Absalom Kibanda amnanga Tundu Lissu, asema Zitto amechezewa mchezo mchafu

Status
Not open for further replies.
Katika ukurasa wake wa facebook Absalom Kibanda ameandika, namnukuu "NAMTAFAKARI ZITTO KABWE: Hivi huyu kijana anastahili matusi, kejeli na dhihaka za namna hii kutoka kwa akina Tundu Lissu na viongozi wengine wa Chadema!!?? Ni stahili yake kuitwa msaliti? Ama kweli siasa ni mchezo mchafu na usio na shukrani"

My take; Kibanda nae anastahili kulaumiwa kwa kuyafumbia macho maovu ya chadema hapo mwanzoni kwakuwa tu alikuwa ananufaika na mfumo wa kifedhuli wa Mbwe......ha na katibu wake mafia wa "Rosse Brigate" Dr sinaraha. Ninaamini Kibanda anajua mengi kuhusu umafia ndani ya cdm na sasa anaishia kusikitika tu. Hayo ndo madhara ya kutojitambua mapema. Lakini afadhali ya Kibanda kwa kuwa yeye ni msuuuk....le uliojitambua!

Naliona anguko la Zitto Kabwe!
26/08/2009 | Posted by Absalom Kibanda | Makala | 29 views
NAOMBA nianze makala yangu hii kwa kuwaomba radhi sana wasomaji wa safu hii, ambao wiki iliyopita niliahidi kuendelea na hoja yangu kuhusu tatizo la ushabiki wa kisiasa, ambalo limekuwa likiliandama taifa hili kwa miaka mingi sasa.

Nimelazimika kuomba radhi kutokana na ukweli kwamba, nimejikuta nikipaswa kuachana na mada hiyo ya ushabiki wa kisiasa, baada ya kuibuka kwa moja ya mambo mazito katika siasa za ushindani na hususan katika medani ya ujenzi wa demokrasia madhubuti ndani ya vyama vya siasa vya upinzani.

Kikubwa kilichosababisha nifikie uamuzi huo, ni tukio kubwa na la kihistoria lililojitokeza wiki hii, ambalo mwanzo wake uko ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho hakuna shaka kwamba, afya yake ya kisiasa ya jana, leo na kesho ina mchango mkubwa katika maendeleo ya kisiasa katika taifa letu.

Tukio hili ambalo baadhi ya watu wanaweza wakaliona kuwa ni dogo na pengine lisilo na maana kubwa, ni lile la uamuzi wa mwanasiasa mchanga na kipenzi cha watu, Zitto Zubeir Kabwe, kuamua kujitoa mhanga na kugombea nafasi ya uenyekiti wa taifa wa CHADEMA.

Niseme bayana kwamba, uamuzi huo wa Zitto, mwanasiasa kijana aliyejizolea umaarufu mkubwa tangu alipoingia katika siasa za kitaifa ndani ya Bunge mwaka 2005, unaonekana waziwazi kuitikisa CHADEMA, na kwa kiwango kikubwa kugusa hisia za viongozi na wanachama wake na wale walio nje ya chama hicho.

Kikubwa kinachoonekana kuzusha maswali vichwani mwa watu wengi, nikiwamo mimi mwenyewe, ni uamuzi wa kijana huyo kuamua kugombea nafasi hiyo pasipo kujali iwapo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe anayemaliza muda wake atachukua fomu au la.

Ingawa watu wanaofahamu ujasiri wa Zitto katika kuchukua maamuzi mazito tangu akiwa shuleni na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaweza wakawa hawajashtushwa na uamuzi wa kijana huyo, ni wazi kwamba, hatua yake ya safari hii itakuwa imewafanya waanze kujiuliza mara mbili mbili kulikoni!

Katika hili la uenyekiti wa taifa wa CHADEMA, naweza kusema waziwazi kwamba, hata kwangu mimi ambaye mara kadhaa nimepata fursa ya kushiriki katika mawazo na maamuzi kadha wa kadha ya Zitto, nimejikuta nikishtushwa na namna alivyofikia uamuzi huu na kuutekeleza.

