Tunamchekelea kuwa kafanya uwamuzi wa kiume na kutoyumbishwa na tunapiga makofi na kishangilia kuendelea kuwa jiwe hasa ushirikiano wa kimataifa kwa kujiona tuna kila kitu na bila sisi wao hawawezi kifanya kitu ndio imani inayotawala mnele ya mtukufu.
Mtukufu hataki vikao vya kimataifa na hataki kuhudhuria bali kajifungia dar na mwisho wa siku kaenda kujifungia kwao na kulelewa na mama kwa kigezo nyumbani ni nyumbani kila mtu ana kwao kama unaona wivu nawe nenda kwenu.
Majirani wanamwita haendi na kajifungia ndani na yuko kinyume na viongozi wenzake japokuwa wamejipendekeza kumwalika lakini kama alivyo ukimshauri mdio unaharibu kabisa.
Tumejigeuza mabeberu kwa majirani zetu kwa kisingizio watatufanya nini? Si wanatutegemea kwa bandari na chakula wafanye wafanyanyo mwisho watakuja wenyewe ndio kauli za sasa toka tanzania kwenda kwa majirani zetu.
Sasa majirani wameunda shirikisho lao na wanaanza kutuhama na kwenda waonako kuna maelewano na diplomasia iliyokomaa.
Hizo tozo na kodi zinaelekea kwingine sie tichape kazi mwisho tutazitapika kodi za nchi waliotukimbia kwa kusifia tusivyovijua ili bajeti iende