
Utashangaa mwezi Oktoba JK atavuna kura za kishindo! Marekani imeitaka Tanzania kujichunguza kwa nini ni maskini wakati kuna raslimali nyingi sana kupita nchi nyingi duniani! Nakumbuka JK aliwahi kusema kwamba hajui ni kwa nini Tanzania ni maskini. Sijui kama sasa hivi ameshapata jibu sahihi!

Wana mpango wa kuahirisha uchaguzi wakishirikiana na "mganga" wao
 
mabilion ya JK nadhani ni kati ya mikakati yaki hovyo hovyo sana katika kuwawezesha Watanzania, kwani wanaofaidi wanakuwa wale wale wa siku zote. Kama kilimo kwanza kingeanza na research ya wataalam kutoka let say SUA na Mzumbe, na kushirikisha wataalumu mbalimbali wa kiuchumi then nguvu ikapalekwa huko tungepunguza umaskini kwa kiwango kikubwa sana. Umaskini wetu ni wa KUJITAKIA ukisababishwa na wanasiasa wetu, wananchi kwa kuwapa kura zao hao madu madu, nzige na parare wakati wa uchaguzi. USA wakuwa wawazi sana na ningekuwa na power kama Usa na EU then ningekata misaada yote Tanzania ili tujifunze kujitegemea na tuache beging mentality ambayo tunayo sana.
 
Utashangaa mwezi Oktoba JK atavuna kura za kishindo! Marekani imeitaka Tanzania kujichunguza kwa nini ni maskini wakati kuna raslimali nyingi sana kupita nchi nyingi duniani! Nakumbuka JK aliwahi kusema kwamba hajui ni kwa nini Tanzania ni maskini. Sijui kama sasa hivi ameshapata jibu sahihi!

Kishindo chja %age tu ndugu yangu.....tatizo kila election ijayo turnout inakuwa less compared na iliyotangulia...ikiwa watanzania 3m wanavote na 2.4m wanamcahgua JK basi si haba atashangilia kuwa ni 2.4/3(80%) ya watanzania wamemchagua lakini in reality ni 2.4/40(6%)tu
 
Back
Top Bottom