Ajali Mbinga-Ruvuma: Gari lapata ajali na kuua Padre mmoja na Makatekista sita

Oooooh my Lord!
Landrover 110 station wagon inapakia watu zaidi ya 28, wakifa bado mnasema wamekufa ka mipango ya Mungu!
 
Hivi si tunaambiwa kuwa Yesu aliuawa kwa ajili ya dhambi za wanadam sasa dhambi gani tena mungu awasamehe.

Tunaendaga kutubu nini? Ata Yesu alikuwa anawaondolea dhambi walikuwa tayari ingawa haimanishi watu wasio kuwa tayari kutubu na kuziacha njia zao mbovu hawakutakiwa....! Kwa neema na rehema za Mungu tutasamehewa!
 
Naomba watu wasichanganye hapa, shule inayoongelewa si kigonsera bali hapo kigonsera jirani na hiyo sekondari ya kigonsera kuna shule nyingine ya sekondari ya makatekista maarufa kama shule ya fr. kawonga ndiyo inayoongelewa hapa!
 
Raha ya milele uwape Ee BWANA na mwanga wa milele uwaangazie, wapumuzike kwa amani.AMINA.

Ninawaombea nafuu ya mapema wale wote waliojeruhiwa.
 
Hii habari hebu iwekeni vizuri ni padre na watumishi wake au mwalimu na wafunzi wake mbona habari inajichanganya!au ni mimi ndio sijaelewa!

Ni padri na wanafunzi wa form two ambao hawakwenda likizo. Huyo Padri Kawonga aliwahi pia kuwa Paroko wa parokia ya Mpepo (namfahamu personally). Nina ndugu yangu pia ambae mtoto wake amenusurika na amelazwa hospitali ya Mbuyula (MBINGA).
 
Naomba watu wasichanganye hapa, shule inayoongelewa si kigonsera bali hapo kigonsera jirani na hiyo sekondari ya kigonsera kuna shule nyingine ya sekondari ya makatekista maarufa kama shule ya fr. kawonga ndiyo inayoongelewa hapa!

Uko sahihi, hiyo sio Kigonsera Sec. School.
 
Wamefariki watu situ ambao ni mmiliki wa shule aliyekuwa anaendesha gari na wanafunzi watano wa kidato cha nne na pili ambao walibaki shule
 
Back
Top Bottom