Ingawa nilikuwa nikijua japo kwa sehemu ndogo kuwa, Zitto alikuwa akipita katika tanuri gumu la kimaamuzi juu ya ama kugombea uenyekiti wa CHADEMA au kutogombea, bado sikuweza kujiaminisha kwamba, kijana huyu niliyemuunga mkono wakati wote alipokuwa akisimamia baadhi ya mambo makubwa ya kisiasa, angefikia hitimisho la kuwashtua watu wengi kwa uamuzi wake huu.

Watu wanaojua masuala ya CHADEMA ni mashahidi wazuri kwamba, uamuzi huu wa Zitto kuchukua fomu kupambana na Mbowe ambaye yeye mwenyewe (Zitto), mara zote amekuwa akimtambulisha kuwa ni ‘mentor’ wake wa kisiasa ndani ya chama hicho cha upinzani, tena kwa staili ya kumshtukiza, umesababisha mtafaruku mkubwa wa mawazo.

Ni wazi kwamba, uamuzi huu wa Zitto kuchukua fomu, kwa kiwango kikubwa umekuwa ni wa faraja kubwa kwa wana CCM, ambao siku zote wamekuwa wakitaka kuiona CHADEMA ikisambaratika na kukipa fursa chama hicho tawala kupumua.

Watu tunaolifahamu hilo kwa ndani, tunatambua vyema kwamba, kwa CCM na kwa maofisa usalama wa taifa waliolelewa katika mfumo wa siasa za chama kimoja, kuanguka au kuporomoka kwa uimara wa CHADEMA wa leo hii, ni jambo la kuliwekea mikakati na kwa kiwango kikubwa kulishangilia.

Kwa wana CCM na wapambe wao hao wa ‘kiusalama’, hatua yoyote ya kuwang’oa kutoka katika madaraka ya CHADEMA au ya kuwadhibiti watu wa aina ya Mbowe, Dk. Willbrod Slaa, John Mnyika na wanasiasa wengine madhubuti wengi tu wa ndani ya chama hicho cha upinzani, ni ya kushangiliwa na kuungwa mkono.

Ni wazi kwamba CHADEMA chini ya uenyekiti wa Mbowe na ukatibu mkuu wa Dk. Slaa, pamoja na kuwapo kwa kasoro zake nyingi za kiutendaji, kiutawala, kimfumo, kisera na pengine hata kiitikadi, imepiga hatua kubwa katika medani ya ushindani wa kisiasa ndani ya nchi hii.

Watu wanaofuatilia historia ya CHADEMA ya siku na miaka ya hivi karibuni, ni mashahidi wazuri kwamba, chama hicho kimeweza kujijengea misingi bora na imara kisiasa, kiasi cha watu wengi kukijengea imani na matumaini makubwa kwamba, kinaweza kikafanya mambo makubwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

Dalili hizi za CHADEMA kujijengea uhalali ambao umejidhihirisha wakati wa chaguzi mbalimbali ndogo zilizofanyika katika miaka ya hivi karibuni, kama zile za Tunduru, Kiteto, Tarime, Mbeya Vijijini, Busanda na Biharamulo, zimekuwa zikikifanya CCM na majemedari wake wa mikakati kujipanga na kukesha wakikiwinda, usiku na mchana.

Mawindo hayo dhidi ya CHADEMA yamekuwa yakijionyesha waziwazi kupitia katika vyombo vya habari, ambako kila mara taarifa za kupikwa na kufinyangwa dhidi ya chama hicho na viongozi wake, kama akina Mbowe, zimekuwa zikiandikwa mfululizo na kupewa uzito mkubwa.

Kwa ustadi mkubwa wa kufinyanga uongo, mawakala wa CCM wamefanya kila linalowezekana kumchimba Mbowe wakitumia falsafa ya Kibiblia isemayo; ‘Mpige mchungaji, kondoo watawanyike’ ili kufanikisha malengo yao haya ambayo matokeo yake hayatamgharibu mwenyekiti huyo pekee yake, au chama anachokiongoza, bali mafanikio yote tuliyopata kidemokrasia kama taifa.

Ni kwa sababu hiyo basi, Mbowe amepewa sifa mbaya kila wakati, akihusishwa na ukabila, ufisadi, udikteta, ubinafsi na kila aina ya sifa mbaya, lengo likiwa ni lile lile la kukivuruga chama hicho na kudumaza nguvu ya kiushindani ya vyama vya upinzani.

