Salma Kikwete Cheo chake ni kipi kikatiba?

Capital

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,455
1,045
Wanajf, bado nashangaa kuhusu yanayotokea mke wa JK ana cheo gani kikatiba? Maana sasa watz tunafanywa kama misukule, hii mijitu inavunja katiba ya nchi wazi wazi na haiogopi. Mke wa rais, kiutaratibu hatambuliki na hivyo ni kama raia mwingine, hapaswi kupata priveldges kama rais, labda katika utawala wa kifalme. wataalam hebu tuwekeni sawa


 
Huu ni usultan ndugu zangu.Leo kaingia mkoani katavi na hakuna kazi iliyofanyika tangu jana yaani wakurugenzi na wafanyakazi wote wapo huko kiwanjani wameenda kumpokea.Pia naomba mnisaidie ndugu zangu.Je ziara zake huwa zinagharamiwa na nani?
 
Ingekuwa wewe ungefanyaje ndo mkeo ana nafasi yake katika chama, na pia anamiliki mfuko wa WAMMA si anatembelea wana mfuko na wanaccm wenzake? wewe ni chadema nin nini? Tuache hayo huo ni utani tu.

Kimsingi hana sifa ya kutembelea nchi (wilaya, mikoa, tarafa hata vijiji kwa kupewa heshima kama kiongozi wa nchi katika ngazi fulani. Utaona anapokrelewa ikulu ndogo na kupewa heshinma zote na kukagua miradi ya serikali kwa kisingizio kuwa yeye ni mjumbe wa nec ya ccm na ccm ndo chama tawala. Hana jipya wala katiba haumruhusu, ni upambe tu na ulimbukeni wa viongozi wetu katika ngazi nazotembelea-angefanya kama chama -hapo sawa kwa kuwa ni mjumbe wa nec ccm.

Hapa TZ si unajua hata baba yako akiwa waziri nawe pia inakuwa nusu waziri? utafanya lolote mtaani kwa jina la waziri husika (babako) bila kuulizwa na watendaji wala polisi-sembuse mke wa rais? OLE WAKO, usiendelee kuhoji -utasweka ndani halafu upatiwe jarada la mauaji ya Kanumba bure
 
Ameenda kama Mwenyekiti wa WAMA, hao walioenda kumpokea ni kiherehere chao, na kama wametumia rasilimali za serikali wanaweza kuchukuliwa hatua (lakini wachukuliwe na nani?)
 
Kama CCM itabaki madarakani miaka mingine kumi tutegemee na wake za wakuu wa Wilaya na Mikoa kuanza kukagua shughuli na ofisi za kiserikali
 
Capital, cheo cha Salma Kikwete ni MWALIMU WA ZAMU
 
Last edited by a moderator:
Ameenda kama Mwenyekiti wa WAMA, hao walioenda kumpokea ni kiherehere chao, na kama wametumia rasilimali za serikali wanaweza kuchukuliwa hatua (lakini wachukuliwe na nani?)

Umenena!! Ni kujipendekeza kwa hao viongozi ili mama akitoka safari aende kumwadithia baba na watu wapandishwe vyeo na kadhalika!! Hata kama angekuwa mjumbe wa NEC, kwani mikoa anayotembelea hakuna wawakilishi wa NEC wanaoweza kukagua hizo miradi??

Ni Tanzania tu haya hutokea!!
 


kama hujui nafasi ya mke wa rais kikatiba nakushauri rudi shule or do your self a favor kaisome katiba...! katiba hujaisoma unadai waendeshwa kama msukule ... watu bana ...
 
Ana cheo cha ufirst lady jamani, si cheo kidogo hicho!
Ila hilo la kupewa taarifa za maendeleo lbda kaona mumewe hafuatilii na wale alio waweka awaamini so ameamua kuusaidia ubavu wake kufuatilia yale malengo yaliyokusudiwa.
 
Hivi Salma akipewa talaka na JK (mfano tu), hizo taarifa anazosomewa na Mkuu wa mkoa atazipeleka wapi?
Anasomewa taarifa na mkuu wa mkoa? That is ridiculous, mkuu wa mkoa anamsomea salma taarifa zinazohusu nini? kama ni ya kweli haya basi watanzania tukubali kwamba sisi ni mazuzu kupitiliza. Kwa style hii, na Ridhiwani naye atakwenda mikoani na kupolekewa na wakuu wa mikoa na kusomewa taarifa za maendeleo za mikoa.

Haya yanatokea kwenye utawala wa Kikwete tu, sina uhakika kama yaliwahi kutokea kabla. Kama utawala wa Nyerere hatukumsikia kabisa mama Maria Nyerere hadi pale alipofariki Nyerere ndipo tulianza kumsikia Maria, ni kwa vipi utawala huu umejaa mama Salma all over, halafu anapokelewa na viongozi wa serikali? Inakera sana.

Na hapo watu mnalalamika ni kwanini nchi inaendelea kuwa na madeni ilihali kinachofanyika hakionekani. Hivi hela ya mama Salma kuzunguka mikoani imetoka wapi kama siyo hiyo mikopo inayoongezeka usiku na mchana? Maana tunajua bajeti ya Ikulu haipitishwi na bunge, so ni wazi kwamba Kikwete anaweza kukopa tu huko na kuja kujipangia bajeti bila kuipitisha bungeni.

Mbona hatujawahi kusikia bunge likipitisha hiyo mikopo?
 
Hakuna linaloshindikana Tanzania, Mama anamsaidia Baba kuweka mambo sawa ili aweze kutimiza ahadi kwa wananchi
 
Heading yako umeuliza swali halafu cha kushangaza kwenye maelezo yako ukalijibu hilo swali. Sasa unataka watu/wataalamu wakueleze nini zaidi wakati jibu umelitoa mwenyewe.
 

wanashindana kusafiri yeye na mumewe.zinazotumika ni pesa zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…