Benbulugu
JF-Expert Member
- Sep 14, 2016
- 801
- 1,170
Nnakupongeza sana kwa kuwaza Kisomi na kimkakati ,kongole kwako mtoa Mada on top of that naishauri serikali au nnaiomba serikali yangu pendwa mikataba ya serikali isiwe ya kudumu(permanent and pensionable kama ilivyo sasahivi bali iwe yamiaka kumi kumi au mitano mitano,kulingana na mahitaji ya mtumishi maana unakuta mtu katumikia let say miaka kumi na tano ashachoka kuitumikia serikali anataka kutoka ila anaogopa kuacha pension yake hivyo kupelekea kufanya kazi kimazoea ,Niheri kuwe na room ya wafanyakazi ku-exit waonapo kua wamechoka kuitumikia serikali ili kupisha damu mpya zenye uhitaji wa kuchapa kazi kuitumikia serikali yao.iwe kama mpishano tu wengine wanaingia wengine wanatoka hii huenda ikapunguza msongamano wa kundi lisilo na ajira ila pia waliochoka kuitumikia serikali walipwe madai yao kwa mda walipotumia serkali waende kulitumikia taifa kwa namna nyingine,sio kulazimishana hadi tufike miaka 60.Kuelekea siku ya wafanyakazi nchini Mei mosi, vijana ambao wanahitimu elimu ya vyuo vikuu tunaomba Serikali yetu chini ya Rais wetu mpendwa Mama Samia na timu yake yote tunamuomba jambo moja nalo ni;
1. Umri wa kustaafu upunguzwe uwe miaka 45 hiari na 55 iwe lazima, badala ilivyo sasa kuwa 50 hiari na 55 hadi 65 lazima.
Suala hili la umri wa kustaafu limekuwa kikwazo kikubwa kwa upatikanaji wa nafasi kwa kundi kubwa la vijana wanao hitimu vyuo vikuu.
Utafiti unaonyesha kwenye idara mbalimbali za serikali kuna wazee wengi ambao tayari wamechoka, hawana tija, hivyo ni vyema umri wa kustaafu ukapunguzwa ili kupisha vijana nao walitumikie taifa lao.
Tunaomba pendwkezo hili lizingatiwe.