Siri ya Dr.Slaa na Dr.Ayub Rioba kuwa na msimamo sawa kuhusu Amani

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Awali ya yote, natumia jukwaa hili kuwapongeza wana UDASA kwa kongamano safi kwa maslahi, bila shaka mjadala unaendelea na sasa hapa JF tuangazie; amani huletwa au huvurugwa na nini?

Mengi yamezungumzwa, lakini mimi hoja zangu nitazielekeza kwa wasomi wawili waliotoa mitazamo sawa kuhusu mantiki ya amani. Dr.Willibrod Slaa na Dr.Ayub Rioba, hoja yao ni moja tu katika hili yaani "amani haihubiriwi,haiombewi wala haitekelezeki kama sera bali haki ni sera ya amani".

Wapo wanaowachukulia wasomi hawa kama wasaliti wa amani, lakini mimi nawaona ni marafiki wa amani. Tufikiri, ni amani huleta haki au haki huleta amani? Kama haki huleta amani, bila haki hakuna amani, hivyo haki ni amani. Ndivyo waonavyo wawili hawa na wengine wenye mtazamo kama wao.

Kwa mantiki hii, Kama msimamo wa Mhe.Mwigulu na Mhe.Nchimbi kuhusu kuombea amani kuna hoja, naomba tujadili maana hata Syllogism argument haipo!
 
ZeMarcopolo; Hakuna binadamu asiyependa amani na hakuna binadamu asiyechukia dhuluma.Tunataka hoja siyo chuki binafsi ndugu yangu. Binafsi nimejaribu kutengeneza categorical argument kuhusu msimamo wa Mhe.Nchimbi kutaka tuzidi kuombea amani bila kumsahau Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mhe.Mwigulu Nchemba.Mfano mdogo, mtu akipokonywa ardhi na kupewa mwekezaji; tufumbe macho tuombee amani isivurugwe au tumsaidie aliyepokonywa ardhi,haki itendeke (fidia halali) kisha amani idumu? Soma vizuri nadharia hizi mbili kisha useme, ipi ni jawabu la amani. Mosi, "Msingi wa amani ni haki, bila haki hakuna amani.Hivyo haki ni amani." Nadharia ya pili, "Msingi wa amani ni maombi, bila maombi hakuna amani.Hivyo maombi ni amani"
 
Last edited by a moderator:
Radhia Sweety; Haya masuala ya Biblia & Quran kama huijui misingi yake ni vema usitumie.Mfano, Yesu alitumia sarafu iliyokuwa na picha ya Kaisari kusema, "Yale ya Kaisari mpeni Kaisari na yale ya Mungu mpeni Mungu".Je, unadhani aliwataka wakristo wasitoe dhaka kwa mfumo wa pesa zenye watawala wa duniani? La hasha, ile ni lugha ya picha. Ukisoma mara 5 mstari ulionukuu, utagundua kwamba haumaanishi kuomba amani bali kuiombea amani tena kwa lengo la kuzidi kupata hekima kutoka kwa Mwenyezi Mungu.Na amani inayozungumzwa hapo ni ile amani ya kiroho na ndiyo maana neno hekima linahitimisha haja ya maombi.Usikurupuke!
 
Last edited by a moderator:
Dah umekosea kifungu ulichoquote hiyo Yeremia 10:13 ni hii
13 Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.

Inategemea unatumia toleo lipi. Mimi natumia Agano la kale.
 
Radhia Sweety; Haya masuala ya Biblia & Quran kama huijui misingi yake ni vema usitumie.Mfano, Yesu alitumia sarafu iliyokuwa na picha ya Kaisari kusema, "Yale ya Kaisari mpeni Kaisari na yale ya Mungu mpeni Mungu".Je, unadhani aliwataka wakristo wasitoe dhaka kwa mfumo wa pesa zenye watawala wa duniani? La hasha, ile ni lugha ya picha. Ukisoma mara 5 mstari ulionukuu, utagundua kwamba haumaanishi kuomba amani bali kuiombea amani tena kwa lengo la kuzidi kupata hekima kutoka kwa Mwenyezi Mungu.Na amani inayozungumzwa hapo ni ile amani ya kiroho na ndiyo maana neno hekima linahitimisha haja ya maombi.Usikurupuke!

Toa umbea wako hapa. Unataka kusema Mungu hajishughulishi na amani ya nchi? Mbona waisraeli walipoona Wakaldayo wanawajia na silaha walimuomba Mungu. Mungu akamchagua Daudi.
 
Last edited by a moderator:
Radhia Sweety; Samahani, sikujua kwamba hujui lolote kuhusu theolojia na hata uwezo wako wa kupambanua mambo ni mdogo. Usichukue neno moja, ukahitimisha kwamba ndiyo mantiki ya mstari mzima.Isitoshe, muktadha wa mstari huo hauendani na kile unachotaka tuamini. Laiti kama ningekuwa siamini kwamba Mungu hajihusishi na amani ya dunia basi ningesema, "yale maneno kwamba heshimuni mamlaka" ni ya uongo.Ukiendelea na umburula wako si ajabu utakufa kwa ujinga.Yesu wa Nazareti amemwaga viti kwanye sinagogi na kusababisha vurugu na taharuki kubwa pale ambapo walipageuza kuwa soko/sehemu ya walanguzi hali ni pahala pa ibada.Unadhani hakupenda amani? Anyway, rudi kwenye mada.Tuwekee hapa hoja yenye strength kwenye premises ya maombi na namna maombi yanavyoweza kudumisha amani badala ya haki.
 
Last edited by a moderator:
ZeMarcopolo; Hakuna binadamu asiyependa amani na hakuna binadamu asiyechukia dhuluma.Tunataka hoja siyo chuki binafsi ndugu yangu.

Mkuu, samahani lakini hii kauli yako iko TOO NAIVE. Hivi unadhani vita vinatokea bahati mbaya? hujui kuna watu wanakaa chini kubuni jinsi ya kuwachonganisha watu ili waanze kupigana then wakawauzie silaha.

Kuhusu dhuluma, ingekuwa watu wote wanaichukia basi dunia ingekuwa alot better place for mankind...
 
Slaa kachanganyikiwa. Yaani huyu jamaa pimbi kweli. Eti anasema amani haiombewi. Hajui hata kusoma Biblia inayosema kwenye kitabu cha Yeremia 10:13 kuwa ''endeleeni kuiombea amani ili Mungu wa Israeli awashushie hekima yake hadi siku ya kurudi kwa Yesu.''
Yeremia 10:13 inasema hivi; Atoapo sauti yake pana mshindo wa maji mbinguni, naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; huifanyia mvua umeme, hutoa upepo katika hazina zake.

Wewe Radhia Sweety haya maneno uliyoandika kwenye mstari mwekundu umeyatoa wapi? Afterall, unaonekana huna hata knowledge ya Biblia. Kwa kuwa kitabu cha Yeremia kipo katika agano la kale, ambapo Yesu Kristo alikuwa bado hajazaliwa. Sasa huyo Yesu unayemwandika hapa umemtoa wapi? Maana hata hilo jina Yesu lilikuwa halijulikani wakati huo.

Yaani Radhia sweety niliyemfahamu mwanzoni mwa mwaka 2012 na huyu anayeandika hivi sasa ni watu wawili tofauti kabisa. Yule Radhia mwenye hekima na uelewa mkubwa wa mambo sijui alikufa, na ID yake kumpa mwingine?

Badiliko dada!
 
Kwani wewe siku zote bado unamwamini huyo demu?
 
Last edited by a moderator:
Hivi Dr Slaa haoni kama ana jidhalilisha kusema amani haiombewi?
Unajua wewe HAMY-D sometimes huwa unaandika mambo ya kichizi chizi sana. Ni theory au principle gani za amani duniani zinazosema amani inaombewa? Uliwahi kusoma course inaitwa "Peace, conflicts and conflicts management? Naamini ungesoma hata module moja tu, usingekaa hapa kuandika haya unayoyaandika. Hivi kama wananchi wananyanyaswa, wanauawa, gharama za maisha zinaongezeka, polisi wanawabambikia kesi watu wasio na hatia, wengine wanawabakwa. Unataka maombi hapo kuzuia hawa watu wasiingie msituni kuing'oa hiyo serikali?

Hizi kazi za kuombea amani waachieni wachungaji na wapiga ramli. Maana wao wanaamini katika Mungu na mizimu. Lakini serikali haiendeshwi kwa misingi ya imani, inaendeshwa kwa misingi ya falsafa, kanuni na taratibu. Acheni umburula nyie CCM, ndiyo maana hali ya nchi inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, kutokana na kuendesha nchi kwa misingi ya imani tena imani za akina Sheik Yahya.
 
Du!! Naona CCM wamevamia JF. Hakika hakuna kisichokuwa na mwisho aminini nawaambia, sijatumwa duniani kuja kuhubiri siasa ila kushudia anguko la CCM. Leo Utaamini haitaanguka kwa kuwa uwezo wako umejazwa zuruma, siku zote usishindane na ukweli. Wewe unasimu au computer inayokuwezesha kuandika haya lakini walio wengi hawana uwezo huo na ndo they love Chadema. Wao wanaipenda Chadema kwa moyo wao wote lakini nyinyi mnaipenda CCM kwa kuwa inawapa pesa na imewapa nafasi ya kuzurumu mali zetu.
Mko na dalili zote za kuanguka, na mmejaa kiburi sana CCM. Hakika is time now, wenye kuona mbali wameshajua na wamejipanga. Real tumieni akiri zenu humu nyie ni wezi tu na mmekubuhu kwa kuuza madawa ya kulevya. Now ni mwaga mboga namwaga ugali
 
Slaa kachanganyikiwa. Yaani huyu jamaa pimbi kweli. Eti anasema amani haiombewi. Hajui hata kusoma Biblia inayosema kwenye kitabu cha Yeremia 10:13 kuwa ''endeleeni kuiombea amani ili Mungu wa Israeli awashushie hekima yake hadi siku ya kurudi kwa Yesu.''

Yeremia 10:13 imeandikwa hivi....
Yeremia 10 : 13
10.13 Atoapo sauti yake, pana
mshindo wa maji mbinguni, Naye
hupandisha mawingu toka ncha za
nchi; Huifanyia mvua umeme,
Huutoa upepo katika hazina zake.
Hiyo uliyoitaja wewe ni Yeremia ya Mas.aburini kwako?
 
Slaa is total disappointment. Kiongozi gani wa dini asiyeamini maombi!!! Hakuna kitu kinaweza kufanikiwa bila kumuomba Mungu...

Yeremia 10:13 imeandikwaje? Kama hadi maneno ya Mungu mnayachakachua kwa chuki zenu za kisiasa Mmelaaniwa nyie
 
Back
Top Bottom