Ahadi ya mzee kikwete hiyo

waandishi wetu wa habari walivyo wajinga utakuta hakuna mtu hata mmoja aliyekwenda kufuatilia issue za huyu mama
 
Taking the extreme cannot justify your point. What about extremees of homeless in America??????

Homeless in USA.jpg
 
Alafu utawaskia watu wanawatetea ccm umumu sijui wanakua na akili zipi hasaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 


Katika kitabu chake "NO HIGHER HONOR" aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa marekani anasema viongozi wa nchi za kiafrika wanaiba fedha za misaada ambazo zingewahudumia wananchi wao na badala yake wanawanunulia wake zao [jewellery] dhahabu na vito vya gharama kubwa sana!!
 
Rais wetu ni taswira ya jinsi Watanzania tulivyo, otherwise kwa nini alichaguliwa 2005 na ataendelea kuchaguliwa tena 2010? Kama Rais ni msanii, ina maana wengi wetu ni wasanii, kama Rais wetu anatoa ahadi hewa, wengi wetu huwa tunatoa ahadi hewa, nk.

Umesema kweli, tungekuwa serious tungechagua Mtu serious.

Tusingepokea tulichopewa wakati wa kampeni, tusingemchagua aliyetupa ushawishi wa pilau, kanga na Tshirts ili apate kura.

Walivyotoa rushwa ina maana wanapokea rushwa.

Tungekuwa watu tunaowajibika, tungemuwajibisha kwa kushindwa kwake.

I entirely agree
 

[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif][/FONT]​
Maisha ya Mtanzania ni matamu lakini ni mafupi mno.
 

Attachments

  • Maisha bora kwa kila  Mtanzania.jpg
    Maisha bora kwa kila Mtanzania.jpg
    54.5 KB · Views: 307
[h=3]Maisha bora kwa kila mtanzania: Embe la Sh. 100 lasababisha vijana kutaka kutoana roho Mbeya.[/h]

[h=3][/h]
JAMAA KAZIMWA MIA YAKE YA EMBE AAMUA KUANZISHA NGUMI YAANI SASA MAEMBE YOTE YAMETAWANYIKA NA NGUMI ZINAENDELEA

<tbody>
</tbody>



KUSAIDIANA IPO JAMAA MWINGINE AINGILIA UGOMVI KAZI IPO HAYA NDIYO MAISHA YA BAADHI YA VIJANA HUKO MANOW RUNGWE Baba V

<tbody>
</tbody>

 
Last edited by a moderator:
Maisha bora kwa kila Mtanzania ni dhahiri wengine hatumo

WALIOSEMA maisha ni safari ndefu, sina budi kuwapongeza kwa maana katika hali ya kawaida ya maisha yetu sisi Watanzania na hususan katika kundi hili la watu wa kipato cha chini, kwa kweli kila kukicha kuna mikiki kibao ambayo kwa njia moja au nyingine inatuongezea ugumu na urefu wa safari ya maisha yetu ya kila siku.

Ukigeuka huku bei ya mafuta juu, nauli za daladala nazo hazieleweki hasa inapofika muda wa jioni utaona kila njia na nauli zake, ukienda hospitali za serikali ndiyo kabisaa, huduma kibao hakuna hivyo kama huna kitu ujue matibabu hupati.

Kwa ujumla kila upande unaomzunguka Mtanzania wa kipato cha chini ni matatizo matupu kana kwamba hakuna mamlaka husika zinazotakiwa kulifanyia kazi jambo hilo !

Kwa kawaida kama siku inatokea kukuanzia vizuri, bila shaka siku hiyo huonekana ni fupi sana kwa jinsi ambavyo saa zinavyokatika kwa ulaini, lakini kama mambo yanakuwa hayajakaa mkao wa kula kwa upande wako, hapo ni dhahiri hata dakika moja kati ya zile sitini za saa, utaiona ni ndefu kwako.

Hebu jaribu kufikiria mwenyewe, ni jinsi gani wale waliopo magerezani, hospitalini, vitani na kwigineko wanavyopata tabu kuivuka dakika moja ya saa wakati wewe mwenzangu na mimi ukiendelea kuinyonya bia yako kiulaini kwa kuagiza moja moto na moja baridi.

Ni dhahiri hamuwezi kuwa katika hali moja, wewe utaendelea kupeta wakati wenzako wakiwa katika machungu makali ya kuivuka kila dakika ya saa kwa manung’uniko na masikitiko makubwa.

Hivyo hivyo ndivyo sisi Watanzania wengi wa kipato cha chini au kwa jina lililowahi kupata umaarufu sana miaka kadhaa ya nyuma yaani ‘walalahoi’ tunavyoendelea kugombana huku Uswahilini kwa kunyang'anyana makopo ya kuendea msalani wakati wale wenye nyadhifa zao kubwa na vipato vya kutisha vya halali na vya kifisadi wakiendelea kupeta katika mahekalu yao huko maeneo yenye sifa zote za miundo mbinu mizuri kwa maisha ya bianadamu.

