AG Werema alishastaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria

na fedha za umma alizopoteza kwa kusamehe kodi (na alikiri bungeni kwamba yeye ndiye aliyewapotosha muhongo na maswi) hatazirejesha?
Mkuu Tpaul, hapa unaongelea swala la uwajibikaji ambalo kwa serikali ya Prof. Kikwete ni ndoto ya mchana. Mtu aliwaambia wezi wa EPA warudishe hela na kutambaa atamwajibisha mwanasheria mkuu wa serikali kweli? Na hata haya maneno ya kusema familia yake au watu wake wa karibu wanahusika na hii ESCROW si ndiyo inakuwa giza kabisa no kuwajibishana
 
Hata kama amekwisha staafu anapaswa apandishwe kizimbani kwa kulisababishia hasara ya mabilioni ya kodi ambayo ilipaswa kulipwa. Ataungana na akina Mramba, Yona na wengine!
 
Kwa mnaosubiri miujiza toka kwa JK juu ya kuwawajibisha wahusika wa sakata la TEGETA ESCROW ni vema mkatambua kuwa AG Werema alishastaafu kwa mjibu wa sheria tokea November 30 2014.

Hivyo basi mtakaposikia anatangazwa AG mwingine msijedhani kawajibishwa.

Kwa ninavyomwelewa mkuu wa kaya ni kuwa atatangaza AG mwingine bila kuongea chochote kuhusu Werema ili watu muamini kwamba kamuwajibisha.
Ala !!! Kumbe ndio maana alikuwa anaomba tena kwa kujiamini na kiburi juu kwamba ashughulikiwe yeye wengine wasiguswe kwa kuwa alijua amekwisha ondoka madaraka!!!!!. Ahsante mkuu kwa kunifungua macho
 
Ala !!! Kumbe ndio maana alikuwa anaomba tena kwa kujiamini na kiburi juu kwamba ashughulikiwe yeye wengine wasiguswe kwa kuwa alijua amekwisha ondoka madaraka!!!!!. Ahsante mkuu kwa kunifungua macho
Ndoo kilikuwa kiburi chake mkuu. Ila kwa tamko la wamarekani wa MCC walitoa jana nadhani anaweza jikuta mbele ya pilato pia maana wazungu hawana mchezo
 
Lakini hela zetu za Eskoro si atarudisha?? na jela si laziama aende??
lets wait for the miracle..nasema miracle kwa sababu vyombo vyet vya dola vimezoea kuwashitakai na kuwafunga wezi wa kuku na mbuzi,sio wzi wa pesa za umma.
 
Prof wetu wa kichina ana ushemeji na Mungu! Hata tezi dume ni mwendelezo wa utani huo! Escrow itakuwa majibu yake ya utani kwa muumba wake. Atapiga tabasamu la kisanii kisha kuomba dua mjengoni magogoni. Hapo mchezo utakuwa umeisha akidhani wadanganyika ni wajinga kama wa pale Msoga!

Mkuu inawezekana sisi wadanganyika ni wajinga ila wajuaji wamegomea hela zao hapo ni wanatonesha tezi dume mpaka hela zirudi serikalini
 
Kwa mnaosubiri miujiza toka kwa JK juu ya kuwawajibisha wahusika wa sakata la TEGETA ESCROW ni vema mkatambua kuwa AG Werema alishastaafu kwa mjibu wa sheria tokea November 30 2014.

Hivyo basi mtakaposikia anatangazwa AG mwingine msijedhani kawajibishwa.

Kwa ninavyomwelewa mkuu wa kaya ni kuwa atatangaza AG mwingine bila kuongea chochote kuhusu Werema ili watu muamini kwamba kamuwajibisha.
usanii tumechoka tuchukue maamuzi magumu mwakani kuipiga chini ccm ndio mpango mzima
 
hII karata ya Prof Tezi sijaelewa

Je Werema atawajibishwa? au ndio amejiudhuru basi imetoka?

Hii nchi bwana eti mtu unashiriki wizi lakini RAISI ANAKUSHUKURU KWA UTENDAJI:sick::sick:
 
I told y'all.

Inadaiwa kuwa Jaji Werema alizaliwa Oktoba 10, 1954.

Kama ni kweli basi ukipiga mahesabu ya haraka haraka leo atakuwa amefikisha umri wa miaka 60, miezi miwili na siku 7.

Kama muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ni miaka 60, basi atakuwa amejiuzulu baada ya muda wake wa kustaafu kupita.

Au inawezekana kwa ndani amestaafu kwa mujibu wa sheria lakini kwa nje tunaambiwa kuwa amejiuzulu.

Kama Escrow inawezekana Tanzania basi kila kitu kinawezekana.
 
Rekebisho: werema kazaliwa 1951 ninamfahamu binafsi. Aliachiwa aendelee ili aondoke na JK 2015.
 
Back
Top Bottom