ufumawicha
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 510
- 213
Ni mwaka wa 22 ninasumbuliwa na tumbo.Mwanzoni ilikuwa ni mara amiba,minyoo na kichocho cha tumbo!Kila nikitumia dawa napata nafuu kwa wiki moja au mbili kisha gwaride linaanza upya.Mei,2015 nimehamia mbeya lakini hali inaendelea!Cha ajabu nimepima hapa na kujibiwa nina madonda ya tumbo.Nikawaona wataalamu wa tiba lishe pamoja na kuwalipa sh.600000/=Hakuna nafuu sasa naishiwa nguvu mwilini naweza hata kuanguka!Mwili unauma sana,mgongo shingo na kiuno ndo usiseme.Imebidi hata kulala niwe nalalia tumbo vinginevyo maumivu ni makali sana!Nipeni ushauri please!!Naomba kwa jinsi nilivyo serious msiweke utani kwenye hili suala langu!
Pole ndugu,japo sijui imani yako lakini nakushauli unapoendelea na matibabu mfate mtumishi wa MUNGU akufanyie maombi,yamkini kuna mambo ya giza pia umeyakumba mahali,kimbia Arusha na umtafute mtu anaitwa Christopher Mwakasege akufanyie maombi.Ni mwaka wa 22 ninasumbuliwa na tumbo.Mwanzoni ilikuwa ni mara amiba,minyoo na kichocho cha tumbo!Kila nikitumia dawa napata nafuu kwa wiki moja au mbili kisha gwaride linaanza upya...
itakuwa una presha nenda hosp. kucheki zaidi, BTW pole sana
tumia juice ya limao sana au weka kwenye chai.........
kuna matatizo mengine ya tumbo hayanaga tiba ili yanakua managed.
Netragen! Netragen! ni dawa ilikuwa inatangazwa kuwa kiboko ya vdonda vya tumbo ifuatilie inaua H.pyroli wa ulcers.
Kama utaweza kufika siku ya Jumamosi pale Mwanjelwa stand ya daladala KABWE fika Jumamosi kunasemina nzuri za afya. Ukifika nitafute kwa namba 0763797853