SoC03 Afya za Watu na Mahitaji ya Jamii

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Teknolojia za kidijitali ni sehemu ya Maisha yetu, na zina uwezo mkubwa sana wa kuboresha afya-za-watu iwapo zitatumika katika sekta-ya-afya.

Mkakati-wa-kimataifa kuhusu Afya ya Kidijitali (tazama bit.ly/digi-WHO), uliopitishwa mwaka wa 2020 na Baraza-la-Afya-Ulimwenguni, unaunga mkono uimarishaji wa huduma-za-afya kwawote ili kuboresha mapato-ya-afya. Pia kuna makubaliano yanayokua kwamba kutumia ubunifu/teknolojia-za-kisasa za-kidijitali kutawezesha watu-wengi zaidi kunufaika kutokana na huduma-ya-afya kwa-wote.

Afya-ya-kidijitali ni neno-mwamvuli linalojumuisha teknolojia-ya-mawasiliano, teknolojia-ya-habari-ya-afya, data-kubwa, akili-bandia, na teknolojia inayoweza kuvaliwa na mgonjwa/mstahiki. Teknolojia-ya-mawasiliano ina uwezo mkubwa wa kusaidia kutoa huduma-bora za-afya na nafuu .Hatahivyo, kuna changamoto ,Teknolojia-mpya inaweza kuwa ghali na kwahiyo ni lazima iendane-vyema na mahitaji-ya-jamii ambapo itatumika, na ya-ubora wa-kutosha ili kuhalalisha mahitaji-ya-kifedha yaliyotolewa. Changamoto nyingine ni ukosefu-wa-usawa uliokuwepo awali katika upatikanaji-wa-elimu, miundombinu na teknolojia katika jamii.

Utumiaji-sahihi, usawa, maadili-ya-teknolojia na uwajibikaji ni lazima ikiwa tutaepuka kukuza ukosefu-wa-usawa wa-kiafya uliopo. Mambo kama vile muunganisho-duni wa intaneti, uwezo-mdogo wa kusoma/kuandika kidigitali, ukosefu wa ufikiaj-wa-mtandao na simu-janja - zinazojulikana kama kiashiria cha-afya cha-dijitali-zinapaswa kuwa muhimu katika fikra zetu tunapojumuisha teknolojia-ya-mawasiliano katika huduma zilizopo.

WHO inafafanua ushirikishwaji wa-jamii kama "mchakato-wa kukuza uhusiano unaowezesha wadau mfano vituo-vya-afya na jamii ,taasisi zisizo-za-serikali/watu-binafsi kufanya kazi pamoja kushughulikia masuala yanayohusiana na afya na kukuza ustawi ili kufikia athari na matokeo chanya ya-kiafya."

Hakuwezi kuwa na mbinu isiyo rasmi ya ushirikishwaji wa-jamii katika upangaji wa huduma-za-afya, kwani kuna tofauti za-kijamii/kitamaduni katika maeneo mbalimbali. Hatahivyo kuna baadhi ya-kanuni za-kawaida zinazotumika katika mazingira-yote, kama usawa, mawasiliano ya-wazi na uwajibikaji.

Kwamfano ikiwa jamii itaombwa kuchangia kiasi-kidogo kusudi kupata chanjo juu-ya Homa-ya-ini ,na endapo kutakuwa na uwezekano wa-jamii kupewa elimu juu-ya namna homa-ya-ini inavyoambukiza ,hivyo jamii nzima yapasa kupata chanjo hiyo kwa kulipia, itakuwa sawa tu kusaidia kuamua ni wakati gani jamii itajikusanya na watu-wa-afya watawachanja watu-wa-jamii hiyo husika, (kwamfano baada ya saa za kawaida za kazi, ili wafanyakazi waweze kuhudhuria miadi) na kiasi gani cha ada itakayolipwa na je itakuwa endelevu au nafuu kwao.

Ikiwa hii itawasilishwa kwa-uwazi tangu mwanzo, na wataalamu-wa-afya watatoa taarifa za-kila-mara na uwepo wa-jukwaa ambapo wanajamii wanaweza kuuliza maswali, mradi kama huo utakuwa na uwezekano-mkubwa wa-kufaulu. Faida nyingine ya kushirikisha jamii wakati-wa kupanga huduma-za-afya ni kuboreshwa kwa-matumizi ya huduma hizo. Hii ni kwasababu ushirikishwaji-wa-jamii unaweza kuwezesha mabadiliko-ya-tabia na mienendo ndani-ya-jumuiya, na kusababisha upokeaji, kukubalika, na matumizi-bora ya huduma-za-afya.

