barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Hali ya taharuki ilizuka ktk eneo la Ubungo darajani mkabala na ilipo mitambo ya Gas ya Songas baada ya waya wa umeme kudondoka ghafla na kusababisha moto mkubwa kuzuka na kuunguza bidhaa mbalimbali yakiwepo "masofa chakavu",vitanda na milango chakavu ambayo ulindikwa pembezoni mwa daraja la Ubungo.
Ikumbukwe kuwa eneo lote na Ubungo,kuanzia "Mataa" mpaka darajani,TANESCO imeweka mabango ya matangazo kuzuia biashara na mkusanyiko wa watu,lkn raia wameendelea kuuza mitumba,mbogamboga,nyanya na bidhaa mbalimbali licha ya tahadhari hilo iliyo kwa namna ya maandishi.
Leo hali ilikuwa tofauti,mara baada ya waya huo kudondoka na kuwakosakosa kina mama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo eneo hilo,baada ya ajali hiyo,wananchi walifanikiwa kupiga simu kitengo cha Dharula cha TANESCO walifika na kuzima umeme na hivyo kutoa nafasi kwa wananchi kuuzima moto.