Afrika kujaribu tena kumshawishi Gbagbo

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,139
12,285
Viongozi watatu wa mataifa ya Afrika Magharibi, watarejea tena nchini Ivory Coast siku ya Jumatatu kwa ajili ya majadiliano zaidi ya kumaliza mzozo wa kisiasa uliodumu kwa miezi kadhaa.
101229123901_ivorycoastprotestors386.jpg
Waandamanaji wanaomuunga mkono Alassane Ouattara

Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya viongozi hao kushindwa kumshawishi Bw Laurent Gbagbo kuachia madaraka.

Mwenyekiti wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi, Ecowas, ambaye pia ni rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema mazungumzo bado yanaendelea.
Mshindi halali

Ecowas ina matumaini kuwa Bw Gbagbo atakubali kuachia ngazi na kumpisha Alassane Ouattara, ambaye anaaminika kuwa ndio mshindi halali wa uchaguzi.

Jumuiya hiyo imetishia kutumia nguvu iwapo atagoma kuondoka madarakani. 100915184542_goodluck_jonathan_386x217_afp.jpg

Mwenyekiti wa Ecowas, Goodluck Jonathan


Kituo cha televisheni cha serikali kimetangaza kuwa mamilioni kadhaa ya wafanyakazi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanaofanya shughuli zao nchini Ivory Coast, watakuwa hatarini iwapo nguvu za kijeshi zitatumika.

"Watarejea tena Januari 3, na watakaporudi, matokeo yake ndio yataamua hatua itakayochukuliwa," amesema Rais Jonathan.

"Panapotokea mzozo, panapokuwa na kutokuelewana, ni mazungumzo ndio yatatatua". amesema rais huyo wa Nigeria.
 
Mimi katika swala la laurent gbagbo sijielewi nichangiaje? Unajua ni ngumu kuchangia wakati hauishi ivory cost ili uwezekujua situation ilikuaje? Mfano hapa kwetu unajua kabisa kuwa sisisim walichakachua. Inawezekana pia qatara kachakachua au yeye mwenyewe gbagbo ndio kachakachua hatujui mimi na wewe kwa hiyo tusichangie kwa hisia tu!!!!!!!!!!!!!
 
Utandawazi kaka...nyumba ya jirani ikifuka moshi huwezi kua na amani hata kidogo...hata kidogo! km ni mfuatiliaji mzuri wa taarifa ya habari kupitia CNN,BBC na ALJAZEERA utakua umezunguka dunia.
 
Back
Top Bottom