Ajifanyia upasuaji kwa kutumia kisu hii kali jamani .............

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
MWANAMUME raia wa Marekani aliyekuwa na matatizo ya ugonjwa wa ngiri aliamua kujifanyia upasuaji kwa kujichana kwenye tumbo ili kutatua tatizo na kisha aliwasha sigara na kuchoma sehemu ya kidonda.Polisi walimkuta mtu huyo akiwa amevua nguo kwenye nyumba yake Los Angeles nje ya mji wa

Glendale katika jimbo la California, Jumapili baada ya mke wake kuwapigia simu kuwafahamisha kuhusu jaribio la mume wake kujifanyia upasuaji
, msemaji wa Polisi Glendale, Sajenti Tom Lorenz alisema.

"Alijichana mwenyewe kwa kutumia kisu cha mkate," Lorenz alisema. "Alimwambia mke wake kuwa alikuwa akichanganywa na maumivu ya ngiri, na hakutaka kusubiri zaidi kwa ajili ya kutibiwa kwa dawa."

Maafisa wa polisi walimwona mtu huyo, baada ya kutoa kisu kwenye tumbo lake, kuweka sigara katika kidonda, alisema Lorenz.

"Sijui kama alikuwa akitaka kujiunguza au kitu chochote," alisema.

Polisi hawakumtaja mtu huyo, lakini Lorenz alisema hakufanya kosa na kwamba inawezekana alishawishiwa na dawa za kulevya au kulewa.

Alipelekwa katika hospitali ya Los Angeles ijulikanayo kama USC Medical Center ambapo aliwekwa kwa saa 72 kuchunguzwa akili.

Spoti Starehe | www.spoti.co.tz
 
Back
Top Bottom