Afisa Usalama Feki ahukumiwa jela miezi 3

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
1685053759191.png

Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara imemuhukumu Patrick Wambura (34) Mkazi wa Bariadi Mkoani Simiyu kutumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani kwa kosa la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati Victor Kimario ambapo amesema Mshtakiwa huyo alijitambulisha kwa Ofisa wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Babati January 18 mwaka jana kuwa yeye ni Afisa Usalama wa Taifa.

Amesema Mshtakiwa huyo alijiita Afisa usalama wa Taifa akidai anafatilia nyaraka za kesi ya Mlale Sogweda ambaye alikuwa na shauri katika Baraza hilo.

Hakimu Kimario amesema upande wa mashtaka uliwasilisha Mashahidi wanne na vielelezo vitano, huku hoja iliyoifanya Mahakama kukubaliana na ushahidi huo ni kuwa Mashahidi waliiambia Mahakama kuwa Mshtakiwa alikuwa anaonekana Mahakamani mara kwa mara akijifanya kuwatetea Watu wakati akijua yeye siyo Wakili.

"Kitendo alichokifanya Wambura siyo kizuri cha kujipendekeza na kujifanya Mtu mashuhuri katika jamii hivyo nakutia hatiani uende gerezani ukatumikie miezi mitatu”
 
Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara imemuhukumu Patrick Wambura (34) Mkazi wa Bariadi Mkoani Simiyu kutumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani kwa kosa la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.
Babati tena!!!
 
Back
Top Bottom