Magnesium
JF-Expert Member
- Nov 9, 2014
- 317
- 185
Kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm msanii na mtia nia wa kugombea ubunge wa Morogogoro kupitia ACT, Suleiman Msindi maarufu kama Afande Sele, amesema kuwa kilichomfanya atoke CHADEMA kutimkia ACT ni kutokuwepo kwa demokrasia katika chama hicho cha 'Zamani' katika kile alichosema ni viongozi kung'ang'ania madaraka.
Ameongeza kuwa ilifika wakati alitakiwa kutoa kiasi cha pesa kipatacho milioni 30 ili kuwashawishi wajumbe kuteuliwa kuwa mgombea ubunge ilhali yeye hayuko tayari. Ameongeza kuwa aliambiwa kama hawezi kufanya hivyo agombee udiwani kwani watia nia wa ubunge ni wengi.
Afande Sele amesema kuwa hawezi kutoa pesa kugombea ubunge wakati wananchi wa Morogogoro ndio wanaomtaka agombee na yeye haendi bungeni kufuata maslahi bali kuwatumikia wananchi ndio maana katimkia ACT.