Afrika ni Bara lililobarikiwa utajiri wa raslimali za kila aina, likalaaniwa viongozi wake

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,900
3,206
Afrika ni bara tajiri sana duniani.

Lina rasilimali za kila aina kuanzia ardhi nzuri inayofaa kulima mazao ya kila aina, maji, hali nzuri ya hewa, uoto wa asili ikiwemo misitu, madini, mafuta, gesi n.k.

Viwanda vingi duniani vinaendeshwa na raw-materials toka Afrika.

Cha kustaajabisha, nchi nyingi za bara hili, hasa zile za kusini mwa jangwa la Sahara, wananchi wake wanaishi katika umaskini uliokithiri!

Hali hii ya umaskini kwa wananchi wa nchi hizi za Afrika, kwa sehemu kubwa zimechagizwa na viongozi.

Viongozi wengi wa bara hili wakishachaguliwa, kwanza huanza kujinufaisha wao na watu wao wa karibu na kuwasahau wananchi waliowaweka pale.

Wengi wa viongozi wetu, ni matajiri wa kutupwa duniani pamoja na kwamba wengi wao, huficha fedha katika nchi zilizoendelea kama vile Ulaya, Amerika Kaskazini, na kwa sasa Asia (Dubai, Singapore n.k).

Kama kweli viongozi wote wa Bara hili wangekuwa wazalendo kwa nchi zao, basi ingetuchukua tu miaka 20 kuzibadilisha nchi zetu hizi toka hapa tulipo hadi kufikia angalau uchumi wa kati.

Lakini jambo la kushukuru ni kwamba nchi nyingi za Kiafrika, vijana wameanza kuamka na kuwakataa viongozi mafisadi.

Hili vuguvugu limeanzia huko Guinea, Mali, Burkina Faso, Niger na tusishangae kuliona likisambaa sehemu mbalimbali za Bara hili zenye viongozi washenzi ambao wako kimaslahi yao badala ya kuwatumikia wananchi wao.

Mungu libariki bara letu pendwa la Afrika.

Tusaidie pia kwa kutuondolea viongozi wa hovyo wasiowapenda watu wao na nchi zao;

Amiin.
 
... LAANA YA AFRICA NI KUCHELEWA KISAYANSI NA KITEKNOLOJIA KUNAKOTUFANYA TUWE TEGEMEZI MUDA WOTE!
TIBA NI KUPITA NJIA YA CHINA, ... TUNAWEZA?
Lakini wanasema Sayansi na Teknolojia ilianzia hapa hapa Afrika Mkuu.
Wazungu walikuja kuichukua hapa kwetu, wakaiendeleza huko kwao.
Sasa, kama wao waliweza, kwa nini sisi tushindwe kama tungekuwa na viongozi makini?!
 
Lina raslimali za kila aina kuanzia ardhi nzuri inayofaa
Swali kuu kutoka nchini Ghana kuhusu utaratibu wa kununua dhahabu na nani anamilki migodi je serikali itajikita kununua toka kwa wachimbaji wadogo kwa bei ya kimataifa?

JIBU LA KUWEZESHA NCHI KUWA NA AKIBA YA DHAHABU, MADINI NA VITO LAPATIKANA

1 July 2023
Gaborone, Botswana

1691505077572.png

Nchi ya Botswana imepata jibu kuwa mfano Tanzania mkataba wa mgodi na mwekezaji wagawane vitofali vya dhahabu na serikali badala ya kusubiri faida ya kwenye balance sheet.

Mgawanyo wa vitofali au almasi au tanzanite inaipa uhuru Tanzania kuhifadhi kitu halisi na kukiuza kwa thamani ya uhakika bila makando kando ya kusubiri mwekezaji asafirishe madini yote nje na mwisho wa siku akuambie faida ni ndogo kama ripoti yake ya katika mahesabu ya mwaka yanavyoonesha .

1 July 2023
Gaborone, Botswana,

Botswana na De Beers Zasaini Mkataba wa Kuendeleza Ushirikiano Tajiri wa Almasi

Chini ya makubaliano mapya ya uchimbaji madini, Botswana itapata mara moja asilimia 30 ya mawe machafu yaliyochimbwa, kutoka asilimia 25, na itapanda hadi asilimia 50 ndani ya muongo mmoja, De Beers na maafisa wa serikali walisema.

Afisa wa serikali ya Botswana na mtendaji mkuu wa De Beers, muungano wa kimataifa wa almasi, walitia saini mikataba ya muda siku ya Jumamosi ili kuendeleza ubia wenye faida, wa miongo kadhaa wa uchimbaji madini ya almasi ambao ulionekana kuvunjika katika miezi ya hivi karibuni.

