Ajali ya Helkopta yaua mawaziri Kenya!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Ajali ya Helkopta yaua mawaziri Kenya!
Sunday, June 10, 2012 | Lebel feature, habari muhimu, Maganga Media, news, picha | Posted by Maganga Media


Imethibitishwa kuwa Waziri wa usalama wa taifa wa Kenya George Saitoti pamoja na msaidizi wake Joshua Ojode ni miongoni mwa watu saba waliofariki dunia kwenye ajali ya helicopter ya Polisi iliyotokea kati ya saa tatu au saa tano leo asubuhi huko Ngong Kenya. Chanzo cha ajali ni kutokana na hali mbaya ya hewa ambapo helicopter hiyo ilikua na marubani wawili akiwemo mmoja wa kike.


.
Waziri wa Usalama wa ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Waziri Saitoti


Abiria wote sita, wakiwemo marubani wawili na walinzi wa mawaziri hao waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.


Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.


Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong. Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.


Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso.
.
.
.
.
DSC05764-800x600.jpg

.
.
.
DSC05743-800x600.jpg

.

120610083600_saitoti_304x171_reuters.jpg





DSC05744-800x600.jpg



DSC05748-800x600.jpg




DSC05749-800x600.jpg





DSC05751-800x600.jpg





DSC05752-800x600.jpg



DSC05753-800x600.jpg



DSC05754-800x600.jpg




DSC05757-800x600.jpg



DSC05760-800x600.jpg




DSC05762-800x600.jpg



DSC05763-800x600.jpg



DSC05765-800x600.jpg



DSC05768-800x600.jpg


DSC05739-800x600.jpg




DSC05740-800x600.jpg





Waliofika kwenye eneo la tukio.
.
.MAONI YAKO
Maganga Media: Ajali ya Helkopta yaua mawaziri Kenya!
 
Mkuu MziziMkavu...kwakuwa hii sio habari mpya tena nadhani TITLE ingefaa kuwa: PICHA ZA AJALI ILIYOUWA MAWAZIRI KENYA......
 
Back
Top Bottom