Mbinu hiyo haramu ya kutumia vyombo vya habari kumchafua Mbowe iliposhindikana, hata wakati ule ikafikia hatua ya kutumia hoja za aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Chacha Wangwe, mawakala hao wa CCM wakaja na mbinu nyingine mbadala.

Mbinu hii haikuwa nyingine bali ile ya kujaribu kuwagombanisha na kuwachonganisha viongozi wa kitaifa wa chama hicho kwa mbinu na staili tofauti.

Wakati fulani mwaka jana, Zitto alipofanya mahojiano na gazeti hili na kuulizwa kuhusu kusambazwa kwa habari za viongozi wa CHADEMA kugombanishwa, alikiri kulifahamu hili.

Wakati huo (Desemba mwaka 2007), vyombo kadhaa vya habari vilianza kuandika habari za kumpamba Zitto, zikimsifu kwa kuwa mwanasiasa kijana machachari na ambaye uwezo wake wa kiuongozi ulikuwa ukikizidi chama hicho na pengine viongozi wengine wa chama hicho.

Taarifa hizi za vyombo vya habari zilinikutanisha na Zitto na tukazijadili naye kwa muda mrefu kabla ya wote wawili kukubaliana kwamba, zilikuwa na lengo la kukihujumu CHADEMA na kuua dhana nzima ya upinzani hapa nchini.

Tulipofikia hatua ya kukubaliana naye, alifanya mahojiano na gazeti hili na akatoa tamko zito
ambalo kwa kiwango kikubwa lilisababisha mawakala wa CCM kuachana na ajenda hiyo. Kwa maneno yake mwenyewe wakati huo akirejea taarifa za vyombo mbalimbali vya habari alisema: ‘‘Tumegundua kuwapo kwa juhudi za makusudi za kutaka kutugombanisha CHADEMA. Hiki ni chama makini, kimezibaini njama hizo na kwa hakika hakiwezi kusambaratishwa.

“…CHADEMA ndiyo imenipa umaarufu mimi… mimi si maarufu kuliko chama. CHADEMA ni taasisi, ni chama ambacho kina misingi ya uanzishwaji wake.

“…(Wanasema) eti nilishinda kwa umaarufu wangu binafsi, si kweli. Niligombea ubunge nikitokea shule, sikuwa najulikana. Nilikuta ‘grassroots network’ ya chama, (chama) hakikujengwa na mimi.

“CHADEMA ilijengwa na uongozi uliokuwepo, nilikuta uongozi ‘intact’ (imara). Katika kila kijiji kulikuwa na uongozi na hata katika vitongoji vyote. Wakati naingia kugombea ubunge kulikuwa na wanachama wa CHADEMA wenye kadi wanaofikia 10,800 katika jimbo zima. Hawa sikuwatafuta mimi, niliwakuta na ndio waliofanikisha ushindi wangu.

“…Katika mazingira kama haya utasemaje kuwa mimi ni maarufu kuliko chama wakati chama ndicho kimenipa umaarufu?

“…CHADEMA ni chama ambacho wenyeviti wake wastaafu wanaendelea kuenziwa na kuhudhuria vikao vyote vya chama… ‘institutional memory’ ipo kuliko katika vyama vingine vya upinzani.

“…Alipohama (Dk. Aman Walid) Kabourou, wengi walidhani ndiyo mwisho wa CHADEMA Kigoma, lakini leo hii CHADEMA ni moto Kigoma kuliko ilivyokuwa awali.”

Ni jambo la ajabu kwamba, karibu miaka miwili tangu Zitto mwenyewe akiri kutambua kuwapo kwa njama hizo za kumkosanisha na viongozi wenzake na pengine kukihujumu chama chao, anaonekana akiingia katika mtego ambao miaka kadhaa iliyopita ulipata kukinasa chama kingine cha NCCR Mageuzi kiasi cha kukifanya leo hii kushindwa kufurukuta hata kufananishwa na baadhi ya watu kuwa ni sawa na shirika lisilo la kiserikali (NGo).

