Airtel yadaiwa mamilioni kortini

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,554
Kampuni ya Airtel imepandishwa kizimbani ikidaiwa fidia ya Sh490 milioni kwa kuitumia sauti ya Nixon Bandago Haule kwenye tangazo la ‘Airtel the Smartphone Network.’

Kesi hiyo imefunguliwa na Haule Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam anayedai sauti inayosikika katika kaulimbiu hiyo na kutumika katika matangazo ya kibiashara ya Airtel ni yake lakini hakutoa ridhaa itumike.

Kwa mujibu wa hati ya madai, kiapo na nyaraka nyingine alizoziwasilisha mahakamani, Bandago anadai kuwa aliingia makubaliano ya awali na ofisa wa Airtel aitwaye Arnold Madale Oktoba mosi mwaka 2017 na baada ya kurekodi sauti aliambiwa asubiri iidhinishwe na menejimenti ili wasaini mkataba jinsi itakavyotumika, muda na haki nyinginezo anazostahili.

Katika hali ya kushangaza, anasema alianza kuisikia kaulimbiu hiyo yenye sauti yake katika vituo vya redio na runinga bila makubaliano yoyote kufanyika hivyo anaiomba mahakama iamuru kuwa mdaiwa alivunja hakimiliki zake.

Sh490 milioni za fidia anayoiomba zinajumuisha Sh390 milioni za hasara aliyoipata kwa ukiukaji huo wa haki miliki na Sh100 milioni kama riba.

Katika majibu yake, Airtel imekana kuwa na mkataba naye wa kutengeneza tangazo hilo isipokuwa ina mkataba na kampuni ya Oglivy Tanzania Limited tangu Novemba 18 mwaka 2015 kwa shughuli zote za masoko na matangazo ya kibiashara kwenye vyombo vya habari.

Airtel imesema Mandago aliingia mkataba na kampuni ya Oglivy Mei 10 mwaka 2018 na akaridhia sauti yake kutumiwa na Oglivy na au wadau wake kwenye matangazo yake na katika kampeni zake za kibiashara kwa malipo ya Sh600,000 jambo ambalo Mandago anasisitiza alikuwa ofisa wa Airtel.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa atashindwa kwenye mkataba maana mkataba hakuingia na kampuni ya AirtelTz bali kampuni ya oglivy.
Kesi nyepesi hiyo.
 
-kwa hiyo unataka kusema kwamba atashindwa kesi kwa kigezo hicho?
-hujui kwamba ataomba ruhusa arekebishe hati ya madai halafu kesi iendelee?
 
Airtel imesema Mandago aliingia mkataba na kampuni ya Oglivy Mei 10 mwaka 2018 na akaridhia sauti yake kutumiwa na Oglivy na au wadau wake kwenye matangazo yake na katika kampeni zake za kibiashara kwa malipo ya Sh600,000 jambo ambalo Mandago anasisitiza alikuwa ofisa wa Airtel.
hakuna kesi hapo, kuchoshana tu
 
Kampuni ya Airtel imepandishwa kizimbani ikidaiwa fidia ya Sh490 milioni kwa kuitumia sauti ya Nixon Bandago Haule kwenye tangazo la ‘Airtel the Smartphone Network.’

Kesi hiyo imefunguliwa na Haule Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam anayedai sauti inayosikika katika kaulimbiu hiyo na kutumika katika matangazo ya kibiashara ya Airtel ni yake lakini hakutoa ridhaa itumike.

Kwa mujibu wa hati ya madai, kiapo na nyaraka nyingine alizoziwasilisha mahakamani, Bandago anadai kuwa aliingia makubaliano ya awali na ofisa wa Airtel aitwaye Arnold Madale Oktoba mosi mwaka 2017 na baada ya kurekodi sauti aliambiwa asubiri iidhinishwe na menejimenti ili wasaini mkataba jinsi itakavyotumika, muda na haki nyinginezo anazostahili.

Katika hali ya kushangaza, anasema alianza kuisikia kaulimbiu hiyo yenye sauti yake katika vituo vya redio na runinga bila makubaliano yoyote kufanyika hivyo anaiomba mahakama iamuru kuwa mdaiwa alivunja hakimiliki zake.

Sh490 milioni za fidia anayoiomba zinajumuisha Sh390 milioni za hasara aliyoipata kwa ukiukaji huo wa haki miliki na Sh100 milioni kama riba.

Katika majibu yake, Airtel imekana kuwa na mkataba naye wa kutengeneza tangazo hilo isipokuwa ina mkataba na kampuni ya Oglivy Tanzania Limited tangu Novemba 18 mwaka 2015 kwa shughuli zote za masoko na matangazo ya kibiashara kwenye vyombo vya habari.

Airtel imesema Mandago aliingia mkataba na kampuni ya Oglivy Mei 10 mwaka 2018 na akaridhia sauti yake kutumiwa na Oglivy na au wadau wake kwenye matangazo yake na katika kampeni zake za kibiashara kwa malipo ya Sh600,000 jambo ambalo Mandago anasisitiza alikuwa ofisa wa Airtel.

Chanzo: Mwananchi
Ya akina FA ilikuwa hivi hivi na walipiga b2
 
Serikali isipoingilia kati hii michezo, itazaa mizizi vibaya mno. Hizi case nyingi ni mashirikiano ya njama kati ya watu ndani ya taasisi na outsiders in expectation ya x% baada ya ushindi.
 
Back
Top Bottom