Ni udhalilishaji mkubwa wa wanawake na mama zetu kwa ujumla.nimesimama pembezoni mwa barabara masubiri daladala mara naona linapita landrover la polisi linawapeleka dada zetu mahakamani,kisa wanafanya biashara ya ukahaba.sasa ninachohoji ni inakuaje au sheria inasemaje kwanini hakuna wanaume wanaoshikwa au wanaotuhumiwa kwa biashara ya ukahaba kama ilivyo kwa wadada zetu? Inakuaje wao tu ndio wanaotuhumiwa pasipo mtuhumiwa wa upande wa pili? Nakereka sana ninapoona hakuna wakulikemea hili.madawa ya kulevya ukishikwa nayo unauza au unatumia mojakwamoja unachukuliwa hatua,baki pia muuzaji na mvutaji pia hivyohivyo,sasa kwenye hili la ukahaba kwanini liwe la upande mmoja??