pole, Baby yaweza pia kuwa mlichotumia kunyoa nywele au ingewahiwa na dawa iliyokubali asingefika hapo. Pia ni ngozi yake ni mengi huwezi jua.
Yenye Hydrocortisone 1% w/w
kama hydrocortisyl skin cream najua ya 15g tube ni kadogo labda wana kubwa ila haijalishi. Pata ushauru wa DK kwanza.
Wengi utumia kwa sehemu ndogo ndogo kuondoa mkauko au madhara na yanaisha, ila kwa baby naona sasa imesambaa kwa hiyo ni kujaribu kwa ushauri mzuri, hiyo itaje tu ukienda kwa dk wa ngozi pia na ataamua mwenyewe ipi bora akimuona baby. Wapeleke wote.
Najua mtu mtoto wao ilichukua muda hadi alipofika miaka minne kupona na walijaribu kila kitu, iliyomfaa akapona now miaka 10 yupo free kabisa ila wazazi waliangaika kila cream/ dawa inabidi utumie kwa wiki 2/3 kabla ya kubadili ndio utajua inafanya kazi au la.
Ukienda kumuona dk wa ngozi hakikisha haujampaka chochote yaani mafuta. Pia acha kumpaka mafuta sasa ukiweza,
Watapona usiwe na wasi muhimu fata masharti na usichokeeee kabisa, waweza badili dk ykiona miezi inaenda no mabadiliko, kuwa mvumilivu sana.