Dakika chache kabla ya tarehe ya mwisho ya usiku wa manane siku ya Ijumaa, pande zote zilitangaza kwamba baada ya mazungumzo ya miaka mingi, walikuwa wamekubaliana kimsingi juu ya mpango wa kuunda upya ushirikiano ambao unaipatia De Beers sehemu kubwa ya almasi yake na serikali ya Botswana sehemu kubwa zaidi ya mapato yake.

Maelezo ya mpango huo bado yanashughulikiwa, maafisa wa serikali na De Beers walisema. Lakini inashughulikia moja ya matatizo makubwa ya serikali ya Botswana, kuhusu mgao wa almasi ambayo inapokea katika ubia wake wa uchimbaji madini na De Beers.

Chini ya makubaliano ya zamani, Botswana ilipokea asilimia 25 ya mawe machafu yaliyochimbwa, huku De Beers ilichukua mengine. Sasa, Botswana itapata mgao wa asilimia 30 mara moja, na hiyo itapanda hadi asilimia 50 ndani ya muongo mmoja, De Beers na maafisa wa serikali walisema.

De Beers alisema katika taarifa yake kwamba imekubali kuwekeza kiasi cha dola milioni 825 katika kipindi cha miaka 10 ijayo kusaidia kuendeleza uchumi wa Botswana. Makubaliano hayo pia yanajumuisha kuanzisha chuo nchini Botswana ambacho kitafundisha wenyeji ujuzi katika biashara ya almasi, maafisa wa serikali walisema

Source : The New York Times
 
Siku tukipata viongozi wazalendo wa kweli mbona miaka 5 ni mingi sn
Nakubaliana na wewe Mkuu.
Tanzania kwa mfano, Benki ya dunia ilitutangaza kuwa uchumi wa kati wa chini ndani ya kipindi cha miaka mitano tu Hayati JPM, tena katikakati ya janga la CORONA ambalo liliathiri dunia nzima!
Hii ilikuwa miaka mitano nyuma ya target ya serikali (ambayo ilipanga mnamo mwaka 2000 kwamba ifikapo 2025 tufike uchumi wa kati). Cha kusikitisha ni kwamba miezi michache tu baada ya kufariki, tukatangaziwa kwamba tayari tumesharudi uchumi wa chini kabisa!
So sad!
 
1 July 2023

Under the new deal announced on Friday, Botswana gets a bigger share of rough stones from their joint venture, Debswana.

Botswana and mining company De Beers have announced a new diamond sales deal.
1691505199728.png

The new deal, concluded on Friday, gives Botswana a bigger share of rough stones from their joint venture.

Debswana, a joint venture between Anglo American unit De Beers and Botswana's government, sells 75% of its output to De Beers, with the balance taken up by state-owned Okavango Diamond Co.

The new agreement covers a 10-year sales deal for Debswana rough diamond production through to 2033 and 25-year Debswana mining licences.

In the run-up to Friday's deal, Botswana President Mokgweetsi Masisi, who is expected to seek re-election next year, had pushed De Beers for a bigger share of Debswana's output.

In March, Botswana announced it would take a 24% stake in Belgian gem processing firm HB Antwerp in a move seen as designed to loosen De Beers' grip on the country's gems.

Botswana supplies 70% of De Beers' rough diamonds
 
Nyimwa Mali upewe akili Africa tumenyimwa maarifa
Kweli kabisa Mkuu.
Mzazi wangu alizoea kunishauri kwamba kuliko kukosa akili, bora ukose nguo maana unaweza kupata msamaria wa kukusaidia.
Lakini kama huna akili, utateseka sana.
 
Ule msemo wa Wahenga wa bora ukose mali, upate akili una funzo kubwa sana. Afrika imebarikiwa watu wenye akili butu mpaka basi. Sijui ni lini tutakuja kuondoka kwenye huu udumavu wa akili.

Imagine wakitokea wabunifu, serikali iko radhi kuwakamata na kuwafunga! Wazawa wanatengeneza bidhaa za kila aina, lakini utashangaa serikali inaagiza bidhaa hizo hizo kutoka nje ya nchi na kwa bei kubwa!!

Viongozi wanabinafsisha na kuuza raslimali za nchi kwa wageni, ili tu wapate 10%, au kupata manufaa binafsi!! Viongozi wengi wanapenda kujigeuza na kuwa miungu watu, mara tu waingiapo madarakani!!

Dah! Wenzetu wenye ngozi nyeupe wanajitambua sana kwa kweli.
 
