Ajali za vyombo vya majini, Bado hatujajifunza kuwa na vifaa vya kisasa na waokoaji

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
5,031
12,792
Tanzania Miaka ya nyuma tulipatwa na majanga ya ajali kubwa za meli zilizopelekea kuzama na kupoteza uhai wa wananchi wengi. Meli ya Mv Victoria Mwaka 1996 ilipozama changamoto ilikuwa vifaa vya uokoaji na wazamiaji(Divers) na tukapata msaada wa wakoaji kutoka South Africa.

Mv Spice Islander na Mv Skagit zilipozama changamoto kwenye uokoaji bado zilijitokeza inapofika Muda wa usiku hatuna vifaa wezeshi Kwa ajili ya wazamiaji. Kivuko Cha Mv Nyerere kilipozama shughuli za uokoaji zilikuwa zinaishia pale giza linapofika.

Tumefanikiwa kuwa na mfumo na kituo Cha uokozi Search and Rescue (SAR) ila manpower na vifaa vya uokozi hakuna.

Licha ya kuwa na eneo kubwa la bahari na maziwa tumekosa Rescue Boat, Night Diving accessories na professional divers, amphibious helicopter, seaplanes.
 
Back
Top Bottom