soma post yangu, nilikwenda kwa wale jamaa pale victoria ndio wakasema ni kirusi, pia my heading ilikuwa na kweshen mak [yaani alama ya kuuliza] naomba mods wairudishe ili ibebe maana halisi, yaani nalalamika na kuuliza at the same time!
Nimekupata mkuu.
Hiyo kweli inakera.
Mimi nginekushauri utafute jinsi nyingine ya kuingia kwenye internet. Kila mwenye tatizo hilo akifanya hivyo, then labda Voda wataliangalia kwa jicho tofauti. Ila mkiendelea kuwapa pesa kwa hizo dakika moja moja, mnakuwa hamjitendei nyie haki, na wala hamtendei haki maendeleo ya kitechnolojia nchini.
Kwa maelezo ya ThinkPad, kama target ya huyo kirusi ni any dialup connection, na huyo worm hajaletwa na Voda, then sidhani kama ni responsibility ya Vodacom kukusaidia. Mimi nilidhani labda huyo Z-Connect anakuja na CD uliyopewa na Voda.
Ila jinsi ya kuifanya Voda ijisikie kusaidia ni kuachana nayo na kutumia connection ya kampuni nyingine ambayo haiko affected na huyo mdudu. Wateja wakipungua pungua kwa sababu hii, then labda Voda watajisikia kusaidia.
Kumbuka hilo ni tatizo lako na sio la Voda. Computer yako ndiyo ina kirusi.
Mwisho sasa nijaribu kukusaidia:
Unatumia operating system gani?
Kama yote yameshingikana, na hauna mtu technical anyeelewa cha kufanya, jaribu ku-reinstall operating system. Hiyo inaweza kusaidia kumuondoa kwa muda. Halafu hakikisha computer yako inapata updates mara kwa mara. Hii inasaidia kuziba holes zinazotumiwa na hao wadudu kuingia kwenye computer yako bila wewe kujua.
Cha muhimu nakushauri wewe na wengine kutumia computer kwa kufikiria. Virus huwa kwa kawaida hawaingiii kwenye computer isiyotumika. Ni matumizi yako na matendo yako ambayo mara nyingi yanakaribisha hawa jamaa.
Kwa hiyo sioni kwa nini asirudi tena kama ukiendelea kufanya yale yale yaliyomleta huyo kirusi.
Watu tunakumbuka kila mara kufunga mlango wakati tunaondoka nyumbani. Mara nyingi tunakumbuka kushusha vioo na kufunga milango ya gari baada ya kupaki. Tena saa nyingine tunajaribu kuufungua mlango kuhakikisha kwamba kweli umefungwa.
Cha kushangaza hatufanyi hivyo hivyo kwa computer. Kupeleka gari service hatusahau, lakini ku-update computer au anti-virus tunaona ni kero. Halafu tanashangaa kwa nini hawa virusi wanakuwa tatizo.