Ni jambo la kusikitisha sana kwamba, leo inapofikia hatua ya mwanasiasa kijana aliyekuwa akionekana kuwa moja ya mazao ya kuigwa ndani ya kambi ya upinzani tangu kukwama kwa akina James Mbatia, Mabere Marando, Augustine Mrema na wenzao wengine wengi, akifuata mkondo ule ule, basi ni wazi Watanzania wanaweza wakajikuta wakilazimika kukata tamaa zaidi na zaidi.
 
Lazima muumie sana, bao la dakika ya 90 tena la counter attack huwa linauma sana!!

Zama za Zitto CDM ndizo zinayoyoma, athari za kujifanya so smart ndani ya Taasisi.
 
kibanda ni mnafiki na hawezi kujiita mzalendo,leo anampinga mbowe wakati yeye kwa mikono yake ameshiriki kummaliza zito kabwe wakati akiwa tanzania daima?huyu ni mchumia tumbo,leo anamtumikia lowasa na rostam..rejeeni walaka wa kibanda wenye kichwa cha habari[NALIONA ANGUKO LA ZITO KABWE]
Mkuu, umeniwahi pokea like za kutosha, hata mimi hiyo makala naikumbuka sana, aliiandika kwenye ule ukurasa wake wa "Tuendako" Tanzania daiama Jumatano! Mmmh, hiyo avator ya mleta uzi nahisi kama akili zake zinafanana na mkao wake vile?
 
Unamchukuliaje mtu anayesifu jambo fulani leo na kesho akaliponda jambo hilo hilo? Ndiyo kusema "very fluid"? Tunahitaji watu ambao ni "very fluid"? Ni mtu gani mwenye tabia ya "very fluid" ambaye wewe unaweza kutamka kwa dhati ya moyo wako kuwa unamwamini. Be honesty with yourself. We most of the time need principle centered people. Siyo watu ambao ni "very fluid".

Fluidity katika politics ni pamoja na diplomasia ya kuvumilia mawazo ya wengine.
Na mawazo hayagandi hata siku moja, yaliyokubaliwa jana si yale ya leo.
Kingunge alikuwa mjamaa wa kutupwa miaka hiyo, leo kinara wa unyonyaji, na bado anapeta siasa za bongo.
Hakuna la ajabu watu kubadili misimamo yao, maana si mawe.

Wiki iliyopita Jk alikaa meza moja na Museveni na Paul Kagame.
Kagame miezi mitano iliyopita aliahidi "kumpiga" JK as a person, kitu ambacho si cha kawaida, na JK alilalamika katika moja za hotuba zake za mwisho wa mwezi.
Leo wanakaa meza moja na kukubaliana , na hata wasipokunaliana lakini watu wanasonga mbele, wakijua fika msimamo wa wengine.

Ni watu calibre ya Hitler wanao ua wasio kubaliana nao, na ni kwa vile upeo wao wa kuona mambo ni mfinyu, ila wana nguvu tu ya kidola.
Na hapo hakuna demokrasia.

Kama mtu hawezi kucheza chess ya siasa, hata JK kasema ni bora akalime.
 
hahahaha nmeipenda hiyo ma presdent is lowasaaaaaaaaa 2015..wasiotaka wajinyonge kama ben saanane kibaraka wa membe na redbrgade artifical wa chadema ambaye yupo kumtetea mbowe japo pia ni kbaraka wa membe najua atakuja chaap kujbu cz akskia neno lowasa huwa anaamin ruzuku ya Cdm 2015 itapunguzwa na kukaguliwa na CAG kila mwaka

naunga mkono hoja.
 
Hapa duniani unaweza ukafanya kazi serikalini miaka yote bila kosa na ukawa na sifa nyingi za ufanyikazi bora lakini ukkikosea siku moja kosa la kukufukuzisha kazi; utafukuzwa na kukosa malipo yako yote bila kukumbukwa mazuri uliyoyafanya. Kosa alilolifanya ni baya sana; hata akiachiwa uanachama atakuwa amehurumiwa. Haaminiki, anatumikia tumbo lake sio chama. Kwa kuwa mpango ulikuwa ni mbaya ndiyo maana walifanya siri na kujiita majina ya bandia ya herufi, maana jambo walilokuwa wakilipanga ni baya sana.
 
