Hivyo vidude vinauzwaga bei sababu ni Honda original kutoka Japan. Ila ukijichanganya ukakinunua hupati mtu wa kumuuzia bei uliyonunulia. Umemueleza ukweli, kumpata mtu wa kukupa milioni 3 hata 2 Kwa hicho kibatavuzi ni mtihani sana. Wanunuzi ni waarabu na wahindi wapo mitaa ya Upanga na Kisutu na huwa wanarithishana wao kwa wao hawaamini kitu alichotumia mbongo. Atatukana ila huo ni uhalisia. Watu wananunua TVS na Boxer mil. 2.6 baada ya miezi 4 au 6 hawapati wa kuinunua Kwa mil.2 Sasa hicho kibatavuzi used cha kuuzia sura utamuuzia nani 3.3!!????