KWA-USHIRIKIANO WANAJAMII WANAPASWA

-Kuimarisha shughuli-za-jamii kwa kuwawezesha wanajamii kujiamulia ni nini kinachowafaa na kwa manufaa ya umiliki-wa-jamii na udhibiti-wa-huduma .

-kuunda mazingira ya kusaidia kwa kudumisha-maliasili na kuhimiza usawa-wa-burudani ya kazini ili kuboresha afya.

-kukuza ujuzi binafsi wa watu katika jamii ili waweze kujiandaa kukabiliana na tatizo-la-kiafya

-kuunda sera-ya-afya ya-umma, ambayo ni pamoja na sheria, ushuru, mabadiliko ya mfumo wa afya.

-Kutoa uelewa mpana kuhusiana na magonjwa yanayoambukiza/yasiyoambukiza.

Ripoti-ya-mradi-wa-kimataifa-wa-Malengo-ya-Maendeleo-ya-Umoja-wa-Mataifa, mamilioni ya-watu bado wanaachwa nyuma, hasa-wale wanaoishi katika-umaskini na wale-wasio na uwezo kwasababu ya jinsia-zao, umri, ulemavu, au kabila.

Robotatu ya makundi-haya wanaishi katika masafa-ya-mwisho ambayo ni maeneo-ya-mbali au magumu kufikiwa ambayo hayana utoaji wa kutosha wa elimu, huduma-za-afya, maji na usafi-wa-mazingira.

Neno masafa-ya-mbali lilitumiwa na wafanyabiashara kufafanua ni wateja-gani waliolengwa walikuwa wa-mwisho kupokea bidhaa na huduma-mahususi. Hivimajuzi, mashirika-ya-maendeleo yamepitisha neno hili kurejelea idadi-ya-watu ambao ni vigumu-zaidi kufikiwa.

Katika maeneo-ya-vijijini, ufikiaji wa masafa-ya-mwisho una sifa ya njia-za-miguu, barabara mbovu, na madaraja-yaliyovunjika/kutokuwepo.Katika baadhi ya misimu huenda zisiweze kufikiwa hata-kidogo.Kwawale wanaoishi karibu na mito, ufikiaji wa-visiwanii unafanywa kuwa mgumu zaidi kwasababu ya mafuriko, utegemezi wa mitumbwi/ngalawa na huduma-duni.

katika maeneo-ya-mijini au pembezoni mwa miji masafa-ya-mwisho inajumuisha maeneo kama vile vitongoji-duni vya-mijini/vitongoji ambavyo havijaunganishwa na huduma-za kimsingi kama vile maji, usafi-wa-mazingira, umeme, mtandao, ufikiaji-wa-simu-za-rununu, na mtandao-wa-usafirishaji. Mwaka 2018, bilioni moja ya idadi-ya-watu wa mijini duniani, walikadiriwa kuwa wanaishi katika vitongoji-duni vya-mijini.

Watu wanaoishi katika masafa-ya-mwisho ni wale ambao hawafikiwi na huduma-za-afya, ambao hawawezi kuchukua hatua zinazohitajika ili kufikia huduma-za-msingi za-afya wanazohitaji. inaweza kujumuisha:-

-Makundi-ya-watu wasio na-uwezo, kama vile watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri, wanawake, wahamiaji, wakimbizi, na watu waliokimbia makazi yao (kutokana na migogoro, mabadiliko ya hali-ya-hewa, na au majanga-ya-asili.

Makundi-madogo kutokana na makabila, dini , au mwelekeo-wa-kijinsia na jumuia-za-kiasili.

-Watu-walio na changamoto-za-kiafya/za-kimwili kamavile wazee-walio na hali-sugu-za-kiafya ,watu-wenye-ulemavu,kamavile wenye usonji,mtindio-wa-ubongo,na tatizo-la-afya-ya-akili ikimaanisha unyongovu/wasiwasi ,kadhalika.

