Sio tunataka trilioni 100+. Hicho ni kiasi walichoiba. Kama wanauwezo wa kulipa au la hilo ni suala lingine. Lakini kama wana hizo trillion 4 maana yk ni Kampuni kufilisiwa. Sasa hizo trillion 4 ni haba, +makinikia pale bandalini na kwamba wizi umethibitiwa, huoni kama huo ni ushindi na ukombozi mkubwa? Hata tukiamua kuwatimua bila kulipwa chochote ni poa, kwani hatutaendelea kuibiwa. Mfano una Marcopolo lako na baada ya miaka 5 umekuja gundua kuwa dereva wako alikuwa anaiba dizel na kukusababishia hasara ya mamilioni ya shillings, hutachukua hatua yoyote kisa dereva wako hana akiba ya hata laki moja? Hata hivyo aliyebeba dhamana ni Barrick. Unaujua utajili wa Barrick. Halafu nani kakwambia kuwa deni ni lazima lilipwe kwa mkupuo? Kama kwenye majadiliano ikathibitika kuwa kweli hasara ni tri.100+ hata jinsi ya kulipa wataafikiana. As long kama uchimbaji wataendelea nao, kitu ambacho hawatapenda kukipoteza tunaweza tukakubaliana nao kuwa kuanzia sasa wao watachukua 4% ya faida na sisi 96% mpaka hapo deni + riba litakapo kuwa recovered, na baada ya hapo business kuendelea ktk mkataba mpya utakaokuwa na manufaa kwa pande zote mbili. Mbuzi (Acacia) kaingia na kufanya uharibifu kwenye shamba la mtu kashikwa na anataka kuchinjwa. Mwenye mbuzi (Barrick) kaja na kuahidi kuleta watu wake kuja kuangalia uharibifu huo na kulipa na kuhakikisha yanaandaliwa mazingira ambayo kama ni yeye mwenyewe Barrick au mbuzi wake hatafanya uharibifu tena. Sasa mnanung'uniko na malalamishi yenu ya nini? Kama mnadhani ngoma hii ni nzito hamuiwezi kaeni kando kwani nani kawaita? Na kama saga hili linawatisha fumbeni macho. Kelele zenu zisije zikatuchanganya.Mnataka Trilioni 100 kwa kampuni ambayo asset zake zote na Mtaji haufikii trilioni 4 wehu kabisa nyinyi