Yaani mkuu haya magazeti yatahoji uchafuzi mkuu 2020, na hizo chaguzi zijazo. Tunajua CCM wamezoea vya kunyonga, na baada ya Utawala wa Magufuli, ndio kabisaaa hawajui kuchinja. Haya Magazeti yatawaumbua, na sitoshangaa yakifungiwa tena
Inashangaza sana kwamba kuna mamia ya wananchi wanashindwa kuchukua maiti za wapendwa wao kisa wanadaiwa gharama za matibabu. Kuna wengi ambao wanafariki kwa kukosa fedha ya kugharimia operesheni na tiba kwa ujumla. Upo sahihi mkuu. Serikali ilitakiwa kuchangia tu.
Hii inanikumbusha saluti...
Habari njema sana, nitaanza tena kununua magazeti. Itakuwa burudani kubwa kuwasoma tena akina KONDO TUTINDAGA, NARONYO KICHEERE, SAED KUBENEA, na wengineo. Hawa jamaa huwa hawaogopi kabisaaa kufukua kinyesi, mizoga na yooote yaliyoooza na kuvunda ila yamefichwa!!
Sikubaliani na mwelekeo wako wa kukiri kwamba ccm wana hoja pale wanapodai CHADEMA ni saccos ya Mbowe. Kinachotokea ndani ya CHADEMA sasa ni kama ilivyokuwa kwa ccm na Nyerere enzi hizo.
Unapokuwa na mmoja anayejitolea sana kwa chama, kukitumikia kwa nguvu zote, kutojitafutia mafanikio au faida...
Nilimsikiliza Zitto Kabwe, mmoja wa vigogo katika viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani hapa Tanzania, akitoa hotuba yake katika mkutano wa Baraza la Vyama vya siasa. Nilimsikia akimuomba Rais Samia, kwa unyenyekevu mkubwa, "asaidie" ili Mbowe awe huru.
Nilisikiliza pia majibu ya rais...
Umewahi kumsikia Profesa J katunukiwa PhD? Au uprofesa? Yeye kaamua tu kujiita kutokana na usanii wake. Hakuwahi kuvaa magwanda ya graduu ya chuo kikuu kama huyo msukuma.
PhD ya Msukuma ni kituko cha pekee, acha kulazimisha wa "kufanana na" Msukuma
Haya, kuna ile PhD ya Magufuli nayo ilizua mjadala, ambao ulizimwa baada ya mpingaji mkuu wa PhD hiyo kupotezwa jadi leo. Ben Saanane. Ya Jaffo sijaifuatilia binafsi, lakini tunaweza kuorodhesha hapa PhD zenye utata:
1) Dr. Magufuli
2) Dr. Msukuma Kasheku
3) Dr. Jaffo
Hivi ile ya Lyatonga Mrema...
Zipo sababu za msingi sana kuendelea na mapambano, hata katika mazingira magumu kiasi gani. Mosi ni kwamba hao wakandamizaji wanabadilika, ipo tofauti kubwa kati ya Mkapa na Magufuli, na Kikwete. Pia kuna haja ya kuwaanika madhaifu yao.
Halafu binadamu tuna tofautiana. Mimi mfano, toka utotoni...
Yaani wewe unaandika kuhusu mada ambayo huna hata ule uelewa wa mwanzo tu. Miradi mikubwa kama ya marekebisho makubwa ya uwanja wa ndege huendana na mikopo. Magufuli kakopa sana tu kwenye miradi mingi. Kosa lakevni kukopa sana mabenki ya biashara, kama ilivyo kwenye hii ishu ya ya Entebe, badala...
Naam, nia ya dhati wanayo, anayeharibu siasa za Tanzania ni maiti ya ccm. Ndio maana ccm huwa hawajibu ngumi za kisiasa za CHADEMA, sababu ccm ni maiti. Polisi na dola ndio wasemaji wao
Kilikuwa kikao cha ndani, lakini wanachama 15 wa CHADEMA waliswekwa ndani. Wakati ccm wanafanya mikutano ya hadhara nchi nzima bila tatizo. Lakini hapo sasa ndio ushangae, chama mmekizuia kufanya mikutano lakini mnakiogopa kama nini sijui.
Inaeleweka kwamba Kikwete ete
CHADEMA wamekatazwa...
Hiyo nayo propaganda tu. Miaka 3 mfululizo mvua zilikuwa nyingi mafuriko kila siku. Sasa kuna ukame maji ya kidatu lazima yapungue.
Enzi za Magufuli alilazimisha wenye viwanda wazime mitambo ili kuepusha mgao wa umeme.
Hii ndiyo ile hadithi ya fisi anamfuatilia binadamu, akiamini ile mikono inayokwenda mbele na nyuma, itadondoka apate mlo! Yaani kumbe mnamgwaya sana Lissu eeh? Sasa hamuambulii kitu. Hamjatosheka tu na akina Lijualikali, Mtatiro na kina Silinde? Lisu ni habari ingine kabisaaaa. Sahauni!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.