kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
UKIZUNGUMZIA nyota waliowahi kutesa katika medani ya soka ya Tanzania kwenye miaka ya sabini hadi mwanzoni mwa themanini basi huwezi kuacha kulitaja jina la Jellah Mtagwa nyota wa zamani klabu za Yanga, Pan African na Taifa Stars.
Nahodha huyo wa kikosi cha Stars kilichoshiriki kwa mara ya kwanza fainali za Mataifa ya Afrika nchini Nigeria mwaka 1980 bado hali yake ni mbaya tangu alipopata ugonjwa wa kiharusi miaka minne iliyopita.
Ukimwona alivyo Mtagwa kwa sasa na maisha anayoishi kwa hakika hauwezi kusema kuwa huyu ndiye ambaye picha zake zilitumika kwenye Stempu pamoja na kuteingenezea nchi heshima ambayo hadi sasa imeshindwa kufikia kwa zaidi ya miaka 30 sasa.
Kutokana na ugonjwa huo wa kiharusi, Mtagwa hana tena uwezo wa kufanya kazi ya aina yoyote ya kumwezesha kupata kipato cha kukidhi mahitaji yake ya kila siku jambo linalomfanya kuwa kama omba omba kwa kutegemea msaada.
Hivi karibuni mara baada ya mwandishi wa gazeti hili kupata taarifa kuwa mchezaji huyo mkongwe bado hali yake si nzuri alifika nyumbani kwake Magomeni Kagera na kumkuta akiwa katika hali ambayo kwa hakika inasikitisha na kutia huruma.
Kwa taratibu na unyonge huku akitembea kwa kuvuta mguu wake wa kushoto Mtagwa alitoka chumbani kwake uso wake ulionekana wenye simanzi kubwa na ambao unahitaji msaada wowote ule ili aweze kukabiliana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na maisha yake ya kila siku.
''Kama unavyoniona sina kitu chochote wala sehemu yoyote ambayo naitegemea ili kukabiliana na hali niliyonayo zaidi ya kutegemea msaada kutoka kwa baadhi ya marafiki wa karibu ambao wamekuwa na mimi tangu nilipokumbwa na tatizo hili mwaka 2006.
''Rafiki zangu hao wamekuwa wakinisaidia sana kila ninapohitaji msaada wao hivyo siwezi kusema vibaya, lakini kwa hakika bado nahitaji msaada zaidi ili niweze kurudi katika hali yangu ya kaiwada,'' alisema Mtagwa kwa sauti ya unyonge ambayo ilisabisha mmoja wa watoto wake kudondosha machozi.
Mtagwa aliendelea kusema kuwa zaidi ya kupata msaada kutoka kwa rafiki zake hao hajawahi kupata msaada wowote kutoka kwa klabu zote alizozitumikia hata Shirikisho la Soka Tanzania TFF.
''Sio TFF wala Yanga au Pan African ambazo zimewahi kunisaidia, lakini kubwa zaidi namshukuru Mungu kwa kile kidogo anachowajalia baadhi ya rafiki zangu nao hunikumbuka kwa kunilipia matibabu na wakati mwiningine fedha za kunisaidia chakula hapa nyumbani.
''Vilevile hata leo hii mambo si mazuri kiuchumi mpaka sasa bado sijatia kitu chochote kinywani kwangu, lakini nashukuru Mungu kwa kila jambo linalotokea mbele yangu na ninaamini ipo siku nitarejea katika hali yangu ya kawaida,'' alisema Mtagwa.
Katika hatua nyingine uongozi wa Chama cha Wachezaji soka Tanzania (Sputanza) baada ya kuulizwa na Mwananchi kama kuna utaratibu wowote wa kumsaidia Mtagwa ambaye ni wanachama wake ulisema kuwa umeandaa utaratibu kwa kuwaandika barua wadau pamoja na wapenzi mbalimbali wa soka nchini wenye mapenzi mema ili waweze kumsadia mchezji huyo.
''Chama chetu ni kichanga na hakina fedha za kutosha kumsaidia mchezo huyo isipokuwa tuliandaa utaratibu wa kuandika barua na kuzisambaza sehemu mbalimbali kwa lengo la kuwaomba wadau na wapenzi wa soka nchini kumsaidia Mtagwa pamoja na mwanachama mwezetu na mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa Stars, Allan Shomary ambaye kwa sasa amepata upofu,'' alisema Katibu msaidizi wa Sputanza, Abeid Kasabalala.
Nakala ya barua iliyoandikwa na Sputanza na kusambazwa kwa wadau mbalimbali wa soka nchini kwa lengo la kusaidia Mtagwa na Shomary ilisomeka.
SOCCER PLAYERS UNION OF TANZANIA.
Taarifa kwa Wadau wote wa soka Tanzania
Bwana Jellah A Mtagwa ni mchezaji wa zamani wa Pan Afrika, Yanga na aliyekuwa Nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars'' ambaye kwa sasa amepatwa na matatizo ya kiharusi (Stroke) hivyo kumfanya awe mlemavu wa mkono na mguu.
Kwa kuthamini mchango wake wa soka katika Tanzania na kwa kutambua nafasi yako katika duru la mchezo huo, Sputanza inakuomba tumchangie mwenzetu huyu kwa hali na mali ili familia yake ipate kujikwamua na hali ngumu inayomkabili kwa kumchangia kiasi chochote ulichonacho kupitia namba yake ya M Pesa 0755 693330.
Kwa maelezo zaidi au makabidhiano ya hundi kwa mlengwa wasiliana na Katibu wa Sputanza kwa namba 0754 270815 na 0713 455255.