Ajali imetokea Buza Mwisho wa Lami

ankol

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
2,113
3,489
Watu wa tatu wanahofiwa kufa katika ajali ilitotokea usiku huu maeneo ya Mwisho wa lami Buza.

Gari hiyo aina ya Scania tanker imefeli kona na kuwaparamia wafanya biashara waliokua pembezoni mwa barabara.

Credits kwa jeshi la polisi lililofika ontime na kufunga barabara na kuwatawanya watu la sivyo madhara makubwa yangetokea ikiwamo mlipuko.

Pichani tanker jingine kulia likifaulisha mafuta ya petrol kutoka kwenye tanker lililopata ajali kushoto.

20230805_211040.jpg

___
DAR ES SALAAM: WATU wawili wanahofiwa kufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyotokea leo Agosti 5 katika barabara ya #Buza, Mwisho wa rami ikihusisha lori la mafuta lililoacha njia na kupinduka.

Mashuhuda wameiambia #DailyNewsDigital kuwa hiyo ni ajali ya pili kwa mwaka huu ikihusisha lori la mafuta kushindwa kukata kona na kupinduka. Hadi sasa (Saa 5:30 usiku) lori hilo bado halijaondolewa na kwamba halijashika moto.

Jeshi la #Polisi na kikosi cha #zimamoto na uokozi hakijazungumzia ajali hiyo. Hata hivyo Wakazi wa eneo hili wanasema ufinyu wa barabara, ongezeko la yadi na wafanyabiashara kando ya barabara kinaweza kuwa chanzo kikuu cha ajali katika eneo hilo ambalo linashuhudia ongezeko la magari na mengi yakiwa malori mabovu.
 
Si ndio wanapaita tanesco kwa mbele kuna chimbo la mdudu??
Yah ndio hapo mdau. Ajabu pamoja na ubize wote pale watu walisukumiwa mtaroni tu lakini hakuna madhara zaidi ya hao marehemu watatu.

Note pia kuna stand ya daladala lakini mida hiyo njia ilikua nyeupe. Ashukuriwe Sir God.

Hata mafuta yaliyoanza kuvuja yalikua upande wa chamber ya diesel na wala si petrol.
 
ILE CORNER YA MWISHO WA LAMI PALE NI MBAYA SANA HASA KWA MAGARI YANAYOTOKA BUZA KUELEKEA UELEKEO WA AIRPORT

WAFANYABIASHARA WASIKAE PALE
 
Back
Top Bottom