Labda Tundu Lissu yuko right according to the best of his knowledge

now swali hapa ni wat does Tundu knows for sure to be accurate?
The one highlited in RED.
Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao majina yao yamepitishwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Lucy Owenya (Kilimanjaro), Esther Matiko (Mara) Mhonga Luhanywa (Kigoma), Anna Mallac (Katavi), Paulina Gekul (Manyara), Conchesta Rwalumulaza (Kagera), Suzan Kiwanga (Morogoro), Grace Kiwelu (Kilimanjaro), Suzan Lyimo (Kilimanjaro), Regia Mtema (Morogoro), Christowaja Mtinda (Singida), Anna Komu (Dar es Salaam), Mwanamrisho Abama (Zanzibar), Joyce Mukya (Arusha), Leticia Mageni Nyerere (Mwanza) na Naomi Kaihula (Dar es Salaam), Chiku Abwao (Iringa), Rose Kamili (Manyara), Christina Lissu (Singida), Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano (Dar es Salaam), Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga (Dar es Salaam).
 
Fluidity katika politics ni pamoja na diplomasia ya kuvumilia mawazo ya wengine.
Na mawazo hayagandi hata siku moja, yaliyokubaliwa jana si yale ya leo.
Kingunge alikuwa mjamaa wa kutupwa miaka hiyo, leo kinara wa unyonyaji, na bado anapeta siasa za bongo.
Hakuna la ajabu watu kubadili misimamo yao, maana si mawe.

Wiki iliyopita Jk alikaa meza moja na Museveni na Paul Kagame.
Kagame miezi mitano iliyopita aliahidi "kumpiga" JK as a person, kitu ambacho si cha kawaida, na JK alilalamika katika moja za hotuba zake za mwisho wa mwezi.
Leo wanakaa meza moja na kukubaliana , na hata wasipokunaliana lakini watu wanasonga mbele, wakijua fika msimamo wa wengine.

Ni watu calibre ya Hitler wanao ua wasio kubaliana nao, na ni kwa vile upeo wao wa kuona mambo ni mfinyu, ila wana nguvu tu ya kidola.
Na hapo hakuna demokrasia.

Kama mtu hawezi kucheza chess ya siasa, hata JK kasema ni bora akalime.

Wale ni watu wana Nchi zao kaka .Zitto yuko within Chadema
Muda wote Zitto amekuwa akipayuka na kudharau viongozi wenzake .Kwa muda sasa amekuwa akifanyia kazi za ofisini online .Zitti kaza za pamoja za kujenga Chama amekuwa hashiriki na CCM walimwambia Chadema wana muhofia hawezi fanywa kitu na akazidi kuweka makundi kwenye Chama leo mnaacha yote haya mnasema Chadema wamvumilie ? Zitto kesha tuomba Watanzania msamaha mwaka jana au mwaka juzi kwa mambo yake ya ajabu ajabu haya .Wacha sasa watu wampe haki .Ana magazeti mengi kanunua aanzishe chapa chake apate kuwa mwenyekiti na Kibanda atamsaidia huko huko .
 
SOURCE:TANZANIA DAIMA 2009

CHADEMA, kiberiti kimejaa
Na Absalom Kibanda:
ZITTO Zubeir Kabwe, amefanikiwa kumtikisa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe na chama hicho na kwa hakika bado anaendelea kukiweka roho joho wakati huu anapoendelea kujipanga kisiasa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Ni wazi kwamba mwangwi wa kishindo cha uamuzi wa Zitto kuamua kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya juu kabisa ya kimadaraka ndani ya chama hicho akikabiliana na Mbowe kabla hajafikia makubaliano na ushauri wa kamati ya wazee wa chama hicho bado unaendelea kukisika ndani na nje ya chama hicho.

