Kuna breaking news kwenye gazeti la Mwananchi kwamba basi la Tashriff limepata ajali na watu 27 wamepoteza maisha. Mwenye habari zaidi aziweke hapa ukumbini. Haya mabasi yanatumaliza tu Watanzania kwa ajali ambazo zinaweza kabisa kuzuilika.
Jamani, tukiacha suala la madereva wazembe, je amuoni kama hizi barabara zilivyofinyu na hazina highway patrol za kuyavuta magari mabovu na kuyaondoa barabarani pia zinachangia. Kwa nini serikali isianzishe mradi wa kuzipanua barabara, kuwalipa matrafiki mishahara mizuri na kuakikisha wavunja sheria wanachangia katika kujenga hizi barabara kupitia faini. Mfano trafiki anapata bonus kulingana na magari anayokamata kwa makosa barabarani etc.
Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha.
Jamani, tukiacha suala la madereva wazembe, je amuoni kama hizi barabara zilivyofinyu na hazina highway patrol za kuyavuta magari mabovu na kuyaondoa barabarani pia zinachangia. Kwa nini serikali isianzishe mradi wa kuzipanua barabara, kuwalipa matrafiki mishahara mizuri na kuakikisha wavunja sheria wanachangia katika kujenga hizi barabara kupitia faini. Mfano trafiki anapata bonus kulingana na magari anayokamata kwa makosa barabarani etc.
Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha.
Ama kweli nyani haoni kundule...!Shadow... una mawazo mazuri ya ubunifu! Lakini sio wengi wanojishughulisha kubuni kama wewe. Viongozi wengi wamekaa kungojea ajali zitokee watoe "vapour" zao halafu kesho yake "business as usual". Akili zao sio tofauti na za nyani ambao wakipigwa na baridi usiku wanajikunyata na kusemezana... "kesho asubuhi na mapema lazima tujenge nyumba". Inapofika asubuhi jua likitoka wanasahau kila kitu....... Ndio akina Makamba na CCM hao... Maneno meeeeeengi...
Nakubaliana nawe, lakini hili la mishahara mizuri si kwa trafiki tu, kila mtu TZ anahitaji kipato kitakachokidhi mahitaji yake, hapo ndio tutaondoa kwa kiasi fulani ama kupunguza rushwa. Hawa trafiki hutoza madereva wanaovunja sheria, hilo lipo, na nakumbuka juzijuzi Kamanda Kova alitangaza kiasi kilichopatikana. Lakini fedha nyingi huishia kwa hawa jamaa, wakimkamata mtu huchukua rushwa na kumuachia, vilevile mtu akijua kuwa kosa lake ni kutoa 50,000 akifika polisi, basi hutoa 20,000 anayoambiwa na kuachiwa. Pia mabasi huwa yanajaza fomu fulani kuonesha waliondoka saa ngapi, ili wakifika katika kituo cha ukaguzi waonekane kama wanaenda mwendo wa kawaida, lakini hili halisaidii, wakifika kwenye hivi vituo hutoa rushwa. Sasa hivi njia ya Mwanza mpaka Dar es Salaam ni kama imeisha, gari zinakimbizwa vibaya mno, na ni hatari, wafuatiliaji ndio hao.
Lakini na raia nasi tuna lawama, gari likikimbizwa kupita kiasi huwa tunakaa kimya, na kama ukisema utaoingwa na wengine kuwa tunataka kuwahi. Mwisho wengi wa madereva ni wabovu, kwa kuwa kila kitu pale TZ waweza pata kwa hela, hawa madereva wengi hupata leseni kwa kuhonga, bila hata kufanyiwa majaribio kwa undani.
Mkuu maneno yako niliyoya-highlight na rangi ya bluu (ambayo ndio wimbo unaoimbwa kila ajali kubwa inapotokea) yanaweza kuonekana kama ni utatuzi wa hilo tatizo lakini mimi siafiki.
Uzoefu unaonyesha kwa sababu mbalimbali, ni vigumu kwa abiria kuweza kum-control dereva. Hata nchi nilizotembelea ambazo hazina ajali za kizembe kama Tanzania sio kazi ya abiria kuwachunga maderava wasizembee. Hivyo basi kama hili limeshindikana inatakiwa itafutwe njia nyingi.
Mara nyingi ajali kama hii zinapotokea serikali husema ni uzembe wa madereva. Ukiangalia vizuri, sababu kubwa ni uzembe wa serikali.
Ajali nyingi ni za koganga lori lililoegeshwa barabarani. Kukosekana kabisa kwa sehemu za kupaki pembeni mwa barabara ndiko kunafanya magari yaegeshwe barabarani.
Barabara ya Dar hadi Tanga naijua sana. Haiwezekani kuegesha gari pembeni kwani hakuna pembeni. Ukiegesha gari lazima uegeshe barabarani. Ni nyembemba kupita kiasi, na haina parking shoulders.
Uzembe wa serikali ulijitokeza tangu kwenye design. Ilibidi ziweko parking shoulders.
Vile viule, uzembe wa serikali unajitokeza wazi wazi sehemu ambazo zimewekwa matuta. Ni wenda wazimu kuweka tuta barabara ya lami bila kulipaka rangi za kuhakiksha linaonekana kabla halijafikiwa.
Chanzo kikubwa cha ajali za magari Tanzania ni uzembe wa serikali. Ni serikali mbovu.
Pia madereva hawataki kufuata sheria za barabara. Huyu dreva wa lori lililoegeshwa barabarani kwa maoni yangu inabidi akamatwe kwa makosa aliyoyafanya na huyo dreva wa bus kuna uwezekano mkubwa labda alikuwa katika speed kali sana na si ajabu haoni vizuri usiku hivyo anahitaji miwani ya kumsaidia kuona vizuri. Kuna haja ya kuwa na sheria kali za barabarani, na pia kupambana na askari wa barabarani wahuni ambao wanabasababisha sheria za barabarani kutoheshimiwa kwa uchukuaji wao wa rushwa.
Tanzania watu wengi wanaendesha bila leseni hawajui chochote kuhusu sheria za barabarani na hata wale wanaozijua sheria hizi hawaziheshimu matokeo yake ndiyo hizo za ajali zisizokwisha zinazosababisha maelfu ya Watanzania kupoteza uhai wao kila mwaka au kupata vilema vya maisha.