2015 tuchague raisi mwenye uzoefu wa biashara na sio mwansiasa.

Tango73

JF-Expert Member
Dec 14, 2008
2,128
1,225
Ndugu wanajamii. Napendekeza mwaka 2015 tuchague mfanya biashara maarufu mwenye mafanikio makubwa na sio mwenye jina kubwa lakini mikopo ya benki kibao. Brazil walimchagua mfanya biashara maarufu mwenye kumiliki viwanda vikubwa vya nguo, na matokeo yake sasa brazil wapo pazuri sana na wameisha jitoa katika recession. Italy wamemchagua Belaruskon Mmiliki wa AC Milani, na mfanya biashara mkubwa pale milan. mambo yao sasa Italy ni mazuri sana. Sasa hapa tanzania naona tujalibu kuwapa uraisi wafanya biashara maarufu , ndugu zangu mnaonaje hilo.
 
Lowasa anafaa sana!
Rostam Waziri Mkuu!
Manji Makamu wa raisi!
 
Kwa nin tusibinafsishe nafai ya urais..yaani tutangaze 'tender'...tunaweza kumpata...Murdoch..
 
Tango sio kila kinachofaa kwa mwenzio nawe pia.... Kipara alikua/ni mfanya biashara

mkubwa saaaaana.... ilisaidia nini?? thou walau uchumi kwake ulikua nafuu katika history ya TZ....
 
Ndugu wanajamii. Napendekeza mwaka 2015 tuchague mfanya biashara maarufu mwenye mafanikio makubwa na sio mwenye jina kubwa lakini mikopo ya benki kibao. Brazil walimchagua mfanya biashara maarufu mwenye kumiliki viwanda vikubwa vya nguo, na matokeo yake sasa brazil wapo pazuri sana na wameisha jitoa katika recession. Italy wamemchagua Belaruskon Mmiliki wa AC Milani, na mfanya biashara mkubwa pale milan. mambo yao sasa Italy ni mazuri sana. Sasa hapa tanzania naona tujalibu kuwapa uraisi wafanya biashara maarufu , ndugu zangu mnaonaje hilo.

Brazil si Tanzania ndugu yangu, Kwanza hangaikia katiba yako - haya yote tuliyonayo ni results ya katiba ya wakoloni. Katiba inampa mamlaka makubwa na ya ajabu Rais. Sasa ukipata Raisi asiye makini ni hatari kwa taifa - na haya ndiyo matunda yake.

Tusitafute mchawi - cha msingi tubadili katiba kwanza.
 
Hivi matajiri wa TZ ni wote wahindi na warabu? Na msiseme Reginald Mengi kwa sababu nyuma yake kuna wadosi.
 
Back
Top Bottom