sweetlady;pole swthat, wanaume ndivyo walivyo mwaya, hawabebeki, hawapendeki, hawana shukrani n.k. Tafuta mahal nenda kapumzishe akil, utapata sukar bure
Maneno ya mtu aliyeumizwa hayo. Inaonekana ni wanawake tu ndo wanaumizwa kwa mtazamo wako wakati kuna wanaume hapa wanalalamika kila siku hapa jamvini. Usipobadili mtazamo wako kwa wanaume utaendelea kuumia kila siku maana hutokuwa na upendo hata kwa yule atakayeonyesha kupenda.
Pole lakini, ndo maisha katika dunia ya mapenzi. Kuna walio na furaha katika mahusiano, Kuna wale wanaoona maisha yao ya mahusiano kama jehanamu. Hata walio na raha kuna changamoto zake maana kukoseana kupo pia. Jambo la msingi ni kutatua tofauti zenu na kusonga mbele.
Back to the topic; Pole dada DA, ni hasira za mda zitaisha japo kwa sasa unaona km hukusitahili kutendewa hivyo ulivyotendwa kwa mtu uliyemwamini na kumpenda.
Jipe moyo- ni mawimbi katika maisha yatatulia na utasonga mbele.