2009 - kisiasa

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Kwa kuwa naamini kuwa; Tunaweza kutofautiana katika mitizamo ya kisiasa lakini sote ni sharti tuishi na kutumika kwa ajili ya MAendeleo ya watu na Taifa kwa ujumla.

Na kwa vile Chama chetu cha Mapinduzi kimeonekana kuwa sasa kimepoteza imani toka kwa wananchi wengi (ndani na nje ya CCM) na hatuoni dalili za kujirekebisha.

Na kwa sababu mwakani tuna muda mfupi wa mwaka kabla ya uchaguzi mkuu, basi tunapaswa kupanga sasa mkakati madhubuti usio na unafiki ili kuwapata Viongozi ambao UTII WAO UTAKUWA KWA WANANCHI KWANZA KABLA YA CHAMA WALA URAFIKI.

Sijui ninyi mnafikiria nini, mimi niko njia panda ama:-

1. Tuwashinikize kwa nguvu zote, kila siku, popote, kwa namna yeyote ya amani vyama vyote vya upinzani Tanzania (wavunje vyama vyao) waungane na tupate mgombea na mwenza wake wanaofafa na kukubalika halafu sote tuwapigie kampeni iliyoenda shule kwa ajili ya kupokea ushindi 2010.
au


2. Tunaoona kuwa CCM ya sasa imepoteza mwelekeo lakini bado tuna nafasi kuliko vyama vingine vya sasa vya upinzani, tujimegue kwa kishindo na kuunda chama tukiite mfano :- CCM-Wananchi na tuwateuwe wawili wasio na mawaa na wenye uwezo wa kuongoza tuwapigie kampeni ya kitaalamu kujiandaa kurejesha Tz katika kuelekea ustawi wa Wananchi.

Pengine wengine mna mawazo tofauti yote yanakaribishwa maana nimeona kuwa siwezi kuendelea kuugua moyoni kwa jinsi ninavyokaa kimya tu wakati nakufa na tai-mbano ya CCM shingoni.
 
CCM - Mageuzi... as long as wafuatao hawamo:

Wanachama wa sasa CCM ambao majina yao yametajwa kwenye kashfa yoyote ya ufisadi, ujambazi, wizi, uzembe, ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka, na mikataba mibovu. Hawa wakishatolewa nje, then we got the party to start with.
 
Mwanakijiji- nakubaliana nawe kabisa!

Mpita njia- Kweli tatizo ni watu (viongozi) walio katika CCM, sasa kama wanangángánia na kutumia mbinu zote chafu hata za kuwahonga wenzetu kiasi cha kuendelea kuwemo humo basi tunaotaka haki na maendeleo hatuna budi ama kuunda kingine au kuungana na wapinzani. Hata kenya ilianza hivyo.

Kutokana na mtandao mpana uliopo tayari wa CCM, kuna watu wengi wanaonyesha kuwa mapinduzi ya kweli yatatokea ndani ya CCM!
Kuna wazee kibao huko vijijini wakati wa uchaguzi bado wanauliza kuwa mimi nataka chama cha Nyerere na hapo ndipo anapiga kura. Sasa afadhali 2010tuwambie kuwa chama cha Nyerere kimegawanyika mara mbili, kile cha mafisadi na kile kipya kinacholinda maadili ya Nyerere utaona jinsi tutakavyorahisisha shughuli hivi pevu.
 
Back
Top Bottom