Adam Mchomvu ampiga msanii Q Chief

lukubuzo Samsis

JF-Expert Member
Nov 3, 2014
2,909
3,340
Adamu 'Mibangi' mtangazaji wa Clouds wa kipindi cha XXL amempiga makonde mazito msanii wa siku nyingi Q Chief/Q Chilla/Savimbi mnamo tarehe 1 March 2023,alivyokwenda kutambulisha/Kupreview Album yake kwenye kipindi hicho, msanii huyo aliweza kujizuia kutokuonyesha hali ya jazba na kuendelea na kilichompeleka.

Msanii Q chief amechukua hatua za kisheria dhidi ya mtangazaji huyo.

Habari zaidi msikilize mwanasheria wa msanii huyo,



Screenshot_20230314_181242_Instagram.jpg
Screenshot_20230314_181356_Instagram.jpg


Hii si mara ya kwanza Adam kufanya shambulio la kudhulu mwili, alifanya hivyo kwa Emanuel Mbasha, Alifanya hivyo Kwa Mtangazaji mwenzie enzi yupo Clouds Dina Marios, Geah Habib,nk hapo hapo clouds na kusababisha kusimamishwa kwa muda asiende kazini.

Hii tabia inaharibu brand ya Clouds iliyowekwa kwa muda mrefu.

Joseph Kusaga huyu bwana mdogo anakuharibia sana hapo clouds fukuza kazi ulinde brand ya kampuni,kampuni kwanza mtu baadae!

Mzaha mzaha hutumbua usaha wahenga walinena,usipoziba ufa utajenga ukuta.Wacha kukumbatia wahuni fukuzia mbali.
 
Huwa nashangaa jamaa huwa inakuwaje anakuwa na hasira za haraka hvyo wakati ni mtu wa masihara sana na kupenda kutania wenzie

Nakumbuka enzi diva the boss akiwa hapo alikuwa hapendi kabisa utani na huyu mwamba,jamaa akianzisha utani diva anamkata fasta(nilikujaga kugundua diva hapendi utani na huyu mwamba maana mara nyingi utani wake huwa ni wa kweli hachelewi kusema make up mbaya kama koboko)

Kimamy baby ndo kimeshamzoea huwa anakitania hakina tako na wala hakishituki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom