Ajabu Hii ya Haki Iliyotolewa na Ibara Moja ya Katiba, Kuporwa na Ibara Nyingine, Ilifanyika Vipi Huku Tuna Washeria Manguli, Wabobezi na Wabobevu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,626
Wanabodi,
Makala ya Jumapili ya Tarehe 22./01/2023\
Screen Shot 2023-01-23 at 7.25.19 AM.png
Screen Shot 2023-01-23 at 7.33.53 AM.png

Leo naendelea na sehemu ya pili ya mada ya wiki iliyopita kuhusu haki kuu mbili za kisiasa zilizotolewa na katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977, na jinsi haki hizo zilivyotolewa na kifungu kimoja, halafu serikali yetu ya wakati huo, ikaja kuzipora kwa kuzitungia sheria batili, na baada ya ubatili huo kubatilishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, serikali hiyo ikafanya kitu cha ajabu, kwa kuupeleka ubatili huo Bungeni, kwa hati ya dharura, na kuliomba Bunge kufanya mabadiliko ya katiba ambayo nayo ni batili, kisha ubatili huo ukachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu ili kuihalalisha batili hiyo!. Haya yote yalifanyika huku Tanzania ndio nchi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki kufundisha somo la sheria, hivyo tuna manguli wa sheria wabobezi na wabobevu, makala hii inauliza, haya madudu ya ajabu hivi, yaliwezekana vipi kufanyika na huku tuna wanasheria hao manguli wabobevu na wabobezi wakiangalia?!.

Kwa wasomaji wapya, anzia hapa Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Kwa mujibu wa ibara ya 64.-(1) Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania yatakuwa mikononi mwa Bunge la JMT. Ila ibara ya 64.- (5) inasema Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka Katiba itakuwa batili.

Tafsiri ya ibara hii kwa mtu wa kawaida ni katiba ndio sheria mama, ikitokea sheria nyingine yoyote iliyotungwa, ikikinzana na katiba, sheria hiyo nyingine inakuwa ni batili automatically, kisheria wanaita null and void ab initio, yaani sheria hiyo batili inakuwa ni kama haipo na haijawahi kuwepo!.

Ibara ya 64 inazungumzia kitu kinachoitwa "the supremacy of the constitution" kumaanisha Katiba ndio sheria Mama, sheria yoyote nyingine itakayo kwenda kinyume cha katiba, sheria hiyo ni batili. Ubatisho huo umefanywa na katiba yenyewe na sio Mahakama Kuu!.

Kazi ya Mahakama ni kutafsiri sheria, baada tuu ya Mahakama Kuu Kuu kuthibitisha sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, sheria hiyo inakuwa imebatilika pale pale kwa mujibu wa Ibara ya 64!. Anayebatilisha sheria batili sio Mahakama Kuu, ni katiba yenyewe!. Kazi ya Mahakama Kuu ni kuthibitisha tuu ubatili na ukiisha thibitishwa, sheria hiyo batili inakuwa imebatika automatically!.

Sheria iliyobalika automatically maana yake ni haipo hivyo hakuna rufaa!. Baada ya kubatilishwa, kazi ya serikali na Bunge ni kurekebisha na kuifuta from the books, na sio kuikatia rufaa batili!.

Ibara ya 5 ya katiba imetoa haki kuu kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofaywa Tanzania. Haki hii ya kuchagua, inakwenda sambamba na haki ya kuchaguliwa kwa mujibu wa ibara ya 21.-(1) kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao.

Haki hizi mbili zilizotolewa na katiba, japo haki ya kuchagua bado ipo, lakini haki ya kuchaguliwa imeporwa kwa kuwekwa shurti batili kwenye ibara ya 39 na 67 kwa shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa!. Wakati wote wa kuwekwa kwa ubatili huu ndani ya katiba yetu, Tanzania tulikuwa na wanasheria tena ma nguli wabobezi na wabobevu, kuanzia serikalini, bungeni na mahakamani!.