Nikiwa miongoni mwa watu ambao tumekuwa tukiitakia mema CHADEMA na hata kuthamini kwa dhati mchango madhubuti wa viongozi wa chama hicho na wanachama wake katika kuimarisha mfumo wa ushindani wa vyama vingi tangu kuzaliwa kwake na hususan kuanzia mwaka 2005 walipomsimamisha Mbowe kuwa mgombea urais, nilipatwa na hofu kubwa kuhusu aina ya mabadiliko ya kiuongozi ambayo chama hicho kinaelekea kuyakamilisha wiki hii.
Si kwamba nilikuwa na hofu kwa kuwa nayaogopa mabadiliko ya kidemokrasia, bali kikubwa kilichokuwa kikinisumbua ni ukweli kwamba, chama hicho kilikuwa kikifanya mabadiliko wakati huu taifa linapojiandaa kwa ajili ya chaguzi kuu mbili, ule wa serikali za mitaa unaokuja siku chache zijazo na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwakani.
Hofu yangu kuhusu hofu hii ya mabadiliko ambayo yangeweza kuwa ya hatari, ilizidi kuongezeka kila mara nilipokuwa nikiyasoma magazeti ama ya serikali au yale yanayomilikiwa moja kwa moja kwa njia za panya na mawakala au makada wa kimikakati wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nilipoanza kusoma habari katika magazeti hayo na kuona namna yalivyokuwa yakishabikia kwa mapana na marefu mpasuko ndani ya CHADEMA mara moja kengele ya hatari ilionekana kuanza kugonga kichwani mwangu na mwangwi wake ukanisukuma kuandika makala yangu ya wiki iliyopita iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho; ‘Naliona anguko la Zitto Kabwe’.
Kama hiyo haitoshi, mazungumzo ya ana kwa ana na yale ya njia ya simu ambayo niliyafanya na vijana mbalimbali walio ndani ya CCM wakiwamo wale walio na ushawishi mkubwa katika Jumuiya ya Vijana ya chama hicho tawala (UVCCM) na wabunge na kuwasikia namna walivyokuwa wakiufuatilia kwa umakini mkubwa uchaguzi wa CHADEMA na takriban wote wakisisitiza haja ya kufanyika kwa mabadiliko ya kiuongozi, mara moja niliiona hatari ikija.

Ilipofika hatua ya Zitto kuchukua fomu, ghafla homa ya uchaguzi ndani ya CHADEMA ikazidi kupanda na takriban vijana (siyo wote) wa CCM ambao wamekuwa na mawasiliano ya kirafiki na mwanasiasa mwenzao kijana kwa muda mrefu, walichukua maamuzi ya kumuunga mkono kwa nguvu kubwa na wote wakarejesha hoja nyingi zilizokuwa zikionyesha udhaifu mkubwa wa viongozi takriban wote wa chama hicho.
Ilipofikia hatua hiyo, mara Mbowe, Dk. Willibrod Slaa, Mnyika, Halima Mdee, Grace Kiwelu, John Mnyika na viongozi wengine wote wa CHADEMA ukimuacha Zitto wakaanza kuonekana kuwa ni watu wasiofaa, wakionekana kuwa hivyo ndani ya chama hicho na nje.
Katika mnyumbuliko huo huo, ndani ya CHADEMA ghafla taswira ya Zitto mwenyewe ikaanza kujipambanua na hali ikazidi kuwa bayana aliporejea kutoka nchini Ujerumani alikokuwa amekwenda kwa shughuli maalum ya ushauri kwa rais wa nchi hiyo. Nguvu zake halisi zikaanza kubainika.
Kile ambacho awali kilionekana kuwa ni uamuzi wake wa kujaribu kutikisa tu kiberiti kikaanza kubadilika kwa haraka na mara Zitto akajitokeza na kuwa tishio la wazi kwa uenyekiti wa Mbowe na kwa hakika akaanza kuwa tishio la majaliwa ya kisiasa ya chama hicho na kambi nzima ya upinzani wakati huu akili za Watanzania wadadisi wa mambo wanapoangalia mustakabali mwema wa ushindani mkali wa kidemokrasia hapa nchini. Ni bahati tu kwamba kiberiti kingali kimejaa.
Kwa hakika tafsiri yangu ya haraka haraka ikanipa jibu moja tu tena la haraka kwamba, maamuzi hayo ya Zitto yalikuwa kwa makusudi kwa ujinga wa wapambe wake wa kushindwa kuona mambo kuwa ulikuwa ikilenga kumhakikishia Rais Jakaya Kikwete ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80 alizokuwa amezipata mwaka 2005.
Ingawa baadhi ya watu wanaweza wakadhani mimi ni mwendawazimu ninapoliangalia tukio la Zitto kugombea uenyekiti wa CHADEMA wakati huu na kuwapo kwa jitihada za makusudi za kumsafishia Kikwete njia mwaka ujao, ukweli unabaki pale pale kwamba, makosa yoyote ya kisiasa yanayoweza kufanywa na viongozi waadilifu ndani ya vyama viwili vya CUF na CHADEMA wakati huu, yana nafasi kubwa ya kumhakikishia Rais wetu ahueni kubwa.
Ukiliacha hilo, mara moja nikakiona kitendo hicho cha Zitto mwanasiasa ambaye siku zote nimekuwa nikimuunga mkono anaposimamia na kupigania masuala ya msingi, cha kuamua kuutumia vibaya mwanya wa kidemokrasia wa kugombea uenyekiti wa taifa wa CHADEMA kuwa kilichokuwa kikilenga kwa kujua au kutojua, kupunguza makali na kasi ya chama hicho cha kushinda viti vingi katika chaguzi za serikali ya mitaa, udiwani na baadaye ubunge.
Nilipojiridhisha kwamba hayo yote yanaweza kutokea kwa sababu tu ya uamuzi wa Zitto kugombea uenyekiti na yakafuata hata kama atashinda au kushindwa katika mchuano huo, nikaona nitakuwa sikuitendea haki ndoto yangu ya siku zote ya kuona demokrasia ya vyama vingi inastawi katika nchi hii ambayo kwa takriban miaka 20 tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi CCM imeendelea kujivunia rekodi madhubuti dhidi ya upinzani.

Nilipoamua kuandika makala ya karipio na onyo dhidi ya Zitto katika safu hii, baadhi ya wasomaji wangu kwa makusudi au kwa kutojua wakakimbilia kuanza kunihukumu wengine wakisema najipendekeza kwa Mbowe ambaye ni mwajiri wangu, naganga njaa, nakandamiza demokrasia na wengine wakasema eti namzuia Zitto kutumia kipaji chake cha uongozi.
Ushawishi wote wa kundi hilo, ambao kwa kiwango kikubwa ulichagizwa na upotoshwaji mkubwa wa hoja yangu uliokuwa ikiratibiwa kwa karibu na vijana wa ndani wa CHADEMA waliokuwa wakimpigania Zitto na wale wa CCM na mawakala wao serikalini ulishindwa kulizuia Baraza la Wazee wa chama hicho, kumuacha kabla ya kumzuia kijana wao, kukiingiza chama chake na taifa katika balaa kwa kumsafishia Kikwete na chama chake mteremko. Ni jambo la kheri kwamba Zitto kwa dhati au kwa shingo upande aliliona hilo.
Kama alivyoandika Ansbert Ngurumo katika safu yake ya Maswali Magumu katika gazeti hili Jumapili iliyopita, Zitto na wapambe wake ambao nilifikia hatua ya kuwaita wajinga ambao waliamua kufumba macho na kuendelea kushangilia makosa ya kumruhusu Zitto kukimega chama ambacho siku zote amekuwa akionyesha kwa vitendo kubwa anakipenda kwa dhati wanapaswa kutulia na kutafakari kwa kina ni kitu gani hasa CCM na mawakala wake walikuwa wakikitafuta kutoka kwake hata ghafla kuanza kukiombea CHADEMA mema?
Kwa hakika unahitaji kuwa na akili za kuku za kusahau mapema ili kujidanganya kwamba, vijana ambao ni wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji au wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), wabunge, mawaziri na wanasiasa wengine serikalini wanaweza wakawa na mapenzi mema na CHADEMA hata kukiombea mema chama hicho wakati huu wakijua kuwa mwelekeo wa taifa ni Uchaguzi Mkuu ujao.
Hivi kweli wanasiasa katika vyama vya upinzani na Watanzania wengine hawajui kwamba, ndani ya vikao takriban vyote vya CCM na jumuiya zake, katika miezi na siku za hivi karibuni wamekuwa wakijadili namna wanavyoweza kushiriki katika kudhoofisha nguvu za CHADEMA kwa Tanzania Bara (baada ya kuidhoofisha CUF) na CUF kwa upande wa Zanzibar?
Hivi akina Mbowe, Slaa, Zitto, na wazee wa chama hicho wanaoongozwa na Mzee Edwin Mtei wamechukua hatua gani ili kuanzisha mchakato mahususi wa kufanya uchunguzi wa kina utakaowawezesha kubaini ni kwa kiwango gani nguvu za kifedha au za kiushawishi kutoka CCM na kwa mawakala wake zimefanikiwa kupenya akili za vijana na wazee wengi ndani ya chama hicho pasipo kujua au kwa kujua kiasi cha kujikuta wakiwa majeruhi wa kushabikia ujinga ambao kwa vyovyote vile matokeo yake yalikuwa yakiwachulia wao na chama chao anguko la kihistoria?
Maswali kama hayo tunapaswa kujiuliza hata sisi wana habari ambao kama ilivyokuwa kwa vigogo hao wa CHADEMA kwamba ni kwa kiasi gani kalamu zetu zimechochea au kudhoofisha jitihada mahususi ambazo ziko wazi na zinazolenga kukisambaratisha chama hicho cha upinzani ambacho hakuna shaka kimejipambanua kuwa chama shupavu katika miaka ya hivi karibuni?