Vile vile wale Watanzania wenzetu kwa uraia, lakini wasiotaka hata siku moja kujifunza lugha ya Kitanzania (Kiswahili) ambayo ni kigezo kimojawapo cha Utanzania nao wakiendelea kupeta huko maghorofani kwa huyo bwana mkubwa National Housing Corperation (NHC) kwa kulipa pesa kidogo ya pango ukilinganisha na kodi kubwa za makazi yetu ya hovyo ya Uswahilini!

Walionena huko nyuma kuwa aliyenacho huongezewa kwa kweli wangekuwa hai ningejikakamua kwa kila hali ili niwatafutie tuzo yoyote ile hata kama ni ya kilalahoi kwa jinsi ambavyo ukweli wa usemi huo unavyojidhihirisha waziwazi katika jamii yetu ya Kibongo.

Enyi mlio nazo, nia yangu siyo kupiga debe ili mpandishiwe kodi, la hasha, nia yangu muondolewe kabisa katika nyumba hizo ili mkakae kwenye nyumba zenu mlizozijenga huko Mbezi Beach na Masaki.

Nyinyi mnaodai kuwa ni wenzetu kiuraia lakini cha ajabu hata hicho Kiswahili ambacho ndio lugha ya taifa hili hamtaki kukiongea kwa kisingizio kuwa hamkijui, kwa kweli nyinyi ndio mnaotakiwa muondoke kabisa, kwa maana tunaelewa fika kama ni pesa mnazo nyingi sana .

Kwa hali hiyo kwanini mwendelee kuachiwa mkae katika nyumba hizo za bei nafuu ambazo zingefaa zitumiwe na wafanyakazi wenye kipato kidogo badala yake wanakaa wale wale wasiokuwa na shida ndogo ndogo na kama zinatokea basi ni zile za kujiuliza leo twende tukatanue bichi gani, Osyterbay au Bagamoyo?

Wewe mwenzangu na mimi ambaye mshahara wako haukufikishi hata mwisho wa wiki ya kwanza ya mwezi, hapo hapo ukitaka kwenda kuoga ni lazima upange foleni, haya tumbo nalo likikukusumbua, inabidi upange foleni pia, LUKU inapokwisha ndio balaa--hailipwi hadi mkunjane mashati na wapangaji wenzanko, ukigeuka nyuma mzee mwenye nyumba huyu hapa, kodi inabidi itolewe.

Kwa kifupi kila ugeukiapo ni matatizo matupu! Ukijiuliza hivi ile kauli mbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania na wewe ulikuwemo katika orodha hiyo ya hao wanaoitwa kila Mtanzania au kuna watu wengine mbali kabisa na wewe wanaostahili kuitwa kila Mtanzania?

Binafsi nafikiri kila Mtanzania lilikuwa ni fumbo fulani kwa ajili ya watu fulani ambalo sisi wengine hatujaweza kulifumbua, ila ni kwamba hatupo wote, wapo wanaostahili kuitwa kila Mtanzania.

Ukijaribu kupiga hesabu zako unagundua kuwa mshahara wako hauwezi kukuwezesha kufanya jambo lolote lile la ziada zaidi ya pesa yako kuishia katika mzunguo huo wa kutatua matatizo ya nyumba unayoishi kabla hata matatizo yenyewe hayajaisha, sasa hayo maisha bora kwa kila Mtanzania na sisi tumo kweli? Jibu lazima liwe hapana.

Hivi ni ufanisi wa aina gani utakaotegemwa kutoka kwa mtu wa aina hii ambaye nyumbani anakoishi amezungukwa na kero kibao, ili aende ofisini ni lazima apambane na kasheshe kibao za usafiri wa daladala, akifika ofisini kazi kibao lakini tarehe ya mshahara haijulikani.

Akiwaangalia mabosi wake kila siku wapo kwenye semina na warsha huku wakilipana posho kibao, wakati wa kurudi nyumbani adha ya usafiri ndio usiseme, mbali ya kugombania hizo daladala pia nauli zake nazo huongezeka kila giza linapozidi kutanda!

Sasa kwanini mtu wa aina hii asiwe na hasira na watawala ambao hawaonekani kabisa kujali hali ngumu za maisha ya Mtanzania wa kipato cha kati na cha chini?

Haipendezi na inaumiza sana wakati haya mateso yote yanamkaba mtu wa kipato cha chini na cha kati, lakini mafisadi waliofisadi rasilimali zetu Watanzania wakiendelea kupeta kana kwamba wao ndio wenye haki zote na nchi hii huku sisi wengine tukiwa ni wasindikizaji wao tu!

Hayo si mambo kabisa, hii kauli mbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania wakati katika hali halisi wengine tunazidi kutaabika kila siku zinavyosonga mbele ni heri ifutwe kabisa.


 
Back
Top Bottom