93.6% ya Watanzania wote walizaliwa baada ya Muungano

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa Nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.

Muungano huu ulioasisiwa na viongozi wakuu wa nchi hizo ambao ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza Tanganyika na Sheikh Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ulifanyika mwaka 1964 kwa nchi zote kuridhia makubaliano hayo.

Wakati nchi hizi mbili zikiungana mwaka 1964, Tanzania ilikadiriwa kuwa na idadi ya watu 9,649,925, kati ya watu hao, wanaume walikuwa 4,432,599 na wanawake walikuwa 5,217,326 sawa na asilimia 46 kwa 54 mtawalia. Aidha, idadi ya watu kwa Tanganyika ilikuwa 9,354,560 wanaume wakiwa 4,291,869 na wanawake 5,062,691. Idadi ya watu Zanzibar ilikuwa 295,365 kati yao wanaume walikuwa 141,800 na wanawake 153,565.

Idadi ya watu waliokuwepo Tanzania wakati wa muungano mwaka 1964 ikiwa ni miaka 59 toka kuasisiwa kwake, imepungua kutoka 9,649,925 na kubaki watu 3,976,320 sawa na asilimia 41.2 ya watu wote waliokuwepo kabla na wakati wa muungano. Kati ya watu hao, wanaume ni 1,826,484 na wanawake ni 2,149,836. Kwa Tanzania Bara idadi hiyo imepungua kutoka watu 9,354,560 na kubaki watu 3,875,304 ambapo kati yao wanaume walikuwa 1,777,988 na wanawake 2,097,316. Kwa Zanzibar idadi hiyo imepungua kutoka 295,365 na kubaki watu 101,016 kati yao wanaume walikuwa 48,496 na wanawake 52,520.

Tangu kuasisiwa kwa muungano hadi kufikia mwaka 2023, miaka 59 baadae, idadi ya watu waliozaliwa na wanaoishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni 57,764,800 ikiwa ni asilimia 93.6 ya watu wote waliopo nchini kwa sasa, kati yao wanaume ni 28,226,646 na wanawake ni 29,538,154 sawa na asilimia 49 na 51 mtawalia. Kwa Tanzania Bara, idadi ya watu waliozaliwa baada ya muungano ni 55,976,043 ikiwa ni asilimia 93.5 ya watu wote Tanzania Bara, ambapo kati yao wanaume ni 27,359,650 na wanawake ni 28,616,393; wakati kwa Zanzibar idadi ya watu hao ni 1,788,757 ikiwa ni asilimia 94.7 ya watu wote Zanzibar, ambapo kati yao wanaume ni 866,996 na wanawake ni 921,761.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa, kati ya watu wote waliopo nchini kwa sasa, asilimia 6.4 walizaliwa kabla ya muungano. Idadi hii ni hazina muhimu kwa Taifa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii, utamaduni na mazingira. Wengi wa watu hawa ni tunu katika kujifunza namna ya utunzaji wa mila na desturi zetu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho hasa katika wakati tulio nao ambao vijana wengi wanaiga tamaduni za kigeni ambazo ni kinyume na tamaduni na mila za asili za Mtanzania.


Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu
 
Kuna Mzee nimewahi kuonana naye yupo hai hata sasa, akianza kunisimulia mambo ya Tanu hadi utapenda vile walivyo kuwa na Uzalendo wa kweli kwenye Nchi, sio hawa Viongozi wa miaka hii.
 
Back
Top Bottom