Ajinyonga kisa kukatazwa kuoa mke wa pili

MJIMPYA

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
506
272
MKAZI wa kijiji cha Ubinga kata ya Mhugi, Tabora, Bundala Mwandu (26) amejinyonga baada ya walezi wake kumkataza kuoa mke wa pili.

Akithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Nzega, Issa Muguha, alisema Mwandu alikutwa amejinyonga Juni 13 saa nne asubuhi katika kijiji hicho.

Muguha alisema, kabla ya kujinyonga, Mwandu alikuwa na mke mmoja na alitaka kuoa wa pili, lakini alipopeleka taarifa hiyo kwa walezi wake, hawakukubaliana na uamuzi huo.

Baada ya taarifa hiyo kukataliwa, Mwandu alifikia uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ya gome la mti.

Akizungumza na gazeti hili, babu wa Mwandu, Bulabo Kinimba, alisema alipopata taarifa ya mjukuu wake kutaka kuoa mke wa pili, alimshauri asubiri mpaka baadaye.

Kinimba alisema alimshauri kwamba kwa sasa umri wake hauruhusu kubeba majukumu makubwa ya familia mbili.

“Nilimwambia asubiri baadaye ndipo angeze mke wa pili, kwani bado ana umri mdogo, nashangaa kijana wangu amefikia uamuzi huu,” alisema babu huyo.
Source: Habari Leo
 
wajinga hao walezi..
mtu anajua mwenyewe ana uwezo wa kumiliki nyumba mbili.wao
kujifanya wanajua ni nini?
 
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa sijui ni lini mwanadamu ataijua thamani yake kuwa iko ndani mwake,haipo kwa mke,mume,mpenzi,baba,mama wala hela au kitu chochote kilicho nje yake!
 
Chunguza hata uelewa wa huyo dogo ni lazima utakuwa mdogo tu. Niaminivyo hakuna sababu iwayo yote inayoweza kupelekea mtu kujinyonga kwani maisha baada ya kifo chako yatakuwa mabaya kuliko uliyakimbia katika uso wa dunia kwa kuogopa fedheha toka kwa wanadamu ambao hawana pepo au moto.
Hasira, kisirani, chuki, upweke uliopitiliza, tabia ya kupenda kulipiza visasi, kukata tamaa hususani kimaisha, kukosa uelewa wa kutosha juu ya Mungu n.k ni baadhi ya tabia zinazokaribisha kujinyonga.
Kabili changamoto katika maisha yako kwa njia muafaka huku ukijenga tabia ya uvumilivu, usikivu unaposhauriwa, kusamehe ukiombwa msamaha wa dhati, jitahidi kuwa na elimu ya kutosha juu ya Mungu n.k
 
Huyo jamaa hata maamuzi ya kifamilia sidhani kama alikuwa nayo, wa ajabu kweli. Aliambiwa asioe forever? watu wengine hawaelewi kabisa maana ya maisha, apumzike alikotaka!!
 
Maamuzi aliyoyafanya yanaonyesha Alikata tamaa ya naisha na alikuwa anatafuta sababu ya kujiondoa duniani!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom