Ajali Ifakara mjini: Basi na treni zagongana, watu wahofiwa kupoteza maisha

Sijui tuwafanyeje madereva wa inji hii. Hili ni janga kubwa! Hata ukiwa Dar unaendesha gari, ukipunguza mwendo tu unapokaribia reli ili uangalie kabla ya kuvuka utasikia nyuma yako unapigiwa honi balaa, na pengine wataku-overtake kwa fujo! Nachotaka kusema hapa ni jinsi madereva wengi wasivyojali umakini wakati wa kuvuka reli.
 
Duh........matukio hayaishi nchi hii.
Nini kifanyike?
Male mahali pema peponi wapendwa.
 
Rip wote uendeshaji wa magari inabidi wawe makini wengi wa madereva huwa wanakua na haraka kuliko upesi
 
Basi ya kampuni ha AL JABIR inayofanya safari kati ya Dsm na Ifakara imegongana na Treni maeneo ya Kiberege, watu zaidi ya 40 wamepoteza Maisha!

Mji Wa Ifakara wazizima, vilio kila kona

Habari zaidi na picha zitawajia karibuni

Huwaga sielewi kwanini huwa mnakuza ivi idadi ya vifo! Au ulitamani wafe zaidi ya 40?!
 
Daah ajali hizi zinatumaliza , mungua azilaze roho za marehemu mahali pema amina
 
Ajali haina kinga kaka! Fikiri kabla hujapost! Hakuomba kuua wenzake!

Mkuu ajali nyingi zinazotokea ni zenye kuzuilika kabisa.. Kama tungekuwa na mifumo mizuri ya miundo mbinu pamoja utii wa sheria asilimia 99 ya ajali za barabarani zisingetokea.. Unapoendesha basi huku umelewa na kupata ajali huwezi kusema ati ajali haina kinga..! Au unapoendesha kwa speed ya 90 mph sehemu ambayo inatakiwa speed limit ya 30 mph na ukapata ajali huwezi kusema ati ajali haina kinga..

Kama dereva ameendesha basi huku amelewa na akasababisha ajali ni wazi huyo amedhamiria kuwaondoa uhai binadamu wenzie..
 
Ajali haina kinga kaka! Fikiri kabla hujapost! Hakuomba kuua wenzake!

aliyepost anazungumzia qualification za madereva wa public transport ziboreshwe wewe hossam unazungumzia nini?
 
Basi ya kampuni ha AL JABIR inayofanya safari kati ya Dsm na Ifakara imegongana na Treni maeneo ya Kiberege, watu zaidi ya 40 wamepoteza Maisha!

Mji Wa Ifakara wazizima, vilio kila kona

Habari zaidi na picha zitawajia karibuni

Mbona TBC saa 2 inasema 13 wamefariki na 40 wamejeruhiwa.
 
Back
Top Bottom