Kumefanyika mambo makubwa Sita
  1. Kwanza umetungwa muswada sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba. Sheria ya Uchaguzi Act. No. 1 ya mwaka 1985. Mchakato wa utungaji wa sheria unawahusisha wanasheria na unaanzia serikalini, ilikuweje kuweje, wanasheria wetu, wakatunga sheria batili inayokinzana na katiba!, hawa wanasheria walio draft sheria hiyo batili ni wanasheria wa aina gani?
  2. Muswada huo wa sheria batili ukatua Bungeni, nako kuna wanasheria manguli, wabobezi wabobevu. Bunge letu tukufu la JMT, likatunga sheria batili hiyo ya uchaguzi. Mchakato wa utungaji sheria wa Bunge pia unahusisha wanasheria kwa kila hatua chini ya mwanasheria mkuu wa serikali kuhakikisha kila sheria inayotungwa na Bunge letu lazima iendane na katiba!, sheria hii batili ya uchaguzi iliwezekanaje kutungwa ili hali Bunge letu limeshehenezwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu?.
  3. Mchungaji Mtikila (Mungu amrehemu) mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, kupinga kipengele kinachomtaka mgombea uchaguzi kudhaminiwa na chama cha siasa. Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Kahwa Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi.
  4. Mahakama Kuu inapotamka sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, kipengele hicho kilipaswa kufutwa pale pale kwa mujibu wa ibara ya 64.- (5) katiba itekelezwe pale pale kwa sheria hiyo kuwa batili kuanzia ilipotangazwa, na ni mara baada ya uamuzi huo wa mahakama kuu kuutangaza ubatili huo, ndipo sarakasi za mambo ya ajabu ya kisheria zilianza!. Mtu anapokutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo jela, hupelekwa jela, kuanza kutumikia kifungo hata kama kama atakata rufaa. Hivyo uamuzi huu wa mahakama ulipaswa kuanza kutekelezwa pale pale!.
  5. Kama katiba ndio sheria mama, Mahakama Kuu chini ya Jaji Lukakingira, ikatamka sheria hiyo ni batili, kwasababu inakwenda kinyume cha katiba, mamlaka pekee nchini Tanzania, yenye mamlaka ya kutafsiri sheria na kueleza ubatili wa sheria yoyote ambayo inakwenda kinyume cha katiba, ni Mahakama Kuu ya Tanzania, baada ya hukumu ya Jaji Lugakingira, ni wanasheria wa aina gani walioishauri serikali kukata rufaa?.
  6. Hili ni tundu kwenye paa letu la mhimili wa Mahakama, baada ya mahakama kuutangaza ubatiliti huo, kitu kikisha kuwa batili, ni ni kama hakipo na hakijawahi kuwepo!, hatua ya kwanza ni kwanza hiyo sheria kubadilishwa kwa kuwa null and void ab initio, hivyo ilibidi ifutwe pale pale!.
Hapa sasa serikali yetu tukufu ya JMT ya wakati huo, baada ya kubwagwa mara mbili mahakamani, ambapo Mahakama Kuu ilitimiza wajibu wake kikamilifu, kwa kuhakikisha ubatili huu unakoma na unaondoshwa!, mambo hayakuishia hapo, badala ya serikali yetu kuuondoa ubatili huo, ndio kwanza ilianzisha sarakasi fulani ya ajabu sana!. Jee serikali yetu ilianzisha sarakasi gani kwenye hili?, tukutane wiki ijayo kwa sehemu ya tatu na ya mwisho ya haki kuu ya kikatiba ya Watanzania, iliyotolewa na kifungu kimoja cha katiba, halafu ikaja kuporwa na kifungu kingine batili cha katiba hiyo hiyo, kilichochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!, na ubatili huo bado ungalipo ndani ya katiba yetu hadi leo ninapoandika makala hii na walioyafanya yote hayo ni wanasheria manguli wetu ambao ni wabobezi na wabebovu, wakiongozwa na wanasheria wa serikali yetu, kisha Waheshimiwa Wange wetu wakabariki!, Mahakama Kuu ya Tanzania, ukaupinga ubatili huu, lakini Mahakama ya Rufani ikaja kufanya kitu cha ajabu sana kuliko!. Tunataka jicho la haki la Rais Mama Samia, liuangazie. ubatili huu!.

Wasalaam.

Paskali
Rejea mbalimbali za mwandishi huyu kuhusu haki katiba "Kwa Maslahi ya Taifa"
  1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
  2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  3. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
  4. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
  5. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
  6. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  7. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
  8. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  9. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  10. Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
  11. Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
  12. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
 
Sioni kwanini unawalaumu wanasheria "manguli" waliopita kutolifanyia kazi tatizo unaloliona ikiwa hata leo hii nanyi mpo?

Watafute wenzako muende mahakamani kupinga unacholalamikia, lakini kitendo cha kutupa lawama kwa wanasheria waliopita kinaonesha hamjiamini, wengi wenu vilaza.
 
Ukwel ni kwamba.. kiongozi wa nchi ndo kila kitu. Weka ndan yule, mtoe flan magereza, wee tumia pesa hata bila kuidhinishwa na bunge haina shida!! Ufuataj wa sheria kusimamia sheria Tanzania bado sana!!!
 
Tunataka jicho la haki la Rais Mama Samia, liuangazie. ubatili huu!.

Wasalaam.

Paskali

Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Back
Top Bottom