Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,159
- 4,443
Hivi mmiliki anahusika vipi?Wadau ndani ya Jf
kila nisikilizapo habari kupitia vituo mbalimbali watu na hata wafanyakazi wa bandalini wamekuwa ni wazito kuwataja wamiliki wa meli iliyozama
kwani kuna nini hapa? yaani hata viongozi wa wakuu wa serikali pia wamesikika wakiwa na kigugumizi cha kuwataja wahusika tunachosikia ni kuwa meli ilitengenezwa mwaka 1966 na wamiliki walikuwa wakibadilishana umiliki siku hadi siku
lakini mmiliki wa mwisho hadi meli ina zama amekuwa kama mungu kila mtu anaogopa kumtaja
kweli Tanzania tumefikia hapa tulipo kwa kuwaficha waliotuumiza?
wadau tunaomba tujue majina kamili ama kampuni iliyokuwa ikimiliki meli hiyo
KARIBUNI