Lakini wanasema Sayansi na Teknolojia ilianzia hapa hapa Afrika Mkuu.
Wazungu walikuja kuichukua hapa kwetu, wakaiendeleza huko kwao.
Sasa, kama wao waliweza, kwa nini sisi tushindwe kama tungekuwa na viongozi makini?!
Sio kwamba wazungu walichukua teknolojia ya Afrika, ila ni kwamba ile tecnolojia ya kufua vyuma tuliyogawiwa na babu yetu, aliyeishi Afrika, wenzetu wameipeleka mbali sana, kutokana na mazingira magumu waliyokutana nayo! ... sisi bado tunafua mikuki na majembe ya chuma laini kinachopindapinda, wakati wenzetu wamerudi na makorokoro yote tunayoona hatuwezi kuishi bila kuyamiliki (zana mbalimbali,silaha, usafiri, mawasiliano, tiba ......!)
TUNA KAZI NZITO! ..... NA, TUSIPOTUMIA AKILI, TUTAMALIZANA!
 
Niger ina Cobult, Uranium, diamond na Platinum.

Ndo nchi yenye kusafirisha nje kwa kiasi kikubwa madini ya Uranium kwenda bara la Ulaya ikiwa mbele ya nchi za Khazakstan na Russia.

Kwa mujibu wa taarifa za maliasili katika nchi mbalimbali duniani, nchini Niger tangu mwaka 1968 ipo kampuni ya Orano (zamani ikiitwa Areva) ambayo ni ya Ufaransa na yamiliki asilimia 45 ya mgodi wa Uranium nchini Niger uliopo jangwani sehemu iitwayo Arlit.

Kampuni ya Orano ni kubwa kama ilivyo kampuni ya Ashanti na Barrick na ni "multimillion company" inouza madini hayo yanotengeneza umeme kwa nchi za Ulaya, hususan Ufaransa na Ujerumani.

Kama ilivyo kwa Tanzania madini hayo huchimbwa kwa wingi lakini malipo yanotokana na mauzo yake huko nje ni madogo sana (twaibiwa) malimilioni ya pesa. Niger hupata fedha za msaada ambazo huja kwa mithili ya mikopo.

Niger ina tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira na wananchi wake hupata shida ya maji safi ya kunywa kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji. Pia uchafu unotokana na uchimbaji wa uranium |(radioactive waste) huleta tishio la magonjwa kwa binadamu na hali hiyo imeiacha nchi ya Niger chini kabisa kwenye orodha za nchi zenye watu wenye afya bora.

Asilimia 10 ya wananchi wa Niger ambao ni milioni 24 waishi kwenye lindi la umaskini wa kutupwa na serikali ya Niger huishi kwa bajeti inotokana na malipo ya mirahaba ya kampuni kama ya Orano.

Kwa mfano huu utaona ni aina gani ya serikali ambayo yafaa kuongoza bara la Afrika lakini tatizo kubwa ni fikra sahihi za kuongoza na pia kuwa na watu sahihi.

Niger ilitakiwa kuwa moja ya nchi tajiri wa kutupwa barani Afrika na yenye bajeti ya kutosha kabisa (kutoka mgodi mmoja wa Uranium kuboresha maisha ya watu wake milioni 24.
 
Afrika ni bara tajiri sana duniani.

Lina raslimali za kila aina kuanzia ardhi nzuri inayofaa kulima mazao ya kila aina, maji, hali nzuri ya hewa, uoto wa asili ikiwemo misitu, madini, mafuta, gesi n.k.

Viwanda vingi duniani vinaendeshwa na raw-materials toka Afrika.

Cha kustaajabisha, nchi nyingi za bara hili, hasa zile za kusini mwa jangwa la Sahara, wananchi wake wanaishi katika umaskini uliokithiri!

Hali hii ya umaskini kwa wananchi wa nchi hizi za Afrika, kwa sehemu kubwa zimechagizwa na viongozi.

Viongozi wengi wa bara hili wakishachaguliwa, kwanza huanza kujinufaisha wao na watu wao wa karibu na kuwasahau wananchi waliowaweka pale.

Wengi wa viongozi wetu, ni matajiri wa kutupwa duniani pamoja na kwamba wengi wao, huficha fedha katika nchi zilizoendelea kama vile Ulaya, Amerika Kaskazini, na kwa sasa Asia (Dubai, Singapore n.k).

Kama kweli viongozi wote wa Bara hili wangekuwa wazalendo kwa nchi zao, basi ingetuchukua tu miaka 20 kuzibadilisha nchi zetu hizi toka hapa tulipo hadi kufikia angalau uchumi wa kati.

Lakini jambo la kushukuru ni kwamba nchi nyingi za Kiafrika, vijana wameanza kuamka na kuwakataa viongozi mafisadi.