Wakati sote tukitafuta majibu ya maswali hayo, tunao wajibu wa kutambua kwamba, pamoja na uamuzi wa Zitto kutangaza kujitoa katika kinyang’anyiro cha uenyekiti, ile sumu kali ambayo tayari imeshapenya mishipa ya uongozi ya chama hicho, haina budi kutafutiwa dawa mahususi ya kuipatia tiba ya haraka kwani tayari vijana wa kazi wa CCM na mawakala wao wameshatamba kwamba wameshakiachia vidonda vingi chama hicho ambavyo wanadai vitaendelea kukitesa hadi wakati wa chaguzi zijazo. Kwa sababu hiyo basi, ninaweza kusema kwa kujiamini kabisa kwamba, kile ambacho leo hii kinaendelea kuelezwa na kusisitizwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa ni demokrasia kandamizi ya ndani ya CHADEMA (eti kwa sababu ya uamuzi wa wazee wa CHADEMA kumzuia Zitto kugombea uenyekiti) si tu kwamba ni majuto ya kukwama kwa ajenda yao, bali ni mkakati mbadala wa kuendelea kukiumiza chama hicho kwa malengo ya kisiasa. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.
 
Kibanda alioona.mbali katika makala hii....kuku tuliowafungulia asubuhi ndo haooo wanarudi bandani
 
Huyo pamoja na Ngurumo ni mojawapo wa waandishi wa habari ambao dunia na Tanzania ilipata kuwa nao. Kibanda ni mtabiri na si mwandishi pekee. Nampenda sana huyu jamaa kwa uandishi wake. Hajui kuremba huyu bwana. Napita tu waungwana.
 
Kibanda aliyeandika haya sio huyu tunayemjua sasa. Ameshakuwa Wakala wa wale wanaotaka kuona Tanzania haisongi mbele sababu ya kushabikia matumbo yao. Unless sasa anatuambia kwamba hiki alichokiandika awali alikiandika kiushabiki ama alishanunuliwa na viongozi wa CHADEMA kipindi hicho. Kwani mazingira yaliyotumika kipindi hicho kwa Zitto na wafuasi wake kukidhoofisha chama anachodai kukipenda sana hayajabadilika sana zaidi yamekuwa mabaya zaidi.
 
Halafu akaajiriwa na HUSSEIN BASHE kada wa CCM kwenye taasisi inayomilikiwa na ROSTAM AZIZ kada wa CCM akitokea kwenye taasisi inayomilikiwa na FREEMAN MBOWE kada wa CHADEMA?
 
Kazunguka sana ila hajaeleza ni kwa vipi kugombea uongozi kwa Zitto kungedhohofisha chama

Kakazana mara UVCCM,mara wafuasi wa Zitto....haeleweki..,kifupi sijamwelewa.

Huyu kweli alikuwa anatetea ajira yake!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom