Mkuu skype, hao airtel ndo wezi kupindukia. Hawakunasa tuu. Nilinunua bundle nikapata mb127, ndani ya dakika 28 za kusoma email hizo mb zimeisha na wakatafuna airtime yangu laki na sitini na tano! Kupiga customer care hamna kitu. Kwenda ofsn kwao wakasema watarudisha network yao ilikuwa na...
Vodacom, mnashughulikia tatizo langu kwa kuwa ni general problem au? Hii meseji yenu nitaitumia kama ushahidi ikitokea mmelamba salio langu muda huo ukifika
Line yangu huwa nawekewa salio na ofisi na naweka salio pia. Sasa nina salio niliweka huwa halitumiki mpaka la ofs liishe. Nikiangalia salio kwa sasa mnaniambia kufikia 04.12.2014 niwe nimelitumia limeisha!! Je, hii ni haki? Kwanini mniwekee limit ya muda ya kuwa na salio kwenye cm yangu?
Sheria ya kodi inasema 'pato lolote mtu analopata kutokana na kazi linatakiwa likatwe kodi' kwahiyo hata hizo taasisi za serikali zisizowakata wafanyakazi wao kodi ni kinyume na sheria.
Bank charge ninazozifahamu ni pale unapodraw kwa atm ni 700 TRAnsaction, monthly charge najua ipo pia ila nafkiri mtu anaposema arrears nahisi ni gharama ulitakiwa uchagiwe lakini hawajacharge! Ukiangalia kwenye statement yako kama unafuatilia utagundua ninachosema ni charge isiyojulikana chanzo...
Mkuu carnys, ni branch ipi hapa Dar umeenda ukapewa huduma nzuri? Natamani nami niende hapo. Kila mwezi unakuta wamekuandikia ' charge arrears' hapo unakatwa kati ya 1500-2000. Ni zipi wakati hata ukichomeka kadi na huku atm mashine haina hela unachargiwa? Hata mi sina hamu nao
Wizi/ujambazi sio mzuri kabisa. Majuzi huku kwetu jet mwisho wa lami hatukulala, tangu saa nane usiku ni risasi zinapigwa tuu na jamaa walikuwa na pikipiki. Walikuwa wanazunguka utafikiri nyumba kwa nyumba na wanatupa risasi mpaka saa kumi hatukuona polisi wala nani kutusaidia. Mungu mkubwa...
Ninavyofahamu mtoto kama ananyonya vizuri na mama yuko tayari kumnyonyesha of course, mama anyonyeshaye hawezi kuona siku zake (normal montly mp). Na kama mama haingii kwenye mp ina maana hawezi beba mimba. Hiyo ni kweli, na nimeshaiprove beyond doubt. Wewe mpe mkeo lishe nzuri na muencourage...
Kama malipo yataenda kwa huyu mheshimiwa kwanini tusimpigie magoti atuonee huruma watanzania jamani?? nafikiri nae ni binadamu na nahisi (sina uhakika) atakuwa na chembe ya huruma. Tukienda ni kina mama wajawazito, watoto waishio mazingira magumu, wanafunzi wanaokaa chini kwake huku machozi...
GeniusBrain, bila shaka haukuwepo kwenye hayo mazingira. Jamani tuache kuwazushia watu. Huyo Lema unayemsema sio Lema mbunge. Ninachofahamu hapo chuoni kuna kiongozi wa wanafunzi anaitwa Lema. Yawezekana aliyekuambia hakukufafanulia hilo.
Jamani, tuache ushabiki katika hili. Mimi nina mdogo wangu namsomesha na wala hapewi huo mkopo na hata mgomo hakushiriki. Angegoma ili iweje wakati hakupewa hata 0%? Lakini nimempokea jana sababu; samaki mmoja akioza wote wameoza!!! Yeye ameniambia na usiasa umo katika kufukuzwa kwao. Katoa...
Ni kweli yawezekana huyo baba amebadilika maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Ila pia kwa ushauri tuu, kama walikuwa hawapo wote kindoa ni bora wakapime kwanza ndo waendelee na maisha. Wanaume bwana, anaweza kujua anaumwa then akaja kumuua dada wa watu. Ni hayo tu.
Yaani ndugu yangu suala la kupata hati milki kutoka ardhi kuu ni kizungu mkuti. Haswa haswa kama ni hapa Dar si mchezo. Nimeanza process ya hati yangu mwaka jana mwezi wa tatu mpaka hivi naandika bado sijaipata hiyo hati. Kama unaanzia manispaa ya Temeke, duuh ni balaa. Mara utaambiwa file...
hii nimeipenda pia. Kwenye comment yako ya 'sio kwa watu kama FF' nimekuaminia baada ya kusoma comment yake. Duuh! Kama ulijua vile atakachoandika. hahahaa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.