Hili vuguvugu limeanzia huko Guinea, Mali, Burkina Faso, Niger na tusishangae kuliona likisambaa sehemu mbalimbali za Bara hili zenye viongozi washenzi ambao wako kimaslahi yao badala ya kuwatumikia wananchi wao.

Mungu libariki bara letu pendwa la Afrika.

Tusaidie pia kwa kutuondolea viongozi wa hovyo wasiowapenda watu wao na nchi zao;

Amiin.
Viongozi na wananchi pia.Wananchi ngangari hawawezi fanyiwa upumbavu na Viongozi.
 
Viongozi na wananchi pia.Wananchi ngangari hawawezi fanyiwa upumbavu na Viongozi.
Ila hili nalo neno!

Japo raia wengi wa Afrika wanawaheshimu sana viongozi Madam.

Sema viongozi wengi wamekuwa wanawa-dissapoint sana.

Kumbuka "like leader like followers".
 
Ule msemo wa Wahenga wa bora ukose mali, upate akili una funzo kubwa sana. Afrika imebarikiwa watu wenye akili butu mpaka basi. Sijui ni lini tutakuja kuondoka kwenye huu udumavu wa akili.

Imagine wakitokea wabunifu, serikali iko radhi kuwakamata na kuwafunga! Wazawa wanatengeneza bidhaa za kila aina, lakini utashangaa serikali inaagiza bidhaa hizo hizo kutoka nje ya nchi na kwa bei kubwa!!

Viongozi wanabinafsisha na kuuza raslimali za nchi kwa wageni, ili tu wapate 10%, au kupata manufaa binafsi!! Viongozi wengi wanapenda kujigeuza na kuwa miungu watu, mara tu waingiapo madarakani!!

Dah! Wenzetu wenye ngozi nyeupe wanajitambua sana kwa kweli.
Mkuu siyo kwamba sisi weusi hatuna akili.
Akili tunazo nyingi sana hadi tunazi-abuse.
Akili zetu tunazitumia kurudishana nyuma.
Akili zetu tunazitumia kuwekeana mitego na vikwazo visivyo na maana.
Utashangaa viongozi badala ya kutumia akili kidogo tu kuwaletea wananchi wao maendeleo, wao wanatumia akili kubwa kudanganya na kuhakikisha uchaguzi ujao wanachaguliwa tena kwa vyovyote!!
 
Afrika ni bara tajiri sana duniani.

Lina raslimali za kila aina kuanzia ardhi nzuri inayofaa kulima mazao ya kila aina, maji, hali nzuri ya hewa, uoto wa asili ikiwemo misitu, madini, mafuta, gesi n.k.

Viwanda vingi duniani vinaendeshwa na raw-materials toka Afrika.

Cha kustaajabisha, nchi nyingi za bara hili, hasa zile za kusini mwa jangwa la Sahara, wananchi wake wanaishi katika umaskini uliokithiri!

Hali hii ya umaskini kwa wananchi wa nchi hizi za Afrika, kwa sehemu kubwa zimechagizwa na viongozi.

Viongozi wengi wa bara hili wakishachaguliwa, kwanza huanza kujinufaisha wao na watu wao wa karibu na kuwasahau wananchi waliowaweka pale.

Wengi wa viongozi wetu, ni matajiri wa kutupwa duniani pamoja na kwamba wengi wao, huficha fedha katika nchi zilizoendelea kama vile Ulaya, Amerika Kaskazini, na kwa sasa Asia (Dubai, Singapore n.k).

Kama kweli viongozi wote wa Bara hili wangekuwa wazalendo kwa nchi zao, basi ingetuchukua tu miaka 20 kuzibadilisha nchi zetu hizi toka hapa tulipo hadi kufikia angalau uchumi wa kati.

Lakini jambo la kushukuru ni kwamba nchi nyingi za Kiafrika, vijana wameanza kuamka na kuwakataa viongozi mafisadi.

Hili vuguvugu limeanzia huko Guinea, Mali, Burkina Faso, Niger na tusishangae kuliona likisambaa sehemu mbalimbali za Bara hili zenye viongozi washenzi ambao wako kimaslahi yao badala ya kuwatumikia wananchi wao.

Mungu libariki bara letu pendwa la Afrika.

Tusaidie pia kwa kutuondolea viongozi wa hovyo wasiowapenda watu wao na nchi zao;

Amiin.
Viongozi wengi waliotawala baada ya mkoloni walikuwa wabinafsi,pia walikuwa hawana mipango endelevu mfano Tz hata urban planning imetushinda miji yetu imejengwa hovyo sana
 
Back
Top Bottom