KWANINI KUNA MASAFA-YA-MWISHO?

 Mifumo-ya-kitamaduni au imani, maadili na vipaumbele, na vikwazo-vya-mawasiliano.Hii inaweza kuwanyanyapaa baadhi-ya-makundi au kuwafanya wategemee wengine kwa ruhusa na/au rasilimali wanazohitaji kutafuta huduma-za-afya kwamfano wanawake/watoto katika jamii zinazotawaliwa na wanaume.

 Maadili na vipaumbele, maadili-ya-kisiasa maranyingi huakisi yale-y- jamii na hii inaweza kubainisha jinsi na wapi rasilimali zitagawiwa. Mfano, watoa-huduma-za-afya na serikali wanaweza kupendelea matumizi ya huduma-za-elimu ya-juu (ambayo inanufaisha wakazi-wa-mijini, huku wakipuuza jamii na huduma-ya-afya ya msingi.

 Vizuizi-vya-mawasiliano hivi ni pamoja na vikwazo-vya-kimaumbile kama vile ukosefu wa ufikiaji-wa-simu-za-rununu au ufikiaji-wa-mtandao. Aidha, kukosekana kwa mikakati iliyotafsiriwa, yakienyeji, na nyeti ya kitamaduni na taarifa-za-afya

inamaanisha kuwa jamii hazifahamu umuhimu wa baadhi ya huduma-za-afya, kama vile. uchunguzi wa mtoto-wa-jicho/presha-ya-macho ni kwaajili ya kuzuia upofu.

KWANINI KUWAFIKIA WATU KATIKA MASAFA-YA-MBALI NI VIGUMU?

 Kukosekana kwa data sahihi

 Muunganisho wa masiliano ni duni na kukosekana kabisa shughuli-za-uwekaji kidijitali na kushiriki-data ambazo huboresha utoaji-huduma unaweza usiwezekane.

 Watu wa masafa-ya-mbali hupata kila maendeleo mwisho,uharibifu-wa-mazingira na umaskini uliokithiri unaweza kupelekea waendelee kutokupata huduma hizo.

 Gharama za kutatua vikwazo hivyo zinaweza kuwa kubwa kupelekea watoa-huduma na wapatiwa-huduma kushindwa kukidhi kwasababu-ya-umbali na sababu gharama hizo zinakuwa hazikuwekwa kwenye bajeti au mpangilio.

ATHARI ZINAZOWAKUMBA WATU HAWA WALIOACHWA

 tayari ni wanachama wa kundi-la-watu wasio na uwezo zaidi katika jamii .

 Hawapati huduma stahiki hivyo kuteseka/kubaki katika maumivu

 Pengo hili la usawa litaendelea kukua isipokuwa masafa-ya-mwisho yatashughulikiwa Kiumakini kwani kadiri idadi-ya-watu-inavyoongezeka-idadi-ya-watu katika masafa-ya-mwisho pia itaongezeka, na kufanya kuwa vigumu zaidi kuwafikia kwa njia rahisi.

NINI KIFANYIKE?

Watendaji na wote wenye dhamana lazima waangazie masaibu-ya-watu katika masafa-ya-mwisho na kutetea uwekezaji wa muda-mrefu wa-serikali katika utoaji wa huduma-za-msingi katika maeneo-ya-mbali .Ikijumuisha vijiji-vya-ndani katika mipango-ya-afya-ya kitaifa ni hatua muhimu katika kuhakikisha kupangilia kuanzia ngazi-za-juu za-serikali, ikiwa ni pamoja na kutoa usaidizi-wa-kibajeti.

Kufikia maili-ya -wisho pia ni sehemu ya shabaha ya Umoja-wa-Mataifa wa huduma-ya-afya kwa wote, ambayo ni pamoja na kupunguza umbali-wa-kijiografia kati ya watu na huduma, na kutoa huduma-muhimu zenye ubora-wa-juu kwa gharam-nafuu, ili wapokeaji huduma wasisukumwe kwenye umaskini au ugumu-wa-kifedha .Serikali ulimwenguni kote zilipitisha lengo hili mwaka wa 2015 na kusisitiza ahadi yao katika 2019, na kwa hivyo zinaweza kuwajibika.
 
Back
Top Bottom