Hili jambo ni very technical; kupanga ni kuchagua! Hoja hapa ikiwa ni aina ya uchumi unauojenga!
JPM na serikali yake tayari wameshachukua njia; kwamba wanajenga central economy; yaani Macroeconomics!
Tatizo ni pale wanapoonekana kusahau kabisa Microeconomic side. Kwa wale wasiofahamu masuala ya uchumi; majority tunaendeshwa na microeconomic side of economy!
Tukirudi kwenye VAT in Tourism. Mosi, VAT yenyewe moja kwa moja inajenga Macroeconomic side. Tukija kwenye impact; VAT itapunguza kwa kiasi kikubwa wale Watalii ambao Magembe kawaita Maskini. Hawa ni wale Watalii ambao wakiingia nchini wanafikia hotel za bei rahisi; ndio wale unakutana nao Posta wanakula mahindi ya kuchoma, ukienda public beach unawakuta; wanakamata madada poa, n.k na kote huko wanachangia sana microeconomic side ambayo ndiyo inaendesha uchumi wa cku kwa cku wa wananchi!
Hawa Watalii wa VAT ni wale ambao wakifika wanafikia Serena Hotel! You'll never ever find them in public places! Hutawakuta na mahindi ya barabarani! Tena usishangae wengine wakafikia Double Tree na wakaondokea Double Tree hata Mjini wasiguse!
Hawa Watalii wa VAT wana faida zaidi kwa wenye mahoteli na hiyo VAT lakini economic impact yao ni ndogo compared kwa Watalii "maskini!"
Kutokana na ukweli huo, naunga mkono Kenyan strategy compared na hii strategy yetu! Strategy yetu ingekuwa economically viable only if tungekuwa tumefikia highest number of tourists wanaoingia nchini kwa kuangalia vivutio tulivyo navyo! Ukitaka kuelewa chukua watu X na Y. X ana hotel yenye vitanda 20 na hana eneo la ziada! Y nae ni hivyo hivyo lakini kuna vyumba vya ziada 10 visivyo na vitanda lakini wote kila cku wanakataa wageni kv hotel zinakuwa zimejaa!
Ktk mazingira kama hayo, X anaweza kuweka VAT/'kuongeza bei kama njia ya kuongeza mapato lakini Y hatakiwi kufikiria kuongeza bei kama njia ya kuongeza mapato wakati kuna vyumba 10 vipo underutilized! Badala ya kuongeza bei na kuhatarisha idadi ya wateja, rational decision kwake ni kuongeza vitanda ili aongeze mapato kutokana na kuongezeka wageni!